Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni shabiki wa Yanga kabla ya kuandika ninachotaka kukiandika hapa.
Tukirudi kwenye mada, TFF kama shirikisho la soka hapa nchini, ni wazi limeundwa kwa mujibu wa sheria na shughuli zake zinafahamika na bila shaka lina mipaka yake
Kwa misingi huo, si kila tukio linalohusu soka linasimamiwa na TFF mengine yako katika ngazi za vilabu na yanaishia katika ngazi za vilabu na wala hayahitaji idhini wala baraka za TFF.
Kwa msingi huu pia, naomba kufahamishwa kama mechi hii ya kilele cha siku ya wananchi TFF wanahusika? Na kama wanahusika, uhusika wao ukoje?
Japo Manara kasema kaalikwa kama MC, binafsi naona ana hoja zaidi ya hiyo ya kujitetea iwapo TFF watataka kumchukulia hatua.
Sheria huwa zina mambo ya ajabu sana na msije kushangaa Manara anaibuka kidedea akitafuta haki yake katika vyombo vingine vya kimataifa vinavyosimamia maswla ya uendeshaji wa soka duniani.
Narudiia, Manara atakuwa amepata ushauri wa kutosha na pia viongozi wa Yanga watakuwa wameshirikishwa na kutoa baraka kwa Manara kuingia uwanjani na kufanya alichofanya.
Pia, uwepo wa Kinana pamoja na picha na mabango yenye sura ya Mama Samia, ni dalili mojawapo ya influence ya kisiasa kutumika kumlinda Manara iwapo TFF watataka kumchukulia hatua.