Turahisishe maisha: Stendi ya Magufuli isiwe mwisho wa ubunifu wa usafiri Dar es salaam

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
105
Reaction score
116
TURAHISISHE MAISHA: STENDI YA MAGUFULI ISIWE MWISHO WA UBUNIFU WA USAFIRI DAR ES SALAAM

Na GULATONE MASIGA

Uamuzi wa Serikali wa kuimarisha matumizi ya Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli iliyopo Mbezi kwa shughuli za kupakia na kushusha abiria ni sehemu ya juhudi za kupanga upya mfumo wa usafiri wa mabasi katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa mtazamo wa mipango miji, usalama, ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa shughuli za usafirishaji, hatua hii ina mantiki.

Lakini katika dunia inayobadilika kwa kasi, ambako muda wa mwananchi una thamani, gharama za uendeshaji zina umuhimu na teknolojia inabadilisha namna watu wanavyosafiri, swali kubwa si kama tunahitaji stendi kuu.

Tunaihitaji.

Swali muhimu ni: Je, tunawezaje kuwa na stendi kuu yenye nguvu bila kumlazimisha mwananchi kulipa gharama zaidi, kutumia muda mwingi zaidi na kupata usumbufu ambao unaweza kuzuilika?

Hapo ndipo ubunifu unapohitajika.

Stendi kuu ni muhimu, lakini mwananchi naye ni muhimu

Stendi ya Magufuli ni miundombinu muhimu ya Taifa. Serikali inapowekeza katika kituo kikubwa cha mabasi, inalenga kuleta mpangilio, usalama, udhibiti wa shughuli za usafirishaji, mazingira bora ya abiria na ufanisi katika jiji. Hilo linapaswa kuungwa mkono.

Lakini mafanikio ya stendi hayapaswi kupimwa kwa idadi ya mabasi yanayoingia na kutoka pekee. Yanapaswa kupimwa pia kwa swali rahisi: Je, stendi hiyo imerahisisha maisha ya mwananchi?

Mwananchi anayesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali anahitaji usafiri salama, wa uhakika na wenye gharama zinazomudu. Lakini pia anahitaji huduma inayozingatia mahali anapoishi, anapofanya kazi na anakoelekea.

Kama abiria anayeelekea Gongolamboto, Kigamboni, Magomeni au maeneo mengine ya Dar es Salaam atalazimika kwenda Mbezi kwanza, kisha kutoka Mbezi kwenda anakoishi, tunapaswa kujiuliza kama mfumo huo unatumia rasilimali za Taifa na muda wa mwananchi kwa ufanisi unaostahili.

Na zaidi ya hapo, ikiwa basi lililomleta kutoka mkoa mwingine linaendelea kuelekea upande huo huo wa Jiji lakini linatakiwa kusafiri bila abiria, huku abiria akitafuta usafiri mwingine, basi kuna gharama mbili zinazozalishwa kwa safari moja.

Basi linatumia mafuta. Mwananchi naye anatumia fedha. Muda nao unapotea. Huo ni mjadala unaostahili kufanyiwa tathmini.

Ofisi za mabasi nazo ni sehemu ya uchumi wa Jiji

Katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, kampuni za mabasi zimewekeza katika ofisi na vituo vyao vya huduma. Baadhi zimekuwa zaidi ya ofisi za kuuza tiketi.

Zimekuwa vituo vya huduma vinavyohusisha maeneo ya kusubiri abiria, migahawa, huduma za malazi au mapumziko, vyoo na huduma nyingine za kijamii na kibiashara. Kuna pia shughuli za usafirishaji wa mizigo, huduma za kifedha na biashara ndogo ndogo zinazozunguka vituo hivyo.

Haya ni majukumu ya sekta binafsi katika uchumi wa jiji. Majengo hayo yameajiri watu. Yamezalisha biashara. Yameongeza thamani ya maeneo. Yamefungua fursa kwa watoa huduma wadogo na yamewafanya wananchi wapate huduma karibu na maeneo yao.

Kwa hiyo, wakati Serikali inasimamia mpangilio wa usafiri, inapaswa pia kuangalia athari za maamuzi yake kwa mitaji iliyowekezwa, ajira na biashara zinazotegemea mfumo huo.

Serikali nzuri si ile inayodhibiti shughuli zote. Serikali nzuri ni ile inayoweka kanuni zinazowezesha sekta binafsi kufanya kazi, huku maslahi ya umma yakilindwa.

Udhibiti wa usalama usiwe sababu ya kuua ubunifu na wala hoja ya usalama katika usafirishaji haiwezi kupuuzwa.

Usafirishaji wa dawa za kulevya, binadamu, bidhaa za magendo na shughuli nyingine haramu lazima udhibitiwe kwa nguvu zote za Serikali. Lakini katika karne hii, udhibiti haupaswi kumaanisha kuzuia kila kitu.

Teknolojia inaweza kutumika.

Taarifa za abiria zinaweza kuunganishwa.

Tiketi zinaweza kuwa za kidijitali.

Vitambulisho vya abiria vinaweza kuhakikiwa.

Mizigo inaweza kusajiliwa na kufuatiliwa.

Kampuni za mabasi zinaweza kuwajibishwa kwa taarifa za safari.

Vyombo vya usalama vinaweza kuwa na mifumo ya kisasa ya kufanya ukaguzi wa kiintelijensia badala ya kutegemea tu eneo moja la kimwili.

Kwa hiyo, badala ya kusema:

“Huduma zote ziende Mbezi ili Serikali iweze kudhibiti,” tunaweza kuuliza: “Tunawezaje kudhibiti usalama bila kumwongezea mwananchi gharama na usumbufu?”

Hilo ndilo swali la Serikali ya kisasa.

Suluhisho si kuchagua kati ya stendi kuu na ofisi za mabasi

Huenda mjadala huu usihitaji mshindi na mshindwa.

Stendi ya Magufuli inaweza kuendelea kuwa kitovu kikuu cha usafiri wa mabasi, huku kukiwa na mfumo uliodhibitiwa wa vituo vya huduma katika maeneo mengine ya Jiji.

Serikali inaweza kuweka viwango maalumu. Kampuni inayotaka kupakia au kushusha abiria katika kituo chake iwe na leseni maalumu.

Iwekewe masharti ya usalama na ubora wa vituo hivyo.

Iwe na mfumo wa kielektroniki wa kutoa taarifa za abiria na safari.

Iwe na utaratibu wa ukaguzi wa mizigo.

Iwekewe viwango vya mazingira, maegesho, usalama wa abiria na miundombinu.

Na Serikali iwe na uwezo wa kusimamisha huduma mara moja pale masharti yanapokiukwa.

Kwa mfumo huo, Serikali haipotezi udhibiti, kampuni hazipotezi uwekezaji, na mwananchi hapotezi urahisi wa huduma.

Stendi ya Magufuli nayo inapaswa kuwa “Commercial Hub”

Ikiwa tunataka mabasi mengi zaidi kutumia Stendi ya Magufuli, basi hatupaswi kufikiria Stendi ya Magufuli kama mahali pa mabasi tu.

Igeuzwe kuwa kituo kikubwa cha biashara na huduma. Stendi ya kisasa kama hii inaweza kuwa mji mdogo ndani ya jiji.

Iwe na maduka, migahawa, benki na huduma za kifedha, vituo vya huduma za serikali, huduma za simu na teknolojia, supermarket, huduma za mizigo, hoteli, ofisi, maeneo ya biashara ndogo na huduma nyingine zinazohitajika na abiria.

Inaweza kuwa kituo cha usafiri kinachounganisha mabasi na mifumo mingine ya usafiri wa mijini.

Inaweza kuwa sehemu ya kukutana kwa biashara.

Inaweza kuwa kituo cha usafirishaji wa mizigo.

Inaweza kuwa eneo la maegesho na kubadilishia usafiri.

Inaweza hata kuwa commercial logistics hub ya Magharibi mwa Dar es Salaam.

Hapo ndipo uwekezaji mkubwa wa Serikali unaweza kuanza kuzalisha mapato makubwa zaidi.

Mwananchi asibebe gharama za mpangilio wa Serikali

Katika kupanga sera, kuna kanuni moja muhimu: Gharama ya uamuzi wa Serikali isiwekwe yote kwenye mabega ya mwananchi.

Mwananchi anaweza kulipa nauli ya basi.

Anaweza kulipa usafiri wa kutoka nyumbani kwenda kituoni.

Anaweza kulipa nauli ya kutoka anaposhukia kwenda nyumbani.

Anaweza kupoteza muda.

Anaweza kubeba mizigo.

Anaweza kuwa anasafiri usiku.

Anaweza kuwa mzee, mama mwenye mtoto, mwanafunzi au mtu mwenye mahitaji maalumu.

Kwa hiyo, kila hatua inayoongeza safari moja ya ziada inapaswa kutazamwa kwa jicho la uchumi wa mwananchi. Muda ni gharama. Nauli ni gharama. Uchovu ni gharama. Usalama ni gharama. Ufanisi wa mfumo wa usafiri unatakiwa kupunguza gharama hizi, si kuziongeza.

Tujenge mfumo wa “Park-and-Ride” na feeder transport

Suluhisho jingine ni kuunganisha Stendi ya Magufuli na usafiri wa ndani wa Jiji.

Abiria anayefika Mbezi asibaki kutafuta usafiri wa kwenda Gongolamboto, Kigamboni au Magomeni kwa shida.

Tuwe na mfumo rasmi wa feeder buses, mabasi madogo au usafiri mwingine uliopangwa unaounganisha stendi na maeneo mbalimbali ya Jiji.

Pia pawe na mfumo wa park-and-ride kwa wananchi wanaotaka kuacha magari yao na kutumia mabasi.

Teknolojia inaweza kumsaidia mwananchi kujua:-

basi lake linaondoka saa ngapi; anatakiwa kufika saa ngapi; anatokea kituo gani; nashukia wapi; gharama ya safari nzima ni kiasi gani; na usafiri gani utamfikisha nyumbani baada ya kushuka. Hapo ndipo tunapoanza kujenga smart transport system.

Serikali na sekta binafsi wakae mezani

Kwa mtazamo wangu, hili si suala la Serikali dhidi ya wamiliki wa mabasi. Ni suala la Serikali na sekta binafsi kutafuta suluhisho bora kwa mwananchi.

Kwa hiyo, ni busara uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wamiliki wa mabasi kukaa chini na kufanya tathmini ya kina ya uamuzi huu.

Tathmini hiyo iangalie mambo manne:-

Kwanza, mwananchi: Je, gharama na muda wa safari vitaongezeka au kupungua?

Pili, Serikali: Je, usalama, udhibiti na mapato vitaimarika?

Tatu, sekta binafsi: Je, mitaji, biashara na ajira zilizopo zitalindwa?

Nne, jiji: Je, mfumo huu utapunguza msongamano na kuboresha mipango miji au utahamisha tu msongamano kutoka eneo moja kwenda jingine?

Majibu ya maswali haya ndiyo yanapaswa kuongoza sera na maamuzi yetu.

Dunia inakwenda kwenye “Integrated Transport”

Miji ya kisasa haifikirii usafiri kama kituo kimoja pekee.

Inafikiria mfumo mzima.

Abiria anatoka nyumbani, anafika kituoni, anapanda usafiri wa masafa marefu, anafika kituo kikuu, anahamia usafiri wa ndani na kufika anakoenda.

Mfumo mzima unatakiwa kufanya kazi kama mnyororo mmoja.

Hatuwezi kujenga miundombinu mikubwa ya kisasa lakini tukawa na mfumo wa huduma unaomlazimisha mwananchi kufanya safari nyingi zisizo za lazima.

Miundombinu ni muhimu, lakini mfumo wa huduma ndio unaoipa miundombinu maana.

Hitimisho: Turahisishe maisha

Serikali ya kisasa inapaswa kuwa na uwezo wa kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja:

Kulinda maslahi ya umma na kuwezesha ubunifu wa sekta binafsi.

Stendi ya Magufuli iimarishwe. Itumike. Iendelezwe. Igeuzwe kuwa kituo kikubwa cha usafiri, biashara na huduma.

Lakini pia ofisi na vituo vya kampuni za mabasi visiangaliwe kama washindani wa stendi kuu.

Vionekane kama sehemu ya mfumo mpana wa huduma ambao unaweza kudhibitiwa na Serikali kwa kutumia teknolojia, leseni, viwango vya usalama na mifumo ya taarifa.

Tusiwe na fikra kwamba ili Serikali ikusanye mapato lazima mwananchi apate usumbufu.

Tusiwe na fikra kwamba ili kuwe na usalama lazima huduma zote zikusanywe eneo moja.

Tusiwe na fikra kwamba uwekezaji wa Serikali lazima uue uwekezaji wa sekta binafsi.

Tunaweza kufanya yote kwa pamoja.

Serikali ipate mapato, sheria zifuatwe, usalama ulindwe, wawekezaji walindwe, ajira zilindwe na stendi ya Magufuli izalishe zaidi.

Na muhimu kuliko yote MWANANCHI ARAHISISHEWE MAISHA.

Kwa sababu mwisho wa yote, thamani ya sera na uwekezaji wa Serikali inapaswa kupimwa kwa kiasi ambacho maisha ya mwananchi yamekuwa rahisi, salama, yenye tija na yenye gharama nafuu.

Dar es Salaam inahitaji usafiri wa karne ya 21. Usafiri wa karne ya 21 unajengwa kwa kuunganisha watu, muda, teknolojia, biashara, usalama na fursa katika mfumo mmoja unaofanya kazi kwa mwananchi.

Turahisishe maisha.

Kwa Maoni Na Ushauri
0768497974
04/09/2026
 
Makala nzuri sana comrade. Kongole
 
MWANANCHI YUPI ANAHITAJI USALAMA ?AKIFA ANAAMBIWA KIFO NI KIFO
Viongozi mara nyingi hufanya yale wananchi wanayotaka. Wananachi wakizoea shida na kuona hayo ndiyo maisha basi viongozi watawafanyia hivyo hivyo. Wananchi wakizoea kupigwa kama ng'ombe na kuona hayo ndiyo maisha, na hawana la kufanya basi viongozi wanawafanyia hivyo hivyo. Kwa kifupi ni kuwa tabia na utendaji wa viongozi hutengenezwa na wananchi wenyewe. Kwa nini watu wanatakaka viongozi waache kufurahia maisha waje kuhangaika na wananchi wajinga wasiojitambua?
 
Sifahamu imekuwaje kuwa na watu,Tena wafanya maamuzi kutokea kuwaza,kupanga na kufikiri Bila,mikakati,utafiti,mpango endelevu na japo ushirikishwaji wa wadau,juu ya athari za maamuzi Fulani Fulani,iwapo wenye dhamana wanakosa ama weledi,ama kutokufanya juhudi kufafa kila Jambo kwa ubora na kiwango vinavyo shahilibasi kupata maini na mtazamo wa watoa na watumiaji wa huduma ungeweza kuondoa changamoto zisizo za lazima.
 
Kazi iendelee.....
Screenshot_20260816-150515~2.png
 
Back
Top Bottom