Turmeric Coconut Basmat Rice

Nilichemsha nyama, nyama hiyo niliiweka chumvi na tangawizi, ilipoiva niliiweka pembeni, nikatenga nyama na supu, nikakaanga vitunguu kama vile ambavyo wanatayarisha kwenye biryani, nilikatakata hoho, karoti na nyanya na kuweka kwenye bakuli moja, nilikuwa na pakti tatu za manjano (turmeric powder) huku ulimwengu nilipo wanafunga pakti sh.100, na pakti 1 ya curry powder.... nilipoanza kupika nilitumia ile supu ya nyama, niliiweka jikoni nikaweka na mchele na nilinyunyizia korosho, waweza kutumia hata zabibu kavu nilitumia Basmati Rice, ile supu ilipokaukia, nikanyunyizia nazi lile tui zito, nikamimina ile manjano na Curry Powder, nikachanganya vizuri, nikahakikisha chakula chote kimechanganyika vizuri na kupata rangi, mwishoni kabla ya kufunikia tena nikamimina zile nyanya, hoho, karoti nilizokatakata na vitunguu vile nilivyokaanga mwanzoni, then unafunikia na kukadiria muda chakula chako kitaiva kabisa, kikiiva kabisa unakoroga vizuri ili vile viungo ulivyo weka pale juu vichnganyike sawasawa na pia vitakuwa havijapondeka pondeka na vitaleta muonekano mzuri, Muhimu supu utakayotumia iwe ya kutosha kulainisha mchele na nazi iwe ya kuivisha lakini visije zidi na kufanya chakula bokoboko.
 
Uwiiiii nampikia mzee ila je siezi tuma mchele wa kawaida?
 
Nitaipikia family yangu next week [emoji39][emoji39]
Asante.
 
kuna sehem inaitwa el mandi ni mgahawa maarufu sana mnazi mmoja..

huwa wanapika pilau ya bismat wanaaiiita mandi..

ni tamu balaaaa

mandi kuku au mandi mbuzi.

wanatumia mchele kama huooo
 
Ila wakuu huu mchele huwa haunibariki yaani huwa sioni kama nakula wali ila vipande vya tambi vilivyofanywa mchele.
 
Mi nina tatizo na mchele aina aina ukiacha huu wetu wakiswahili. Mapishi yangu yote yanayohusisha mchele natumia mchele wa kawaida. Pia viungo kama turmeric vinanishinda kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…