MKAKA WA CHUO 2
Member
- Aug 15, 2022
- 5
- 0
TUPO KATIKA DUNIA YA MASHINDANO, WASHINDI NA WATU WAO NDIO WATAPATA RAHA NA AMANI YA DUNIA.
Maisha yetu ya kila siku yanahusisha harakati tofautitofauti ambazo tunazifanya katika mazingira mbalimbali. Harakati hizi kwa kawaida huwa na lengo kuu moja la kutuingizia kipato ili tuweze kuendesha maisha yetu ya kila siku. Katika shughuli hizi ambazo tunajishughulisha mara nyingi huwa kuna watu wengine ukiachana na sisi wanaofanya shughuli hizo hizo. Ili kuhakikisha unafanikiwa katika shughuli yako, lazima uhakikishe ufanisi, usahihi na ubora wa shughuli hiyo unayoifanya.
Suala la kufanya shughuli mbalimbali katika jamii bila ya kuzingatia ufanisi na ubora wa shughuli yako, kunaweza kusababisha ugumu katika kufanikisha malengo yaliyowekwa katika mradi husika. Katika hali ya kawaida ni muhimu kuwafahamu watu wanaofanya shughuli kama unayoifanya wewe ili kujua ni namna gani wenzako wana hakikisha ufanisi katika shughuli zao, vilevile ni muhimu kuwajua watu kama hao ili uweze kujua ni vipengele gani huwa ni changamoto kubwa kwa wenzako ambazo wewe kama mtu mwenye kujishughulisha na shughuli husika uweze kujua kivipi unaweza kuepuka changamoto hizo.
Vijana wengi wakitanzania tunakumbwa na kasumbu ya kujiweka mbali na ushindani katika harakati zetu za kila siku, jambo hili ni kinyume kabisa na uhalisia wa dunia tuliyonayo hii leo. Dunia ya leo kila kitu kipo katika hali ya ushindani ni muhimu kujua hata kama wewe hautaki kushindana katika maswala mbalimbali ya kimaisha, lakini dunia inakuelekeza wewe kama kijana kushindana kwasababu asili ya dunia tuliyo nayo ni dunia ya ushindani, kutokukubaliana na mazingira hayo ya ushindani ni sababu moja wapo kushindwa kuendana na dunia ya leo, hivyo pia ni vigumu kuhakikisha mafanikio katika maisha yako, kwasababu wewe kama kijana hauwezi kuendana na uhalisia bora wa dunia yetu.
Ili kujua uhalisia wa dunia ni mashindano, angalia katika kila shughuli za kutafuta maisha lazima kutakuwa na mshindi na mshindwa au mpotezaji, kwamfano katika sekta ya elimu wewe kama mwanachuo hatakama ukisema hautaki kushindana lakini lazima uongozi wa chuo au shule utampata au kumtafuta mwanafunzi bora katika kila darasa, ikumbukwe wewe kama mwanafunzi au mwanachuo hauhitaji kushindanishwa lakini mfumo ndio umekushindanisha bila ya wewe mwenyewe kupenda.
Katika maisha haya kama kijana lazima ujue kwamba mashindano yapo kila siku na kila sehemu, hivyo unaposhindwa kuendana na uhalisia huu wa maisha lazima ujiandae kufeli katika harakati zako iwe ni biashara, elimu na kadhalika. Suala la ushindani ni jambo la msingi na la muhimu sana katika dunia yetu ya hivi sasa, kwasababu kutokana na ushindani baina ya pande mbalimbali au makundi mbalimbali jambo hili limeleta chachu ya maendeleo katika nchi zetu, kwa mfano vijana wanaposhindana kutafuta pesa na kufanya kazi kwa bidii, jambo hili hupelekea vijana hawa kukua kiakili na vilevile hali za uchumi wao zinaweza kuboreka.
Hivyo basi kama kijana wakitanzania ni muhimu kukubaliana na uhalisia wa dunia tuliyonayo na kukubali kuingia katika mashindano ambayo yanaendelea katika shughuli zetu tunazozifanya kila siku.
Ukiwa kama mshindani ni lazima ujue unaenda kushindana katika biashara yako na watu wa aina gani, lakini pia katika jambo la kuzingatia katika kushindana kwako ni kuhakikisha kushindana kwako kunakuletea tija na faida, sio jambo la sawa kushindana katika jambo linalokupatia hasara, ni jambo la ajabu kwa kijana kukata tamaa katika kushindana katika biashara zako, kwasababu mashindano haya yanalenga kukuongezea faida katika biashara yako.
Kuna namna mbalimbali za ushindanaji katika shughuli zetu za kila siku kwa mfano wafanya biashara wanaweza kushindana katika kupata wateja wengi katika maduka yao, yaani kila mmoja katika hawa wafanya biashara anataka awe na wateja wengi kuliko mwenzake, hapa tayari mashindano yameanza, sasa kuna watakao tumia matangazo kwa maandisha, wengine watatumia vipaza sauti, wengine watatumia watu wawapigie debe katika biashara zao lakini kuna watakao tumia vyombo vya habari kama vile redio na televisheni. Sasa huko ndio kushindana ili kupata wateja wengi katika biashara zao ili kuleta tija katika biashara.
Kama kijana mpambanaji lazima ujue kwamba hayo ni mashindano na lazima uwe tayari kushandana ili kujihakikishia faida katika biashara yako, unaposema wewe hushindani na watu, mwisho wa siku unaweza kushindwa kuendeleza biashara yako. Kwa upande mwingine mashindano yanaweza kufanyika katika ubora wa huduma zinazotolewa kwa mfano katika shule za watu binafsi, watu wengi hupeleka watoto wao katika mashule haya kwasababu ya ufaulu mzuri, kwahiyo wewe kama mmiliki au msimamizi wa shule fulani ya mtu binafsi lazima uhakikishe ufaulu wa shule hiyo unakuwa mzuri ili kuongeza ubora na biashara katika mradi huo wa elimu.
Kwa upande wa wakulima na wafugaji, ni muhimu kujua kwamba watu wengi katika nchi yetu wanajishughulisha na shughuli hizo mbili, hivyo ni muhimu kujua kwamba lazima mazao unayoyalima yawe na ubora mzuri ili yaweze kushindana katika soko la mazao wakati wa kuuzwa, vilevile wafugaji ili ujihakikishie faida katika shughuli yako hiyo lazima uendane na uhalisia wa dunia, hivyo ni muhimu kuhakikisha wanyama wako wanakuwa na afya na mvuto kwa wanunuzi, lakini pia kwa wanyama kama vile ng'ombe lazima ujihakikishie kwamba wanakupatia maziwa kwa kiasi cha kutosheleza ukilinganisha na gharama unazozitumia.
Kuna baadhi ya nyakati, katika mashindano ya kibiashara, baadhi ya wafanya biashara hushusha bei za bidhaa zao, suala hili lazima wewe kama kijana uwe nalo makini kwasababu na wewe unaweza kushusha bei ya bidhaa zako mwisho wa siku ukapata hasara, katika kushindana kwako ni muhimu kujua lengo kuu la mashindano yako ni kupata faida na siyo ili mradi kuuza bidhaa zako. Ndugu zangu wa tanzania, bila ya kushindana nchi yetu isingefika hapa. Tuhakikishe tunashindana ili kukuza uchumi wa familia zetu na nchi yetu kwa ujumla.
BY: MKAKA WA CHUO.

Upvote
0