Tupia uongo uliodanganywa ukiwa mdogo na wazazi wetu.

Tupia uongo uliodanganywa ukiwa mdogo na wazazi wetu.

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Wangu ni huu

Kinyonga akiwa anazaa/kujifungua basi anapasuka na kufa ndipo mtoto anatoka nilikuwa naumia sana akili sasa mtoto wake anatunzwa na nani ikiwa mama lazima afe!!

Mamba akihisi njaa kama hajala na hana uhakika wa kula siku hiyo anaacha mdomo wazi nzi wanajaa kufuata harufu ya mdomo wake unaonuka basi anaufunga kisha nzi wanakuwa chakula chake

Mwingine

Mama aliniambia watoto wachanga wanaokotwa mtoni mida ya usiku kuna siku nilitoa woga nilishuka mtoni usiku saa mbili nione watoto maana mama aliniambia wanakuwa wengi mzazi unajichagulia tu cha ajabu sikuona nilipomuuliza akaniambia wameisha wao peke yao ndo wanapewa taarifa.

Wazazi ni noma wa kipindi kile 🤣🤣[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Walikuwa wakinisimulia(danganya) sana uwepo wa shing'weng'we(mazombi).
 
1. Watoto wananunuliwa
2. Wanaume hasa watu wazima hawajambi
3. Ukila una imba imba utakuwa muongo ukubwani
4. Kupiga mluzi usiku unawaita nyoka na wanyama wengine wakali (kwetu kiijini mjue)
 
1. Watoto wananunuliwa
2. Wanaume hasa watu wazima hawajambi
3. Ukila una imba imba utakuwa muongo ukubwani
4. Kupiga mluzi usiku unawaita nyoka na wanyama wengine wakali (kwetu kiijini mjue)

Hapa hata mm walihi kuniambia hiv
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hawakukudanganya, ni uzembe wako tu.
Hebu kuwa rais bwana utupunguzie bei ya bia.
Sasa hivi ni RAIS pia....

Najulikana kama 'rais wa kaunta'
Huwa siwezi kunywa bia nikiwa sijakaa kaunta kabisa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom