Tupo Sahihi ama kuna Tatizo!

Tupo Sahihi ama kuna Tatizo!

Hivi wanawake mnawasomesha wa nini?? Hilo lilikuwa jukumu la wazazi wake... akukuzidi ndio kama hivo... asilimia kubwa ya wanaume wanaosomesha na kuwaendeleza wake zao wanaishia hapa....

Endelea kusali sana, Mungu atakusaidia
:confused2::confused2::confused2:
 
Pole sana Tikitimaji mkeo anaonekana ni mbinafsi sana ..
Mkalishe chini na umwelezi yale ambayo hupendezwi nayo kama ataendelea hivo unahitaji msaada wa wazazi wake ..
najisikia kukuhurumia sana
 
pole sana ndugu yangu, ndoa yako imegeuka ndoano, nashindwa kukushauri maana nimepata
maelezo ya upande mmoja tu, ningepata na upande wa pili ingekuwa safi sana......
wanawake ndugu yangu siku zote akishaona anaweza siamama mwenyewe huwa ni changamoto
kubwa kwenye ndoa, wachache sana wanaotambua mume ndo kichwa cha familia......
nakushauri uvumilie tu, ndo msaraba wako huo, nawe endelea na mambo yako kimya kimya
kama vile humuoni, usijihusishe wala kumuuliza mambo yake, naamini itamuuma sana, hata
ushauri usimpe, atarudi mwenyewe...
 
Hiyo ni dalili mbaya sana katika ndoa na naweza kusema kuwa ndoa yenu inapumulia mashine. Kaa na mkeo uongee nae kuhusu hizo issue na jinsi zinavyokukwaza mweleze kwa utulivu na busara ya hali ya juu sana na pia mwambie ndoa inawafanya kuwa mwili mmoja ndio maana ulimsomesha kwa kujinyima ili mfaidi matunda yake kama mwili mmoja anavyofanya mambo kwa ubinafsi na kushirikisha ndugu zake zaidi na wewe akikutenga si kitu kizuri na mwambie kuwa kinaweka ndoa yenu ktk mashaka makubwa

mwambie kuwa hilo tatizo linakuumiza na kukukwaza sana na limetia doa kubwa sna ktk ndoa yenu. Mweleze yote yaliyo moyoni ili si kwa kumsimamnga bali kwa kumuelimisha zaidi

Baada ya hapo kaa kimya kabisa angalia kama atajirekebisha au la, na kama asipojirekebisha siku moja waite wapambe wenu wa harusi waeleze, au wazazi wake au mshenga au mtu mzima yoyote anayeweza kumsikiliza na ukiona bado anaendelea siku moja mrudishe kwao kama wiki hivi akaweke akili yake sawa na mweleze kabisa kuwa naomba uende kwenu tabia zako zinaanza kunishinda

Ndoa yako iko hatarini sana wewe tu hujui ila nina uhakika kuna vingi anavifanya kwa kukuficha jaribu kuchunguza unaweza kukuta hata anajenga nyumba bila kukutaharifu na ukiona hicho kitu kimetokea nakushauri uachane nae mara moja hata kama mna watoto 10 mmezaa nae ni dalili mbaya sana kwenye ndoa ni zaidi ya kuwekewa sumu ufe

Mkeo ni mtu mbaya sana fanya maombi wakati unaendelea kuchukua hizo hatua
 
pole sana ndugu yangu, ndoa yako imegeuka ndoano, nashindwa kukushauri maana nimepata
maelezo ya upande mmoja tu, ningepata na upande wa pili ingekuwa safi sana......
wanawake ndugu yangu siku zote akishaona anaweza siamama mwenyewe huwa ni changamoto
kubwa kwenye ndoa, wachache sana wanaotambua mume ndo kichwa cha familia......
nakushauri uvumilie tu, ndo msaraba wako huo, nawe endelea na mambo yako kimya kimya
kama vile humuoni, usijihusishe wala kumuuliza mambo yake, naamini itamuuma sana, hata
ushauri usimpe, atarudi mwenyewe...
ushauri wako si mzuri unadhani akimchunia si ndio utakuta ameshajenga majumba na yeye kugeuzwa Bushoke ni bora amweleze mapema kabla hayajafika huko maana kuna watu wanamjaza ujinga mke wake na akiendelea atamjengea mkewe kiburi na baadae kudharaulika sana ni bora alianzishe mapema tu ili kama kuachana waachane mapema au kama kujirekebisha ajirekebishe sasa sio unaacha mpaka baadae kiburi kinakomaa baada ya kuwa na mali nyingi ambazo yeye hawezi kuzipata
 
Hivi wanawake mnawasomesha wa nini?? Hilo lilikuwa jukumu la wazazi wake... akukuzidi ndio kama hivo... asilimia kubwa ya wanaume wanaosomesha na kuwaendeleza wake zao wanaishia hapa....

Endelea kusali sana, Mungu atakusaidia

Ushawahi kuusikia wimbo wenye mashairi haya?
"Sisi wanaume tuna moyo wa huruma, tukiwa na gari mwanamke tunambeba... sisi wanaume wema wetu ni hasara, ukienda sinema mwanaume unatoboka ...mishahara yetu ni sawa, wakati mwingine yao mikubwa kushinda ya mwanaume..."

It doesn't matter how much the wife earns, the husband is expected to be bread winner. Kwa hiyo dhana ya 'cha mwanaume ni cha familia lakini cha mwanamke ni chake" imejengeka kwa wanawake walio wengi. "Once" mwanamke anapokuwa na kipato kikubwa kuliko mumewe wengi wao heshima kwa mume hupungua. Wengi wetu tumeshasikia kauli zinazofanana na hii "...mwanaume gani yule anakuja kunikopa mimi mwanamke..?"

Ndugu yetu chukulia kuwa hii ni tabia waliyonayo wanawake wengi. Ila kama wachangiaji wa mwanzo walivyosema, kaeni mzungumze. Inawezekana ndugu yetu hujatoa dukuduku lako kwa shemeji yetu hivyo shemeji yetu anafanya vitu ambavyo hadhani/hajui kuwa vinakukera.
 
Hivi ile thredi ya JS ipo wapi.....
 
Mzee hapo kosa ni lako. Hakuanza siku moja kufanya haya. Alianza taratibu na wewe ukawa unamwangalia tu, hukuona kama ni noma sasa unakuja kushituka leo wakati mambo yashaenda mrama.

Nyumbani kwangu mimi ndo Rais, waziri mkuu, waziri wa fedha, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi. Wizara za maendeleo ya jamii na chakula ndo anaachiwa yeye. Kwa hiyo mambo yote yanayohusu fedha lazima yaanzie kwangu. Hawa watu sometimes wanahitaji kupendwa kwa mipaka. Akishagundua kwamba umekufa na umeoza kwake anachukua advantage hiyo kukaa kichwani kwako (niwieni radhi akina dada, lakini hivyo ndivyo mlivyo).

Biblia yenyewe inasema wanaume ishini na wake zenu kwa akili. Ulifikiri ni akili gani ambayo biblia imesema? Lakini pia biblia inasema wanawake wawatii waume zao. So maamuzi yako yanatakiwa kuwa final. Sisemi umpe kipigo mke wako, bali nasema ni lazima uwe na overall power juu ya yale yanayohusu nyumba yako na familia yako.
 
Back
Top Bottom