Kama kumbukumbu zangu ziko sawa CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA walisusia bunge la katiba likiwa katikati ya majadiliano na likiwa ktk hatua nzuri ya kupata katiba nzuri ya wananchi. Sababu kubwa ya kususa ilikuwa ni kutokubaliana na CCM juu ya muundo wa Mungano, wakati CHADEMA wakitaka muundo wa serikali tatu, CCM wao walitaka tubaki na serikali mbili kama ilivyo sasa.
Mimi kwa mtazamo wangu naona wapinzani walipoteza nafasi muhimu kabisa ya kupata katiba mpya kwani ktk mchakato kama ule huwezi kupata kila kitu, ni lazima ukubali kupoteza baadhi ya mambo ili mengine yaende. Kwa mfano kwenye ile rasimu kulikuwa na mambo mengi mazuri zaidi ya muundo wa muungano. Tungekubali kuliacha hilo lkn tungepata mengine kama tume huru, kuhoji uchaguzi wa rais mahakamani na mengine ambayo sio ya ksiasa kama haki za wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, walemavu na makundi mengine, hlf hilo la muundo wa muungano lingeweza kuja baadaye baada ya kupata hiyo katiba mpya. Lkn ksbb wanasiasa siku zote ni wabinafsi na wanavutia upande wao, hatma yake tumekosa yote.
Sasa miaka sita baadaye ndo tunataka tena katiba mpya ktk serikali ambayo ina vipaumbele tofauti na haina interest tena na mambo ya katiba mpya...
Je mchakato wa katiba mpya utafanikiwa ktk utawala huu wa awamu ya sita? Kwa maoni yangu inawezekana lkn itakuwa kwa mbinde sana, itatumika nguvu kubwa sana kufikia hatua tuliyokuwa tumefika kipindi kile. Na lazima tujifunze kutowaachia wanasiasa pekee ndo waamue hatma ya maisha yetu.
Mungu ibariki TANZANIA.