Tusahau ya kampuni ya NICOL, hii ndio biashara itakayotutoa sisi watanzania

Tusahau ya kampuni ya NICOL, hii ndio biashara itakayotutoa sisi watanzania

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,074
Reaction score
3,743
[video=youtube_share;fpcvJiO-rjk]http://youtu.be/fpcvJiO-rjk[/video]

MUTUAL FUNDS

WATANZANIA TUNAHITAJI HIZI MUTUAL FUNDS KWA HALI NA MALI TUYASAHAU YA NICOL ILA TUANZE SAFARI MPYA

KWA MSAADA WA YOUTUBE TUNAWEZA KUANZA KUJIFUNZA KUHUSU HIZI MUTUAL FUNDS

HALAFU TUJADILI
 
Last edited by a moderator:
C.T.U
Nimekuwa nikiuliza na kujiuliza kama Tanzania tuna Private Sector Pension Scheme na kote nilikouliza sijapata majibu. Nimehoji pia kama Sheria zetu hasa ya Social Security Act na Capital Markets and Securities Act kama zinatoa fursa hii.

Hoja uliyoleta Mkuu C.T.U ni muhimu kuliko watu watakavyoichangia. Tunapohamasisha ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, mambo makuu ambayo Sekta ya umma popote duniani inayoyatarajia kuyapata kutoka Sekta binafsi la kwanza kabisa ni pesa/mitaji ya kuendeshea miradi, mengine ni teknolojia, na ujuzi wa kusimamia na kuendesha utoaji wa huduma za umma.

Kwa uchanga wa Sekta binafsi ya Tanzania ni dhahiri kwamba bila jitihada ya maksudi tunaweza kujikuta huu ubia unageuka kuwa Public-Foreigners-Partnership na hivyo kuleta tofauti ndogo sana kati ya athari za Ubinafsishaji (Privatization) na Ubia (PPP). Na kwa mifano michache hili limeanza kujitokeza. Mfano nani ameona mbia kutoka Sekta binafsi ya Tanzania ameshiriki kwenye uwekezaji wa miradi michache ifuatayo:
  • Bandari ya Bagamoyo: Mkataba kati ya Serikali na Wachina?
  • GE & Symbion Power na Serikali ya Tanzania?
  • Makaa ya Mawe Mchuchuma-Liganga kati ya Sichuan Hongda Group na NDC (SPV Tanzania China International Mineral Resources Limited)?
  • Uzalishaji wa Umeme Mtwara kati ya China na Serikali ya Tanzania?
Lipo tatizo la ushirikishwaji lakini pia lipo tatizo la Uwezo wa sekta binafsi yetu kimitaji na kiujuzi. Bado sekta ya umma haijatambua kuwa imeruhusu zama za dola kuhodhi uchumi kuwa zilipendwa na wakati huohuo bado sekta binafsi Tanzania haijafahamu uwepo wa fursa ya kuchukua majukumu ya sekta ya umma katika kuendesha miundombinu na kutoa huduma za umma.

Ukijaribu kuliangaza kwa undani tatizo la mitaji ni kubwa zaidi ya mengine na lina athari mbaya sana kwa deni la Taifa katika siku zijazo. Katika mazingira ya PPP niliyozungumzia ni kama hakuna local financial instruments za kuweza kufadhili miradi mikubwa. Miradi ya PPP ni miradi inayohitaji mikopo/mitaji mikubwa inayotumia kipindi kirefu sana katika marejesho (>25 years). Window nyingi zilizopo kwenye taasisi za kifedha nchini ni zile zinazoiva ndani ya muda mfupi. Hakuna taasisi yenye Uwezo wa kukopesha mathalani TZS bilioni 200-300 kwa miradi kama kumi mfululizo ambazo zitalipwa kwa miaka 20. Je, nini athari ya uchumi wa nchi kuwa na mitaji/mikopo mingi iliyotolewa na taasisi za nje, kufadhili makampuni ya nje katika kuendesha miradi ya ndani?

Wazo uliloleta ni moja ya mawazo mazuri ambayo binafsi naafikiana nayo. Ni wakati sasa tuwe na mifuko ya makabwela itakayosaidia katika uwekezaji mkubwa. Tuboreshe sheria zetu za masoko ya mitaji na dhamana (Capital Market and Securities) ziwe kichocheo za Sekta binafsi kujifunza utamaduni wa kuweka hazina (Savings).

Hakuna kitu kimekuwa kikiniuma katika miaka ya hivi karibuni hapa JF kama mada za maana kama hii kukosa wachangiaji.
 
Ni kweli Kabisa Mada kama hizi zinakosa wachangiaji
labda tuwaombe kina Invisible na modes wengine waiweke hii mada as sticky

anyway ni kweli kabisa kabwela kama mimi tunaweza kuwekeza kwenye haya makampuni makubwa ila sasa tatizo kama sio changamoto ambayo iko mbele yetu wenzetu kibao walikwisha haribu
mfano Nicol, sina uhakika kama Deci na wao walikuwa Mutual Funds (wataalamu wanaweza kuja kutuambia kwa hili)

kuna maada tulikuwa tunajadili kule jukwaa la mchanganyiko

kuna mtu alisema kuwa mutual funds kuanzisha sasa hivi itakuwa ngumu kwani watu wana kumbukumbu mbaya na jinamizi la nicol

na mimi nikawajibu kuwa kipindi kile baada ya Meridian kuyeyuka watu wasingefungua account bank

upepo siku zote hupita na mwisho wa siku watu husahau na kuendelea

tukisema serikari ianzishe Mutual Funds kwamba kutakuwa kuna more security watu wataanza kuweka habari za kisiasa

mara ooh "kodi zetu zaliwa na magamba" nadhani wajua lugha za mitaani zinavyoongelewa

hivyo basi kwanza nachoshauri ELIMU itolewe kwa kiasi kikubwa, wataalamu wa uchumi, wanazuoni, wanasiasa na watu mbali mbali wenye upeo na mambo haya ya Mutual Funds wajaribu kutoa elimu ili huu mpango wa kuwa na Mutual Fund zetu utimie
Nawasilisha
 
Mkuu ni Kweli, Ila Tatizo lina kuja kwa Watanznia wenyewe, Uelewa ni Mfinyu sana mkuu na Mfumo wa UJamaa haujatutoka kabisa, Ishu kama hizi kwenye nchi za Kibepari zilikuwepo miaka mingi sana, Tanzania tunatatizo lubwa sana na mifano ni mingi mno.
- Chukulia mfano wa Mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
- Kune ile UTT mpaka sasa Watanzania walio nunua Vipande pal hawafiki laki 5 katikanchi yenye watu milioni 40,

- Na hii chaine yake ni kubwa sana na inaenda hadi kwenye ishu za kifamilia, Nchi nyingi sana Duniani familia huungana pamoja na kuanzisha kampuni ya biashara ya familia na huendeshwa kifamilia, ILA TANZANIA PEKEE NDO UNAWEZA KUTA BABA ANA MILIKI MABASI NA MTOTO ANA MABASI NA ZOTE ZINA COMPETE HICHO KITU HAKIPO KWA WENZETU.

-Na hata NICOL still waliokuwa wamenunua share mule ni wachache sana n wengi waikuwa wana nunua za laki 5 ni wachache walio wka mule pesa nyingi sana my be Milioni 500 hadi 1 bilioni, na ishu iko kwenue uoaga,

-Watanzania mtu akisha jenga Nyumba yake ya kuishi na ana duka hapo nje na Dairy anaona wateja wanajazana kununua vitu ndo anakuwa amemaliza kazi ukimwambia ishu hizi atakuon wa ajabu.

HIVYO ISHU NI MFUMO WETU ULIVYO NA WATANZANIA WENGI SANA WANAPENDA INDIVIDUALISM,

- Cheki hata Kampuni za Ujezi, Tanzania kuna kampuni nyingi sanaza Ujanzi, Ila kwa hizo kampuni moja moja hakuna hata moja inayo weza kufurukuta mbele ya kampuni za Kigeni za Kichini ay wazungu kampuni kama SOGEASTOM ya Wafaransa
- Na hizi kampuni zetu hakuna hata mmoja yuko tiyali kuungana tena ndo unakuta mtu mmoja ana vijikampuni vitatu

SO WAKUU HI MUTUAL FUND INAHITAJI ELIMU MOJA YA AJABU SANA
 
Ni kweli kabisa tunarudi kule kule la kuunganisha mitaji

mitaji iunganishwaje

hapo ndipo kunapobidi kuumiza kichwa na kuplan sie kama watanzania
 
tukisema serikari ianzishe Mutual Funds kwamba kutakuwa kuna more security watu wataanza kuweka habari za kisiasa
Naamini Unit Trust of Tanzania ni aina ya mutual fund - inaendeshwa na serikali. Imekuwepo sasa kwa miaka kadhaa na inaendeshwa kwa mafanikio ukilinganisha na Nicol (binafsi) iliyojifia.
 
Baadhi ya video alizoonyesha mleta uzi zina ugomvi na waendeshaji/mameneja wa mutual funds, hasa wa binafsi, wanavyofaidika sana na funds hizi kuliko wawekezaji. Mimi binafsi pia nisingependa kujiingiza kwenye funds za mameneja binafsi kama Nicol, hata zikianza tena. Lakini zikiendeshwa na serikali, ilimradi zinaendeshwa vema ili kukulipa gawio zuri, si mbaya - maana faida ichukuliwayo na serikali ni kama kodi kwa maendeleo.
 
Ni kweli kabisa ni vyema SERIKALI ianzishe Mutual Funds maana hapo kidogo watu watakuwa na imani kwani ni kitu cha serikali

na ndio maana nikasema WANASIASA pia watusaidie katika hili
 
… wenzetu kibao walikwisha haribu mfano Nicol, sina uhakika kama Deci na wao walikuwa Mutual Funds (wataalamu wanaweza kuja kutuambia kwa hili)…..kuna mtu alisema kuwa mutual funds kuanzisha sasa hivi itakuwa ngumu kwani watu wana kumbukumbu mbaya na jinamizi la NICOL

Muundo wa wazo la NICOL lilikuwa na bado ni wazo hai. Kukosea njia ndiyo kujua njia. Kuna sababu mbalimbali zilizoikwamisha NICOL kutofikia malengo yake. Ninakumbuka tatizo lilianzia kwenye Initial Public Offer (IPO) kutopata subscribers wa kutosha. Kwa mtazamo wangu, siasa za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa na athari kubwa katika kutofikia malengo ya IPO. Dr. Salim Ahmed Salim na waadilifu wengine wanaoshiriki katika siasa za nchi hii walikuwa wanaiunga mkono NICOL kwa mtazamo wa kuwawezesha wazawa na kuhakikisha hatma ya ubinafsishaji haiishii kwenye kuuza mashirika ya umma kwa wageni na wenyeji wachache. Mtazamo huu ulitafsiriwa kinyume na watawala na waliokuwa wanaandaliwa kurithishwa utawala. Ziliibuka hisia za NICOL kuonekana kama chombo gheresha cha kukusanya fedha za kumfadhiri Dr. SAS. Kwa hiyo badala ya serikali kuwaunga mkono kwa dhati, kukawepo na uhusiano wa mashaka. Pia nia ya mmoja wa waasisi na Kiongozi wa NICOL wakati huo kujiandaa kugombea ubunge katika jimbo ambalo angepambana na shemeji wa Mtawala wetu yalikaribisha misuguano baridi na Serikali. Mwisho wa yote NICOL haikuweza kuandikisha hata nusu ya waraka wa matarajio (Prospectus). Wakapewa muda wa nyongeza lakini bado hawakufikia nusu. Na kutokana na tafsiri potofu ya Watawala wetu hata kile kidogo walichokusanya hawakuweza katika mashirikia waliyokuwa wamelenga. Lengo kubwa la NICOL wakati huo lilikuwa kuinunua Benki ya NMB iwapo ingeuzwa. Baadae ilikuja kuuzwa lakini ikaangukia mikononi mwa Benki ya Wanaushirika wa Netherland (Rabo Bank).

Kwa ufupi, unapokosea, kilicho sahihi si kuachana na jambo ulilokuwa unafanya bali kufanya tathmini kujua kwa nini ulikosea na ulikosea wapi ili ujipange upya kuliendeleza jambo lako kwa usahihi zaidi. Edson angeridhika na kukosea jaribu lake la kwanza, leo hii dunia ingekuwa bado inawasha vibatari.

Kwa uelewa wangu, Deci ilikuwa revolving fund aina ya Ponzi Scheme. Ni tofauti na Mutual Funds. Kwenye mutual funds hatutoi hela kuwagawia wanahisa kwa mgunzumko wa kutegemea mmoja alete na mwingine apewe. Bali tunatoa gawio katika muda maalumu kulingana na hisa za mwanahisa. Na hili linategemeana na matokeo (Profit or loss) ya uwekezaji katika vitega uchumi ambavyo hiyo fund imewekezwa.
…hivyo basi kwanza nachoshauri ELIMU itolewe kwa kiasi kikubwa, wataalamu wa uchumi, wanazuoni, wanasiasa na watu mbali mbali wenye upeo na mambo haya ya Mutual Funds wajaribu kutoa elimu ili huu mpango wa kuwa na Mutual Fund zetu utimie
Nawasilisha
Nawashukuru waasisi wake maana miaka hiyo ya 2005 walinipa kibarua kama karani wa uhamasishaji wa manunuzi ya hisa za NICOL pale mlimani. Fursa hii ilinipa nafasi ya kushuhudia uelewa wetu juu ya masuala ya hisa na masoko ya hisa. Kama ulivyosema C.T.U uelewa wetu juu ya masoko ya mitaji, amani na hisa uko chini sana. Nilipita kila corridor, kila idara na kila ofisi pale mlimani. Nami nikiwa ndo nimefunuliwa kujua mambo ya hisa, sikushangaa sana kubaini uelewa wa wanafunzi wa masomo ya Biashara katika maeneo haya bali niliuzunika kutumia muda mwingi kuwaelimisha watu waliokuwa kwenye idara ambazo watu wake wanahusika moja kwa moja na tasnia hii.

… tukisema serikari ianzishe Mutual Funds kwamba kutakuwa kuna more security watu wataanza kuweka habari za kisiasa mara ooh "kodi zetu zaliwa na magamba" nadhani wajua lugha za mitaani zinavyoongelewa
Kwa mtazamo wangu kuiachia serikali ianzishe Private Mutual Funds litakuwa kosa la kiufundi. Chombo cha Sekta Binafsi lazima kianzishwe na Sekta Binafsi, Kiendeshwe na Kumilikiwa na Sekta Binafsi. Serikali iwajibike tu kuweka frameworks. Maana chombo kikiisha kuwa Public Limited Company (PLC) lazima Serikali ichukue jukumu lake kulinda maslahi mapana ya umma.
 
Muundo wa wazo la NICOL lilikuwa na bado ni wazo hai. Kukosea njia ndiyo kujua njia. Kuna sababu mbalimbali zilizoikwamisha NICOL kutofikia malengo yake. Ninakumbuka tatizo lilianzia kwenye Initial Public Offer (IPO) kutopata subscribers wa kutosha. Kwa mtazamo wangu, siasa za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa na athari kubwa katika kutofikia malengo ya IPO. Dr. Salim Ahmed Salim na waadilifu wengine wanaoshiriki katika siasa za nchi hii walikuwa wanaiunga mkono NICOL kwa mtazamo wa kuwawezesha wazawa na kuhakikisha hatma ya ubinafsishaji haiishii kwenye kuuza mashirika ya umma kwa wageni na wenyeji wachache. Mtazamo huu ulitafsiriwa kinyume na watawala na waliokuwa wanaandaliwa kurithishwa utawala. Ziliibuka hisia za NICOL kuonekana kama chombo gheresha cha kukusanya fedha za kumfadhiri Dr. SAS. Kwa hiyo badala ya serikali kuwaunga mkono kwa dhati, kukawepo na uhusiano wa mashaka. Pia nia ya mmoja wa waasisi na Kiongozi wa NICOL wakati huo kujiandaa kugombea ubunge katika jimbo ambalo angepambana na shemeji wa Mtawala wetu yalikaribisha misuguano baridi na Serikali. Mwisho wa yote NICOL haikuweza kuandikisha hata nusu ya waraka wa matarajio (Prospectus). Wakapewa muda wa nyongeza lakini bado hawakufikia nusu. Na kutokana na tafsiri potofu ya Watawala wetu hata kile kidogo walichokusanya hawakuweza katika mashirikia waliyokuwa wamelenga. Lengo kubwa la NICOL wakati huo lilikuwa kuinunua Benki ya NMB iwapo ingeuzwa. Baadae ilikuja kuuzwa lakini ikaangukia mikononi mwa Benki ya Wanaushirika wa Netherland (Rabo Bank).

Kwa ufupi, unapokoseasa, kilicho sahihi si kuachana na jambo ulilokuwa unafanya bali kufanya tathmini kujua kwa nini ulikosea na ulikosea wapi ili ujipange upya kuliendeleza jambo lako kwa usahihi zaidi. Edson angeridhika na kukosea jaribu lake la kwanza, leo hii dunia ingekuwa bado inawasha vibatari.

Kwa uelewa wangu, Deci ilikuwa revolving fund aina ya Ponzi Scheme. Ni tofauti na Mutual Funds. Kwenye mutual funds hatutoi hela kuwagawia wanahisa kwa mgunzumko wa kutegemea mmoja alete na mwingine apewe. Bali tunatoa gawio katika muda maalumu kulingana na hisa za mwanahisa. Na hili linategemeana na matokeo (Profit or loss) ya uwekezaji katika vitega uchumi ambavyo hiyo fund imewekezwa.

Nawashukuru waasisi wake maana miaka hiyo ya 2005 walinipa kibarua kama karani wa uhamasishaji wa manunuzi ya hisa za NICOL pale mlimani. Fursa hii ilinipa nafasi ya kushuhudia uelewa wetu juu ya masuala ya hisa na masoko ya hisa. Kama ulivyosema C.T.U uelewa wetu juu ya masoko ya mitaji, amani na hisa uko chini sana. Nilipita kila corridor, kila idara na kila ofisi pale mlimani. Nami nikiwa ndo nimefunuliwa kujua mambo ya hisa, sikushangaa sana kubaini uelewa wa wanafunzi wa masomo ya Biashara katika maeneo haya bali niliuzunika kutumia muda mwingi kuwaelimisha watu waliokuwa kwenye idara ambazo watu wake wanahusika moja kwa moja na tasnia hii.

Kwa mtazamo wangu kuiachia serikali ianzishe Private Mutual Funds litakuwa kosa la kiufundi. Chombo cha Sekta Binafsi lazima kianzishwe na Sekta Binafsi, Kiendeshwe na Kumilikiwa na Sekta Binafsi. Serikali iwajibike tu kuweka frameworks. Maana chombo kikiisha kuwa Public Limited Company (PLC) lazima Serikali ichukue jukumu lake kulinda maslahi mapana ya umma.

Ni kweli Kabisa swala la Elimu pia linahitajika sana mie nashauri watu ambao watakuwa wanajitolea katika kufundisha watu kuhusu somo zima la hisa na vitu kama hivyo
watu wengi wako interesting kujua ila sasa tatizo sijui huwa ni nini...
wengi wanaishia tu kusema nitatafuta muda nitatafuta muda mwishoni siku zinayoyoma, miaka inaenda

hivyo basi kwa wataalamu wetu wa haya mambo ikiwemo wewe mkuu ericus kimasha ingekuwa ni vizuri zaidi kama ungekuwa ungetupa nondo mbili tatu zinazohusu mambo haya

naamini tutajifunza mambo mawili matatu ambayo tutaweza kuyatumia na kuweza kujiendeleza katika harakati zetu za kupambana na uchumi
 
Wabongo wanafanya mambo yao kupitia SACCOS na VICOBA siku hizi.

That is alsmo some kind of Mutual Fund...
 
Wabongo wanafanya mambo yao kupitia SACCOS na VICOBA siku hizi.

That is alsmo some kind of Mutual Fund...

Saccos ni tofauti kabisa na Mutual Funds mkuu
TOFAUTI
 
Kindly, please explain the major difference(s).

Mutual Funds watu wana invest kwenye major companies ambazo ziko public so mara nyingi watu wanacheza na stock exchange

saccoss nadhani wote tunajua ni vikundi vya kukopa

na mutual funds watu hawakopi ni strictly investing
 
SACCOS hazikatazwi kununua hisa au kuingia ubia na makampuni makubwa.

Mutual Fund inaweza kuwa na utaratibu wa kukopeshana, haikatazwi kisheria. Kwa sababu kwenye mutual funds sio lazima mtu ajiunge kama individual, wanaweza kujiunga kama kikundi. By the way, SACCOS inaweza kuwa member wa mutual fund too. The same applies to VICOBA.

My point ni hii>>> concept ya watu kuchanga mitaji na kufanya biashara pamoja sio concept mpya. Hivi sasa inafanyika in small scales in the face of SACCOS na VICOBA.
 
C.T.U na wote mnaofuatilia mada hii, habari ifuatayo itawavutia pia!

UTT roots for expanding saving culture

By Lusekelo Philemon, 3rd August 2013

The Unit Trust of Tanzania (UTT) has stated that Tanzania can only develop if the number of Tanzanians adopting a culture of saving and investing increases.

Head of UTT's Investor Service Centre in Arusha, Chediel Mugeta made this observation here this week when addressing representatives of the Arusha-based Savings and Credit Cooperative Societies (SACCOS).

The forum was meant to create a platform for SACCOS' representatives to extensively discuss opportunities available in the scheme and how individuals and companies could access those opportunities.

He said it is high time for Tanzanians irrespective of age to develop a culture of saving and invest in UTT, as this improves their future security in life.

The trust has been established to manage collective investment schemes and encourage savings through wide participation in the ownership of distributed shares, he said, urging parents to ensure that they create an environment for children develop a saving culture. This is still quite low in Tanzania's public domain, the official emphasized.

Participants at the forum commended UTT for its endeavors to reach out in most regions, admitting that a saving and investing culture is still rudimentary.
"It is high time for Tanzanians wherever they are to develop a saving culture, which is an important aspect for family and individual security," said a participant, John Pallangyo.

UTT is an extension of the Dar es Salaam stock exchange meant to establish, launch and manage collective investment schemes on shares traded on the DSE. It runs schemes like Umoja Fund, Wekeza Maisha, Watoto Fund, Jikimu and Liquid Funds.

SOURCE: THE GUARDIAN http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=57779
 
SOURCE: THE GUARDIAN Home

AWESOME
hivi vitu kama
UTT kwa kweli inabidi zipate support ya mimi wewe huyu na yule
so far nimetembelea mtandao wao nikaona sio mbaya ku share na wana jf
http://www.utt-tz.org

ni muda wa sisi kuchambua mchele ni upi na pumba ni upi
ni muda wa sisi kufunguka na kuamua kujenga maisha yako ya miaka 5 ijayo 10 mpaka 30

ni muda wa sisi kuwaandalia maisha watoto wetu

ifike mahali watanzania tuwe na nidhamu na fedha kwa kuwekeza sehemu mbali mbali
kwani ni dhahiri kabisa na inafahamika kuwa mtanzania akipata hela ya ziada badala ya kuwekeza yeye anaenda kwenye kiti kirefu

wakati angeweza ku save
 
Kwa miaka mingi sana nimefikilia swala la kuleta hizi financial vehicles kwenye Tanzania market, nadhani Umoja Fund is some kind of mutual fund lakini there is very few information kuhusu fund. Ukweli ni kwamba Watanzania hawana knowledge ya kutosha kuhusu MF, pili hakuna sheria ya kuongoza MF na tatu lack of liquid investment vehicles nayo inachangia. Kama utatengeneza MF Portfolio it is obvious kwamba utawekeza kwenye Kilimo na Private Equity (ambayo nayo ni mzozo kwa bongo).

Kama kuna mtu ambae yuko interesting na kuexplore this sector, am willing to share some information. Cha muhimu ni how to raise capital investment fund, kudetermine ROI, kujua jinsi ya kulobby TZ government to write a guideline laws.
 
Back
Top Bottom