Tupike chapati za maji (yaani za kumimina)

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Kwanza utaanda unga wako wa ngano kisha kitunguu na karoti kama una penda hoho uta weka, kitunguu kisage usikate na hoho saga kwenye vile vidude vinauvyo uzwa buku buku, baada ya hapo uta vichanganya na unga kisha uta weka maji polepole.

Baada ya hapo uta weka sukari kidogo na chumvi kisha yai kisha changanya mvhanganyiko wako hakikisha usiwe mwepesi uwe mzito kiasi

Baada ya kuona mchanganyiko ume kuwa mzito utaanza kupika chota kidogo kidogo weka kwenye flampeni na uanze kuzungusha ili litokee duara kama hivi

Baada ya hapo utaweka kwenye sahani au poti ina tegemeana na unavyo penda wewe mimi nimeweka kwenye sahani kama hivi

Una weza kula na kinywaji chochote mimi nimetumia mtindi na mboga za majani huo ndio mlo wa usiku

Wapenzi wa Man U leo tunalala na viatu kwa furaha
Kama wewe ni yanga na shabiki wa man u leo kula vizuri ushindi uko mikonon mwetu
 
Hongera mwachi zinaonekana vizuri.

Mi sipendi hii kitu.

Huwa nawapikia, ile ya mwisho ndio najipikia mwenyewe naikaushaaaa naila ikiwa bado ya moto, zaidi ya hivyo siwezi πŸ˜…
 
Hongera mwachi zinaonekana vizuri.

Mi sipendi hii kitu.

Huwa nawapikia, ile ya mwisho ndio najipikia mwenyewe naikaushaaaa naila ikiwa bado ya moto, zaidi ya hivyo siwezi πŸ˜…
Aajahaha una penda zile zakuungua zinakuwa kama kau kau sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…