Tupike makande

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hope mpo
Vyedi kabisa

Jana nilikuwa na hamu ya makande nikaamua kuyachemsha jana usiku wakat naangalia tv nikawasha jiko la mkaa nikaweka makande yakawa yanaiva pole pole mda wa kulala ulipofika nikajaza maji ya kutosha nikasepa

Leo nimerudi zangu nikaanza maandalizi yangu yangu

Nika andaa karoti hoho na kitunguu maji baada ya kumaliza nika chukua sufuria yangu inayo tosha nilijua makande kidogo kumbe mengi bhna nikaweka mafuta vizur baada ya mafuta kupata moto nikaweka kitunguu

Baada ya hapo nikaikaanga karoti vizuri ili nipate ile rangi ta karoti kande zangu zisiwe nyeupe

Baada ya kuona karoti zimekuwa kama vile nataka nikaweka hoho
Then nikaja kuweka sasa makande yangu yalikuwa mengi sikutegemea ase

Baada ya hapo nikaweka maji kidogo ilo nipate mchunzi nikaweka na chumvi kidogo kwenye chumvi kuwa makini weka kidogo kidogo unaweza ukaweka nyingi mwisho wa siku chakula ulikuwa na hamu nacho ukakichukia tena hamu ikakatika tu kisa chumvi

Baada ya hapo nikachukua nazi yangu nikaweka yote huwa natumia mara tatu ila leo nimeweka yote kutokana na uwingi wa chakula

Baada ya kuweka nazi nikaacha itokete kidogo vizuri nikaipua

Hapo zingine nilikuwa nimepunguza nimeweka kweye poti. Mlo uhu unaweza ukapika jumamos kwa wewe bachela kama siku iyo unafanya zako usafi unapika vizuri tu usiwe na haraka

Makande mengi sana naona kesho nitabeba nipoenda kwenywe maangaiko nikale na wenzangu
 

Attachments

  • 1739974263621.jpeg
    489.2 KB · Views: 6
Nimeyamiss
Kesho napika
 
Hapo sasa upate na orange juice ya baridi unaweza ukatafuna vidole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…