Turudi kwenye unyago au tuendelee na kitchen party?

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Ndoa za siku hizi hazidumu, kina dada wengi hawajui mapishi, hawawezi kujisafisha na kuweka nyumba zao katika hali ya usafi.
Hawajui mahitaji ya waume zao, hawajui kuwatunza wala kuwaridhisha.
Kazi kwelikweli.
Eti sababu yao ni kwamba wamesoma, mambo ya ndani ya nyumba ni kazi na wajibu wa housegirl.
Mafunzo ya unyumba wanayapata kwa ufupi tu kwenye kitchen party.
Je nini kifanyike?
 
Tatizo ninaloliona mimi ni mmomonyoko wa maadili.
Hata wanaume sikuhizi wamekuwa wa hovyo tu, kina dada hali kadhalika.
 
.....tuwaache tu na masomo yao....tuoe mahouse gal,ndio wanajua wajibu wa mke
 
Wala mtu hahitaji unyago kujua kupika..usafi n.k

Sema tu hata wamama siku hizi wanaona mabinti zao hawana haja ya kuharibu kucha zao kuosha vyombo na kupika wakati mfanyakazi yupo...alafu hapo utakuta yeye mwenyewe alishaacha kupikia familia yake zamani hivyo haoni umuhimu.Hizi shughuli mtu anatakiwa afundishwe tangu mdogo...kwanzia miaka 11 hivi na kuendelea!
 
kwa mwendo huu house girl akikuzidi speed utamlilia nani?
Leo hapa jamvini nimeona eti house girl anafua hadi nguo za mama mwenye nyumba, jamani ni wapi twazipeleka ndoa zetu?
 
kwa mwendo huu house girl akikuzidi speed utamlilia nani?
Leo hapa jamvini nimeona eti house girl anafua hadi nguo za mama mwenye nyumba, jamani ni wapi twazipeleka ndoa zetu?

Ukweli ni kwamba kiwango cha uwepo wa nyumba ndogo siku hizi kimeongezeka...
 
Ukweli ni kwamba kiwango cha uwepo wa nyumba ndogo siku hizi kimeongezeka...


Tuko kimeongezeka kwa kuwa wanawake wamekuwa mno waigaji hawako real wanaolewa hawajui kupika wala kufua wala kumcare mume yaani wapo wapo tuu. Kila kitu kinafanywa na house gal mpaka kutandika kitanda cha master bed room na kufua boxer ni house gal, maji ya kuoga anaweka house gal, chakula anakutengea house gal wakati mke kakaa anatizama kideo, baa mnakuwa wote na wife wewe ukiagiza konyagi yeye anaagiza valuer
Sasa ukipata nyumba ndogo inayojua kucare unasahaui hata kwenu
 
<br />
<br />
hii ya valuer ni noma
 
wanawake wengi n wavivu sana,akiwa na hausegel au bint mdogo nduguye bac huyo ndo atafanya kila kitu,utamkuta housegal anapika af mtoto kakojoa au haja kubwa mama mwenye nyumba anamwita housegal au nduguye.m nadhan c kichen party wala unyago vi?
 
wanawake wengi n wavivu sana,akiwa na hausegel au bint mdogo nduguye bac huyo ndo atafanya kila kitu,utamkuta housegal anapika af mtoto kakojoa au haja kubwa mama mwenye nyumba anamwita housegal au nduguye.m nadhan c kichen party wala unyago
 
Na leo nitauliza tena. Hivi kitchen party kwa Kiswahili inaitwaje? Na kwa nini inaitwa kitchen party? Asili yake ni wapi? Ni Tanzania? Kama ni Tanzania kwa nini sasa inaitwa kitchen party?

Kuna anayejua?
 

Naz sijui napatia au nachemsha hapa
Swala sio unyago wala kitchen party
Swala zima hapa ni malezi ya watoto wetu maana watoto wanalelewa kudekezwa mpaka wanapitiliza
Utakuta msichana mkubwa kabisa au mvulana mkubwa kabisa anafuliwa nguo na house gal anaandaliwa msosi mezani na house gal na akimaliza house gal anakuja kuondoa vyombo na kuosha
Anatandikiwa kitanda na house gal
Sasa mtu kama huyo anafikiia kuwa anatakiwa kuoa au kuolewa tuseme zaidi hawa wa kuolewa. Anaenda kw amumewe hajui kupika, kufua, wala hajawahi kutandika kitanda chake mwenyewe. Unafikiri hapo hata kama utampa mafunzo ya unyago wa mwezi mmoja au kitchen party ya masaa au wiki moja atafundishika ajue kuwa kuna kupika au kufua au kupiga deki nyumba au kumjali mumewe amtengee chakula au hata maji ya kuoga au ajue mumewe anavaa nguo gani kama sio unaleta balaa
Ndo hao sasa wanaoishia kuwa ndani ya nyumba kila kitu kinafanywa na house gal na yeye anajiweka as if majukumu ya ndani hayajui ni ya house gal
Akigeukwa na the same house gal wala hana haja ya kulalamika
Tukubali malezi ya watoto yanachangpia sana na sidhani unyago wa muda mfupi au kitchen party inasaidia kufanya lolote kwa watu wa aina hii
Nisamehe kama nimetoka nje ya mada
 
Wazazi wetu hasahasa wanaojiita wamesoma wanaponda sana hii sayansi kimu kwa watoto wao wa kike,mie nadhani akina mama wakubali tu bila shuruti waanze kuwafundisha mabinti hawa 'tunu' za mwanamama wa kiafrika,wafundishwe kupika,usafi wa jumla,kuvaa,maana ya mme n.k

Unyago una maana japo ni vigumu leo kueleweka mbele ya k.party,tatizo la ndoa siku hizi kuvunjika na wanawake kuachwa si elimu bali tatizo ni kuondoa msisitzo kwenye mambo ya msingi,namaanisha as long as mwanamke ana moral values na anawajibika kwenye hayo mambo ya msingi,kwa nini umwache??lakini kama mabinti wataendelea kuwa rigidy basi sie wanaume hatuko radhi kuwaoa,tutaishi nao kama vimada (Comcubines) na mwisho tutawafukuza warudi makwao na mama zao wajiandae kuwapokea hawa mabinti zao.
 
asante dada kwa somo, nikikua sijui kuwa kazi ya mke/mwanamke ni
- kupika
-kujisafisha
- kusafisha nyumba
-kumtunza mume(sijui na mume anamtunza mke, au wanatunzani???!!!)
-kumridhisha mume ( mie nilidhani wanandoa wana jukumu la kuridhishana)

sasa wife ataisoma laaazma atekeleze haya, mie nikirudi miguu juu kwenye makochi kutazama mpira kama sijaenda bar nikaka hadi saa tano usiku!!
 
Sasa nimehitimisha hakuna mtu anayejua kitchen party asili yake wapi na wengi wanaoshiriki hata hawajui wanachokifanya. Ndiyo maana wengi mnakuwa hamzielewi. Mara kufundishwa kukata viuno mara kupeana vyombo mara sijui kufundishana jinsi ya kujiosha. Yaani ili mradi tu.
 
Ukweli ni kwamba kiwango cha uwepo wa nyumba ndogo siku hizi kimeongezeka...
<br />
<br />
dah...
Tunaenda nje kufuata peace of mind and pleasure.
Hawa wanawake wa doti komu hovyo kabisa.
 
Hivi role ya mwanamke ktk ndoa za sasa ni nini?
Na ya mwanamume ni nini?
Kwanini ndoa zisipodumu ni kosa la mwanamke?

Kama house help hatakiwi; kwenye ndoa ambayo couple wote ni waajiriwa nunueni dish washer, mashine ya kufulia etc ili kurahisisha kazi! Peaneni zamu ya kupeleka watoto daycare, clinic etc!

Otherwise mke awe 100% housewife na mume aprivide everything na ampe credit card mkewe kwa matumizi binafsi! Otherwise tutadanganyana!

Mwisho, nina ushaidi wa kutosha pale mke anakuwa perfect wife lkn mume hatulii! Naamini juu ya joint responsibilities! Girls acheni kuwatafutia excuse wanaume wanapokosa; it is none of ur doing ni uchafu, uzandiki na umalaya wake tu! Hakuna sababu yoyote ya mwanaume kucheat; bali kuna sababu za kuachana! Full stop!
 
Mimi siwezi kula chakula kilichopikwa na housegirl wakati mke wangu yupo!
House girl hafui nguo zangu labda mke awe amesafiri mwaka mzima hata hivyo nitapeleka kwa dobi.
Mtoto wangu yeyote hasa wa kike mwenye zaidi ya miaka 10 hafuliwi na housegirl
Housegirl hafanyi kazi za jikoni wakati binti zangu hapo nyumbani wamekaa tu hawana kazi.
Watoto wengi wa siku hasa wa kike wanawaza tu ngono kila wakati na hawafikirii mambo ya nyumbani. Wapumbavu kweli kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…