Naamini Unit Trust of Tanzania ni aina ya mutual fund - inaendeshwa na serikali. Imekuwepo sasa kwa miaka kadhaa na inaendeshwa kwa mafanikio ukilinganisha na Nicol (binafsi) iliyojifia.tukisema serikari ianzishe Mutual Funds kwamba kutakuwa kuna more security watu wataanza kuweka habari za kisiasa
ni kweli kabisa tunarudi kule kule la kuunganisha mitaji
mitaji iunganishwaje
hapo ndipo kunapobidi kuumiza kichwa na kuplan sie kama watanzania
Baadhi ya video alizoonyesha mleta uzi zina ugomvi na waendeshaji/mameneja wa mutual funds, hasa wa binafsi, wanavyofaidika sana na funds hizi kuliko wawekezaji. Mimi binafsi pia nisingependa kujiingiza kwenye funds za mameneja binafsi kama Nicol, hata zikianza tena. Lakini zikiendeshwa na serikali, ilimradi zinaendeshwa vema ili kukulipa gawio zuri, si mbaya - maana faida ichukuliwayo na serikali ni kama kodi kwa maendeleo.
… wenzetu kibao walikwisha haribu mfano Nicol, sina uhakika kama Deci na wao walikuwa Mutual Funds (wataalamu wanaweza kuja kutuambia kwa hili)…..kuna mtu alisema kuwa mutual funds kuanzisha sasa hivi itakuwa ngumu kwani watu wana kumbukumbu mbaya na jinamizi la NICOL
Nawashukuru waasisi wake maana miaka hiyo ya 2005 walinipa kibarua kama karani wa uhamasishaji wa manunuzi ya hisa za NICOL pale mlimani. Fursa hii ilinipa nafasi ya kushuhudia uelewa wetu juu ya masuala ya hisa na masoko ya hisa. Kama ulivyosema C.T.U uelewa wetu juu ya masoko ya mitaji, amani na hisa uko chini sana. Nilipita kila corridor, kila idara na kila ofisi pale mlimani. Nami nikiwa ndo nimefunuliwa kujua mambo ya hisa, sikushangaa sana kubaini uelewa wa wanafunzi wa masomo ya Biashara katika maeneo haya bali niliuzunika kutumia muda mwingi kuwaelimisha watu waliokuwa kwenye idara ambazo watu wake wanahusika moja kwa moja na tasnia hii.…hivyo basi kwanza nachoshauri ELIMU itolewe kwa kiasi kikubwa, wataalamu wa uchumi, wanazuoni, wanasiasa na watu mbali mbali wenye upeo na mambo haya ya Mutual Funds wajaribu kutoa elimu ili huu mpango wa kuwa na Mutual Fund zetu utimie
Nawasilisha
Kwa mtazamo wangu kuiachia serikali ianzishe Private Mutual Funds litakuwa kosa la kiufundi. Chombo cha Sekta Binafsi lazima kianzishwe na Sekta Binafsi, Kiendeshwe na Kumilikiwa na Sekta Binafsi. Serikali iwajibike tu kuweka frameworks. Maana chombo kikiisha kuwa Public Limited Company (PLC) lazima Serikali ichukue jukumu lake kulinda maslahi mapana ya umma.… tukisema serikari ianzishe Mutual Funds kwamba kutakuwa kuna more security watu wataanza kuweka habari za kisiasa mara ooh "kodi zetu zaliwa na magamba" nadhani wajua lugha za mitaani zinavyoongelewa
Muundo wa wazo la NICOL lilikuwa na bado ni wazo hai. Kukosea njia ndiyo kujua njia. Kuna sababu mbalimbali zilizoikwamisha NICOL kutofikia malengo yake. Ninakumbuka tatizo lilianzia kwenye Initial Public Offer (IPO) kutopata subscribers wa kutosha. Kwa mtazamo wangu, siasa za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa na athari kubwa katika kutofikia malengo ya IPO. Dr. Salim Ahmed Salim na waadilifu wengine wanaoshiriki katika siasa za nchi hii walikuwa wanaiunga mkono NICOL kwa mtazamo wa kuwawezesha wazawa na kuhakikisha hatma ya ubinafsishaji haiishii kwenye kuuza mashirika ya umma kwa wageni na wenyeji wachache. Mtazamo huu ulitafsiriwa kinyume na watawala na waliokuwa wanaandaliwa kurithishwa utawala. Ziliibuka hisia za NICOL kuonekana kama chombo gheresha cha kukusanya fedha za kumfadhiri Dr. SAS. Kwa hiyo badala ya serikali kuwaunga mkono kwa dhati, kukawepo na uhusiano wa mashaka. Pia nia ya mmoja wa waasisi na Kiongozi wa NICOL wakati huo kujiandaa kugombea ubunge katika jimbo ambalo angepambana na shemeji wa Mtawala wetu yalikaribisha misuguano baridi na Serikali. Mwisho wa yote NICOL haikuweza kuandikisha hata nusu ya waraka wa matarajio (Prospectus). Wakapewa muda wa nyongeza lakini bado hawakufikia nusu. Na kutokana na tafsiri potofu ya Watawala wetu hata kile kidogo walichokusanya hawakuweza katika mashirikia waliyokuwa wamelenga. Lengo kubwa la NICOL wakati huo lilikuwa kuinunua Benki ya NMB iwapo ingeuzwa. Baadae ilikuja kuuzwa lakini ikaangukia mikononi mwa Benki ya Wanaushirika wa Netherland (Rabo Bank).
Kwa ufupi, unapokoseasa, kilicho sahihi si kuachana na jambo ulilokuwa unafanya bali kufanya tathmini kujua kwa nini ulikosea na ulikosea wapi ili ujipange upya kuliendeleza jambo lako kwa usahihi zaidi. Edson angeridhika na kukosea jaribu lake la kwanza, leo hii dunia ingekuwa bado inawasha vibatari.
Kwa uelewa wangu, Deci ilikuwa revolving fund aina ya Ponzi Scheme. Ni tofauti na Mutual Funds. Kwenye mutual funds hatutoi hela kuwagawia wanahisa kwa mgunzumko wa kutegemea mmoja alete na mwingine apewe. Bali tunatoa gawio katika muda maalumu kulingana na hisa za mwanahisa. Na hili linategemeana na matokeo (Profit or loss) ya uwekezaji katika vitega uchumi ambavyo hiyo fund imewekezwa.
Nawashukuru waasisi wake maana miaka hiyo ya 2005 walinipa kibarua kama karani wa uhamasishaji wa manunuzi ya hisa za NICOL pale mlimani. Fursa hii ilinipa nafasi ya kushuhudia uelewa wetu juu ya masuala ya hisa na masoko ya hisa. Kama ulivyosema C.T.U uelewa wetu juu ya masoko ya mitaji, amani na hisa uko chini sana. Nilipita kila corridor, kila idara na kila ofisi pale mlimani. Nami nikiwa ndo nimefunuliwa kujua mambo ya hisa, sikushangaa sana kubaini uelewa wa wanafunzi wa masomo ya Biashara katika maeneo haya bali niliuzunika kutumia muda mwingi kuwaelimisha watu waliokuwa kwenye idara ambazo watu wake wanahusika moja kwa moja na tasnia hii.
Kwa mtazamo wangu kuiachia serikali ianzishe Private Mutual Funds litakuwa kosa la kiufundi. Chombo cha Sekta Binafsi lazima kianzishwe na Sekta Binafsi, Kiendeshwe na Kumilikiwa na Sekta Binafsi. Serikali iwajibike tu kuweka frameworks. Maana chombo kikiisha kuwa Public Limited Company (PLC) lazima Serikali ichukue jukumu lake kulinda maslahi mapana ya umma.
Saccos ni tofauti kabisa na Mutual Funds mkuu
TOFAUTI
Kindly, please explain the major difference(s).
Mutual Funds watu wana invest kwenye major companies ambazo ziko public so mara nyingi watu wanacheza na stock exchange
saccoss nadhani wote tunajua ni vikundi vya kukopa
na mutual funds watu hawakopi ni strictly investing
C.T.U na wote mnaofuatilia mada hii, habari ifuatayo itawavutia pia!
UTT roots for expanding saving culture
By Lusekelo Philemon, 3rd August 2013
The Unit Trust of Tanzania (UTT) has stated that Tanzania can only develop if the number of Tanzanians adopting a culture of saving and investing increases.
Head of UTT's Investor Service Centre in Arusha, Chediel Mugeta made this observation here this week when addressing representatives of the Arusha-based Savings and Credit Cooperative Societies (SACCOS).
The forum was meant to create a platform for SACCOS' representatives to extensively discuss opportunities available in the scheme and how individuals and companies could access those opportunities.
He said it is high time for Tanzanians irrespective of age to develop a culture of saving and invest in UTT, as this improves their future security in life.
The trust has been established to manage collective investment schemes and encourage savings through wide participation in the ownership of distributed shares, he said, urging parents to ensure that they create an environment for children develop a saving culture. This is still quite low in Tanzania's public domain, the official emphasized.
Participants at the forum commended UTT for its endeavors to reach out in most regions, admitting that a saving and investing culture is still rudimentary.
"It is high time for Tanzanians wherever they are to develop a saving culture, which is an important aspect for family and individual security," said a participant, John Pallangyo.
UTT is an extension of the Dar es Salaam stock exchange meant to establish, launch and manage collective investment schemes on shares traded on the DSE. It runs schemes like Umoja Fund, Wekeza Maisha, Watoto Fund, Jikimu and Liquid Funds.
SOURCE: THE GUARDIAN Home