Tupo Karne ya 21: Kwa Nini Mfumo wa Benki Ukikata Pesa Kimakosa, Mteja Ndiye Anayeumia?

JJoh

New Member
Joined
Sep 1, 2012
Posts
2
Reaction score
3
Hello wana JF,

Bwana, mimi ni mteja wa muda mrefu wa hizi benki zetu, lakini kuna jambo nimekutana nalo hivi karibuni limenipa ukakasi sana. Najiuliza, tupo mwaka gani huu? Teknolojia imepiga hatua kiasi hiki, lakini bado mteja anaweza kukatwa pesa kimakosa na akahitaji kupitia mchakato mrefu kiasi hiki ili kurejeshewa fedha zake?

Nilifanya malipo ya Control Number kupitia SimBanking ya CRDB. Muamala ukawa una-fail. Nikajaribu tena mara mbili, kila mara transaction inafika mwisho lakini inaonekana kama imegoma, na Control Number yenyewe haionyeshi kuwa imelipwa.

Baada ya kuona hivyo, nikaamua kuacha SimBanking na kutumia Mixx by Yas kufanya malipo hayo. Safari hii malipo yakafanikiwa na Control Number ikalipwa.

Baadaye ndipo nikagundua kitu kingine cha kushangaza: CRDB walikuwa wamenikata pesa mara tatu!

Kwa mfano, kama Control Number ilikuwa Tsh 1,000, badala ya kukatwa Tsh 1,000 mara moja, nilikatwa Tsh 1,000 mara tatu, jumla Tsh 3,000.

Hapa ndipo nikaanza kujiuliza, mfumo ulifeli upande gani?

Nilichofanya ni kuwasiliana na benki kupitia simu, email na online chat kuwaeleza tatizo. Kwa sababu hata kwa akili ya kawaida, kama Control Number hiyo tayari imelipwa, inapaswa kuwa na validation kwamba haiwezi kulipwa tena. Hasa Control Numbers za taasisi kama DSE (Dar es Salaam Stock Exchange).

Lakini badala yake, mfumo unashindwa kufanya transaction, halafu baadaye unaendelea kukata pesa kwenye account ya mteja mara kadhaa?

Nilipopeleka malalamiko yangu, nikaambiwa niende tawi la benki kuwasilisha tatizo.

Nikawauliza swali rahisi tu:

Mfano ningekuwa nje ya nchi, nikafanya transaction, mfumo ukafeli na benki ikanikata pesa mara tatu kimakosa, halafu nikarudi Tanzania baada ya mwaka mmoja au miwili—ina maana ningesubiri miaka miwili ndipo nirudi tawi kuomba kurejeshewa pesa zangu?

Hapo ndipo unajiuliza kama kweli mifumo yetu imejengwa kwa ajili ya kumrahisishia mteja maisha au imetengenezwa ili kila tatizo limrudishe mteja kwenye tawi.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba bank statement yenyewe inaonyesha wazi kabisa pesa imekatwa mara tatu, wakati Control Number husika imelipwa mara moja tu.

Kwa hiyo taarifa zote zipo.

Transaction ipo.
Statement ipo.
Control Number ipo.
Payment status ipo.
Na kosa la mfumo linaonekana.

Lakini bado mteja anatakiwa afunge safari, aende tawi, aandike barua, halafu asubiri.

Na mimi kwa kuwa nilikuwa ndani ndani, nililazimika kutumia muda na gharama kusafiri hadi mjini kwenda benki.

Nikaandika barua ya kwanza tarehe 24/08 nikielezea tatizo na kuomba kurejeshewa fedha zilizokatwa kimakosa.

Mpaka tarehe 13/09, pesa hazikuwa zimerudi na sikupata feedback yoyote.

Nikaandika tena barua nyingine tarehe 14/09. Baada ya siku mbili nikarudi tena tawi kuulizia. Nikaambiwa tu kwamba barua imeenda.

Sawa, lakini imeenda wapi? Imefanyiwa nini? Inachakatwa na nani? Na nitarejeshewa lini?

Hapo ndipo ninapoona kuna tatizo kubwa zaidi ya transaction yenyewe.

Tatizo sio tu kwamba mfumo ulikosea. Tatizo ni mfumo wa kurekebisha kosa unapokuwa umeshindwa.

Tunaweza kuelewa kwamba teknolojia inaweza kuwa na technical failure. Hakuna mfumo usioweza kupata hitilafu. Lakini taasisi kubwa inapaswa kuwa na mfumo wa automatic reconciliation, reversal na refund pale transaction inapofeli au inapobainika kuwa mteja amekatwa zaidi ya kiasi kinachotakiwa.

Mteja hapaswi kuwa ndiye anayegundua kosa, afuatilie kosa, aandike barua, asafiri hadi tawi, halafu tena afuatilie majibu ya kosa ambalo hakulifanya yeye.

Na hapa ndipo swali langu kwa benki zetu linapokuja:

Kama mfumo wenu umeweza kunikata pesa ndani ya sekunde chache, kwa nini mfumo huo huo unashindwa kuzirejesha ndani ya muda unaofanana pale inapothibitika kuwa zimekatwa kimakosa?

Teknolojia inapaswa kumrahisishia mteja maisha.

Haiwezi kuwa ukitaka kutoa huduma au kukata pesa, mfumo unafanya kazi kwa sekunde chache, lakini ukitaka kurekebisha kosa la mfumo, mteja anaambiwa “fika tawi, andika barua, subiri.”

Hii ni karne ya digital banking, real-time transactions na automated reconciliation. Dunia imeshapiga hatua kubwa sana.

Kama nchi na kama taasisi, tunahitaji upgrade kubwa sana kwenye mifumo yetu na zaidi kwenye namna tunavyowahudumia wateja pale mifumo inapofeli.

Naomba kuuliza wana JF, wengine mmewahi kukutana na hali kama hii?

Transaction inafail, pesa inakatwa, halafu kurejeshewa pesa zako kunakuwa mchakato mrefu kuliko hata kufanya transaction yenyewe?

Tunaweza kuendelea kusema tuna digital banking, lakini kama mteja bado analazimika kwenda tawi kuandika barua ili kurekebisha kosa ambalo mfumo umefanya, basi kuna sehemu bado tunahitaji kujiuliza maswali magumu.
 
Unazani upo US?
Hii ndio bongo mzee, pamoja na kuandika kwa ufasaha bila kuacha maswali lakini sahau hao mabenki kubadirika, wana vichwa vigumu hatari.
 
Natamani hayo mabenki (taasisi za fedha) ziwe akaunt JF kama ilivyo kwa TANESCO, DAWASCO nk ili iwe rahsi kutoa majibu kwa changamoto zinazowkuta wateja wao

Hii ni platform nzuri sana na ingesaidia kuwafikia watu wengi ambao kwakweli hawawezi kila mara kufika katika matawi husika kupanga foleni na kutumia muda mwingi hapo kupata utatuzi wa changamoto zinazoweza kutolewa maelezo kwa dakika chache
 
Na ndiyo maana, hata wao wakimuwekea pesa mteja kimakosa, haraka sana mteja anapita nazo, ili wahangaike kufuatilia...

Cc: Mahondaw
 
Hello wana JF,

Bwana, mimi ni mteja wa muda mrefu wa hizi benki zetu, lakini kuna jambo nimekutana nalo hivi karibuni limenipa ukakasi sana. Najiuliza, tupo mwaka gani huu? Teknolojia imepiga hatua kiasi hiki, lakini bado mteja anaweza kukatwa pesa kimakosa na akahitaji kupitia mchakato mrefu kiasi hiki ili kurejeshewa fedha zake?

Nilifanya malipo ya Control Number kupitia SimBanking ya CRDB. Muamala ukawa una-fail. Nikajaribu tena mara mbili, kila mara transaction inafika mwisho lakini inaonekana kama imegoma, na Control Number yenyewe haionyeshi kuwa imelipwa.

Baada ya kuona hivyo, nikaamua kuacha SimBanking na kutumia Mixx by Yas kufanya malipo hayo. Safari hii malipo yakafanikiwa na Control Number ikalipwa.

Baadaye ndipo nikagundua kitu kingine cha kushangaza: CRDB walikuwa wamenikata pesa mara tatu!

Kwa mfano, kama Control Number ilikuwa Tsh 1,000, badala ya kukatwa Tsh 1,000 mara moja, nilikatwa Tsh 1,000 mara tatu, jumla Tsh 3,000.

Hapa ndipo nikaanza kujiuliza, mfumo ulifeli upande gani?

Nilichofanya ni kuwasiliana na benki kupitia simu, email na online chat kuwaeleza tatizo. Kwa sababu hata kwa akili ya kawaida, kama Control Number hiyo tayari imelipwa, inapaswa kuwa na validation kwamba haiwezi kulipwa tena. Hasa Control Numbers za taasisi kama DSE (Dar es Salaam Stock Exchange).

Lakini badala yake, mfumo unashindwa kufanya transaction, halafu baadaye unaendelea kukata pesa kwenye account ya mteja mara kadhaa?

Nilipopeleka malalamiko yangu, nikaambiwa niende tawi la benki kuwasilisha tatizo.

Nikawauliza swali rahisi tu:

Mfano ningekuwa nje ya nchi, nikafanya transaction, mfumo ukafeli na benki ikanikata pesa mara tatu kimakosa, halafu nikarudi Tanzania baada ya mwaka mmoja au miwili—ina maana ningesubiri miaka miwili ndipo nirudi tawi kuomba kurejeshewa pesa zangu?

Hapo ndipo unajiuliza kama kweli mifumo yetu imejengwa kwa ajili ya kumrahisishia mteja maisha au imetengenezwa ili kila tatizo limrudishe mteja kwenye tawi.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba bank statement yenyewe inaonyesha wazi kabisa pesa imekatwa mara tatu, wakati Control Number husika imelipwa mara moja tu.

Kwa hiyo taarifa zote zipo.

Transaction ipo.
Statement ipo.
Control Number ipo.
Payment status ipo.
Na kosa la mfumo linaonekana.

Lakini bado mteja anatakiwa afunge safari, aende tawi, aandike barua, halafu asubiri.

Na mimi kwa kuwa nilikuwa ndani ndani, nililazimika kutumia muda na gharama kusafiri hadi mjini kwenda benki.

Nikaandika barua ya kwanza tarehe 24/08 nikielezea tatizo na kuomba kurejeshewa fedha zilizokatwa kimakosa.

Mpaka tarehe 13/09, pesa hazikuwa zimerudi na sikupata feedback yoyote.

Nikaandika tena barua nyingine tarehe 14/09. Baada ya siku mbili nikarudi tena tawi kuulizia. Nikaambiwa tu kwamba barua imeenda.

Sawa, lakini imeenda wapi? Imefanyiwa nini? Inachakatwa na nani? Na nitarejeshewa lini?

Hapo ndipo ninapoona kuna tatizo kubwa zaidi ya transaction yenyewe.

Tatizo sio tu kwamba mfumo ulikosea. Tatizo ni mfumo wa kurekebisha kosa unapokuwa umeshindwa.

Tunaweza kuelewa kwamba teknolojia inaweza kuwa na technical failure. Hakuna mfumo usioweza kupata hitilafu. Lakini taasisi kubwa inapaswa kuwa na mfumo wa automatic reconciliation, reversal na refund pale transaction inapofeli au inapobainika kuwa mteja amekatwa zaidi ya kiasi kinachotakiwa.

Mteja hapaswi kuwa ndiye anayegundua kosa, afuatilie kosa, aandike barua, asafiri hadi tawi, halafu tena afuatilie majibu ya kosa ambalo hakulifanya yeye.

Na hapa ndipo swali langu kwa benki zetu linapokuja:

Kama mfumo wenu umeweza kunikata pesa ndani ya sekunde chache, kwa nini mfumo huo huo unashindwa kuzirejesha ndani ya muda unaofanana pale inapothibitika kuwa zimekatwa kimakosa?

Teknolojia inapaswa kumrahisishia mteja maisha.

Haiwezi kuwa ukitaka kutoa huduma au kukata pesa, mfumo unafanya kazi kwa sekunde chache, lakini ukitaka kurekebisha kosa la mfumo, mteja anaambiwa “fika tawi, andika barua, subiri.”

Hii ni karne ya digital banking, real-time transactions na automated reconciliation. Dunia imeshapiga hatua kubwa sana.

Kama nchi na kama taasisi, tunahitaji upgrade kubwa sana kwenye mifumo yetu na zaidi kwenye namna tunavyowahudumia wateja pale mifumo inapofeli.

Naomba kuuliza wana JF, wengine mmewahi kukutana na hali kama hii?

Transaction inafail, pesa inakatwa, halafu kurejeshewa pesa zako kunakuwa mchakato mrefu kuliko hata kufanya transaction yenyewe?

Tunaweza kuendelea kusema tuna digital banking, lakini kama mteja bado analazimika kwenda tawi kuandika barua ili kurekebisha kosa ambalo mfumo umefanya, basi kuna sehemu bado tunahitaji kujiuliza maswali magumu.
hizo ni changamoto za kawaida kwenye matumizi ya teknolojia gentleman. Pole sana.

In fact,
kuna urahisi mkubwa sana katika kufanya malipo ya ankara kieletronic. Na tunafanya hivyo mara nyingi sana bila kulalamika kwasababu tunafanikiwa na kuokoa muda na usumbufu wa kufika hadi benki.

Hata hivyo,
ni lazima tukubali kwamba hizo ni miongoni mwa changamoto zisizoepukika katika matumizi ya teknolojia. Changamoto ya kimtandao au changamoto binafsi za kibinadamu katika kufanya malipo kieletronic, zisifanye tukachukia yale mengi na mazuri sana tuliyoyafanikisha kwa mfumo huo huo wa malipo kieletronic.

Nadhani changamoto hizo zinafaa kuchukuliwa kama fursa ya wewe mteja kua makini zaidi wakati mwingine unapofanya automated transactions 🐒
 
Huo ni wizi tu, ma bank ya bongo ni wezi sana na hii ni kutokana bado wanatumia mfumo wa zama za kale za mawe. Wakati mamtoni wanafunga matawi ya banks na ma teller kukosa kazi huko bongo bado mtindo ule ule wa kizamani. Sidhani kuna mtu anaweza kunishawishi kufungua account bank bongo, labda kwa bank za Kenya zilizopo bongo lakini sio CRDB sijui wezi tu hao.
 
Back
Top Bottom