UKWELIYAKINIFU
Member
- Oct 6, 2020
- 27
- 50
Kwa upande wa CCM, huduma za afya zinachukuliwa kama huduma za msingi zinazolenga kupatikana kwa urahisi, gharama nafuu na kuweza kujenga taifa la wachapa kazi. Na mifano ya awali ya kilichofanyika kama kuongeza vituo vya afya kutoka 718 hadi 1,205; zahanati kutoka 6,044 hadi 7,242; hospitali za halmshauri 77 hadi 148 zikijengwa mpya 71 na ukarabati wa hospitali za rufaa 23. Pia uanzishwa matibabu ya ubingwa bobezi kwenye Hospitali ya Mlongazila; Uboreshaji wa Hospitali ya MOI na ajira kwa wahudumu wa afya imepelekea huduma za afya kufika maeneo mengi, walipo watu wa kipato cha chini. Lakini upatikanaji wa vifaa na dawa umepunguza nguvu ya ubidhaishaji wa huduma za afya kwa watu masikini.
Mambo haya yamegusa moja kwa moja watu wote na kuipa nguvu ilani ya CCM katika kushawishi wapiga kura, kwa kutoa mwelekeo unaopimika kwa hatua mahususi za yale yaliyofanyika kuliko maneno matupu yasiyothibitika kitakwimu, kibajeti na mkakati wa utekelezaji. Matumaini kupitia “unabii wa kisiasa” wa CHADEMA unakosa mashiko yakuweza kuaminisha umma kuwa sekta binafsi ndio dawa ya haya, wakati ushahidi wa awali kabla ya haya yalifanywa na CCM sekta hiyo ndio ilihujumu huduma za umma kwa maslahi binafsi ya wafanya biashara wa afya.
CCM imejikita zaidi katika kujenga jamii yenye afya ya uchumi, jamii, siasa na mwili kupitia maono ya ushiriki wa kila mmoja kama askari wa kufanikisha haya. Ilani ya CCM inajengwa katika dhana ya siasa kama utumishi wa kusimamia wanachi kustawisha maisha yao, kwa kuondoa matabaka ya awali ambayo yalitupa kando watu maskini. Uchumi shirikisihi unaosimamiwa na dola katika kuondoa uholela wa soko lililokosa huruma kwa tamaa ya faida na maslahi binafsi, ni dhima kuu. Kwa upande mwingine, upinzani na hasa hasa CHADEMA wanaangalia kurudisha nguvu ya soko lisilothibitiwa na kuwaacha wenye nguvu na wasio na nguvu kushindanishwa.
Tatizo lingine, tunaona nguvu ya sheria zinazomtazama mtu katika ubinafsi, juu ya nguvu ya jamii zikipamba kila hatua ya kubomoa mifumo inayosisitiza uchumi na huduma shirikishi zinazotokana na nguvu za watu wenyewe. Itakadi kuu za uliberali mamboleo za umimi na ubidhaishaji wa huduma za jamii, ni kaa la moto litalolinda maslahi ya wenye mitaji, na pengine wanasiasa wenye nguvu na wafadhiri wa mtazamo huu unaotuaminisha kwamba, wakati wote soko linatoa haki sawa. Ni juu ya wanachi kuchagua kati ya chama kinasukuma haki za kijamii hasa zinazojidhihirisha kwenye ilani ya CCM au kuchagua makuadi wa soko holela yanayotanguliza maslahi na kuuza utu wa watu masikini na nchi kwa vipande vya fedha.
Vita yetu kwa sasa kama taifa ni ya kitabaka na kiitikadi, inayolenga kurudusha nguvu na ustawi wa kijamii kwa watu masikini. Vita ya kisheria inayopendekezwa na upinzani imefungwa minyonyoro ya itikikadi ya adui tunayepambana naye, ambaye kwake soko huru ni njia ya kuendeleza unyonyaji wa rasilimali. Mwelekeo wetu inabidi kusaidia juhudi zinazolenga kuleta ukombozi wa kweli, ustawi wa jamii na fikra huru zinazotanguliza haki za kijamii kuliko haki binafsi zinazoongozwa mantiki na nguvu ya soko. Ilani ya CCM imejiweka bayana kwa matendo na nia thabiti ya kuongoza watanzania katika ukombozi wa kweli.