Tusahau ya kampuni ya NICOL, hii ndio biashara itakayotutoa sisi watanzania

Ndugu mnafuatatilia mada hii, napenda kuchukua fursa ya mjadala huu kuwaomba wale wanaomiliki hisa katika makampuni ambayo hisa zake zinauzwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kama vile TWIGA, TBL, CRDB, n.k. kushiriki katika utafiti wangu.

Nimeandaa dodoso ambayo unaweza kujaza online, kwa kugonda kwenye link ifuatayo:

https://www.surveymonkey.com/s/58DLYW8

Ukimaliza kujaza, bofya kitufe cha "Done", nayo itanifikia mara moja.

Natanguliza shukrani za dhati, kwa wale watakaopenda kuchangia katika utafiti huu.
 
Bado wachanga tukikuwa tutafika.

Kwanini usianzishe?

Hapo wa kuogopwa ni huyo jamaa mwenye briefcase.
 
Napenda sana hizi mutual funds but lazima nikiri naziogopa nikichek ya nicol hata yaliyotokea kwenye financial crisis huko USA jinsi hao managers walivyocheza na investments za watu bei za hisa zikaporomoka watu wakala hasara while wao managers wakijilipa bonus na kusepa nakiri napata uoga kwakweli though kuunganisha mitaji its the best idea kwa watu na mataifa maskin kama yetu ili kustay competitive
 
Bado wachanga tukikuwa tutafika.

Kwanini usianzishe?

Hapo wa kuongopwa ni huyo jamaa mwenye briefcase.

DADA YANGU FAIZA FOXY vitu kama hivyo huwezi kuanzisha mwenyewe kuna vitu vingi vya kuangalia
kama

board of trustee n.k

Hapa sasa ndiko kuna msala kwani ni lazima uweke watu experienced na wenye hadhi fulani katika jamii hiyo na kwa nchi zetu hizi hizi Mutual Funds zinazokufa kila leo watu wengi wanaogopa viti hivi kwani wanaamini kibaya chochote kikitokea CV zao zitaharibika

na kama ujuavyo Investment Business ni business yenye ku contain risk sana
 


But kwa wenzetu wana MF ambazo ziko strong sana pamoja na kitokea kwa ile inshu ya 2008 iliyopelekea Kupotea kwa ramani kwa
LEHMAN BROTHERS
 


Mkuu kwanza kabisa naomba nishukuru kwa kuchangia mada hii

mie binafsi niko interesting ku explore this sector lakini ni vyema kabisa kama ni information tu share hapa ili mimi, yule na wao waweze kujua na kufumbua upeo wao kuhusu hizi financial vehicles
 

Usijifunge mwenyewe, weka proposal na feasibility yako vizuri, ikikaa sawa ntakusaidia kupata wadhamini na hata wawekezaji.
 
Usijifunge mwenyewe, weka proposal na feasibility yako vizuri, ikikaa sawa ntakusaidia kupata wadhamini na hata wawekezaji.


safi sana dada yangu natumaini hata watu ambao walikuwa hawajui waanzie wapi nahisi kwa post yako itatoa mwanga sana kwa vijana
 
Hizi nondo nimezipenda sana mkuu C.T.U Mi nikajua wewe unakaunta tera peke yake kumbe hata huku kwenye uchumi unakaunta tera pia.
 
Last edited by a moderator:
Hizi nondo nimezipenda sana mkuu C.T.U Mi nikajua wewe unakaunta tera peke yake kumbe hata huku kwenye uchumi unakaunta tera pia.

kawaida tu mkuu
kidogo kidogo tunajifunza kutoka kwa waungwana wengu tu hapa jf
 
Mutual fund ni very interesting financial investment tool, kuna mambo mengi sana yakuangalia before to put it pamoja. Lakini important zaidi ni diversification of risk, na hii unaweza kuipata tuu kama utakuwa una sector mbali mbali ambazo unaweza kuwekeza na kujua parformance ya hizo sector historical. Tatizo la Tanzania ni kwamba kwanza hakuna sector nyingi ambazo zipo public, nyingi ni private na Wanye sector hizo hawaitaji mitaji kutoka kwa watu private wanategemea sana Bank. Pili sheria za Tanzania zinabana kupeleka mitaji nje ya Tanzania, hivyo huwezi kutoa pesa Tanzania kuweka kwenye world largest index kama SP 500.

Hivyo option kubwa Tanzania ni kuwa na Private Equity, ambayo hii unaweza kuamua unawekeza kwenye sector mbili au tatu then kutokana na ROI za ile investment unaweza toa dividend kwa investors in quarterly base na kuonyesha Portfolio growth. Huwezi chukua western private equity model na kuimplement Tanzania, it will never work. Hivyo creativity ndio key kubwa sana. You need to be creative kwa kutengeneza mfumo unaondena na mfumo wa Tanzania.

Kikubwa sana ni first, how are you planning to raise capital? This is a focal point, sababu kunaitajika enough liquidity ya kufanya wewe uweze kujiendesha na wewe uweze kuwekeza. Pili, wapi utawekeza hizi fedha, what are the guidelines za kuwekeza na ni kwa vipi those guideline will be parallel to Tanzania law. Tatu, You will need your own money to win the trust of other people monies. Mimi nilipiga mahesabu ya at least million 100 kuanzia na hii ni portfolio capital not cash to run operational, you will need that too.

Mwisho you need investment salesman, na hawa ni wagumu sana kuwapata Tanzania. People who knows how to make a pitch on Investment vehicles.
 
kutumia ni muhimu kwa uchumi kukua. kuweka akiba kuna faida pale tu akiba hiyo inapowekezwa. Akiba kidogo zinapounganishwa huwa akiba kubwa ambayo huweza kuwekezwa katika mradi mkubwa wenye manufaa makubwa. Watanzania tuna matatizo matatu makubwa: kwanza hatujiamini, pili hatuaminiani na tatu ni umimi. NICOL ilikufa kwa vile wenye nguvu za kisiasa na kiushawishi hawakuwaamini wale wenye weledi na kuthubutu. badala ya kuweka nguvu za fikra na fedha kwenye kapu moja tukaingia kwenye malumbano ya kipuuzi na kupambana kama panzi huku kunguru akina rabo bank, Kempisk na wengine wakijitwalia mali zetu bure bwerere. Serikali ya Tanzania inaongozwa na ndugu zetu wasiojua tofauti kati ya wageni na wazawa. wao anafikiria ili mradi kampuni iko nchini na inalipa kodi basi inachangia sana kukuza uchumi. mutual funds tukizielewa vema tukazianzisha na kuziendesha kiadilifu zitaweka uchumi wetu mikononi mwetu. lakini ili tuumiliki uchumi utakaokuwa mikononi mwetu lazima tuachane na mawazo madogo ya kuwa na biashara yangu tufikirie kuwa na biashara za kutawala sekta nzima. Hivi viduka na vikampuni vya kujenga ghorofa mbli tatu havitaweza kuichangamsha vya kutosha mifuko hii. Tutumie kwa uangalifu, tuweke akiba kwa hekima na tuwekeze kwa kwa umahiri. PAMOJA TUTAWEZA. USHINDI WAHITAJI USHINDANI
 

Sheria zipo nenda CMSA watakuelimisha zaidi
 
Serikali ifungue milango waje wawekezaji wa nje wanaoaminika waaanzishe hapa ili tujifunze na sisi.
 

Katika nchi ambayo Fixed Deposits zinzowekwa kwenye mabenki zinalipa hadi 14% inabidi ujipange sana maana RISK ipo juu mnoo. Unashangaa umesha commit funds mwaka mzima kwa 8% ghafla demand ya loanable funds inafikia 14% hapo lazima manager ukune kichwa.
 

Nimekupa like mkuu,unachoongea ni sahihi kabisa,uelewa wa wasomi tena wa hayo hayo masomo ya biashara juu ya hiz issues ni mdogo sana ,na ukija kwa general public ndo kabisaa patupu. Like nyingine ni kweli kuwa mutual funds inabid iwe kwa muundo wa PLC then mkono wa serikali utaingia kama tu unavyoingia ktk kuhakikisha mazingira bora kwa wawekezaji .kusema kwamba wanasiasa waingie hapa tena ni kurud kule kule tulikotoka
 
Mkuu, ulichokisema ni kweli ila umesahau kuwa tatizo kubwa ambalo linachangia kwa Tanzania ni kuwa na wataalamu wachache kwenye suala la uwekezaji na hili ndio linachangia matatizo yote na vitu vyote ulivyo vitaja hapo juu.
Kwa kipindi kirefu Watanzania wamekuwa wana dhana kuwa wahasibu ndio wataalamu wa mambo ya uwekezaji kwa Ulaya na USA pamoja na nchi nyingine zilizoendelea wala sivyo hivyo wataalamu wa uwekezaji ni kama Investment Analyst, Fund Manager ni wazuri kwenye speculating (Speculator) ambao wanahusika na future performance ya miradi sio waatalamu wa uhasibu wanaohusika na past records za kampuni na hapa ndio kunaleta utata kwa Tanzania.
Tunaitaji zaidi wataalamu wa miradindio watakao weza kupeleka miradi mbele. Mimi binafsi ni mtaalamu wa miradi ni Investment Analyst na background yangu ni engineering. Tukiweza kuwa na wataalamu wengi wa miradi tutaona mabadiliko makubwa lasivyo watu kutoka nje yaani wawekezaji watakuja Tanzania watavuna na kuondoka na faida yote na huku tukibakiwa na faida ndogo ambayo haiwezi kuleta mabadiliko makubwa kwenye uchumi wa nchi.
 
Mimi binafsi siwezi kuwekeza kwenye mutual funds hapa Tanzania katika haya mazingira ya sasa. NICOL imechangia woga wangu but kikubwa ni udhaifu wa regulatory authorities kusimamia haya mambo. Mfano kuna watu walifanya Insider Dealing NICOL ikanunua hisa kwenye kiwanda cha dawa cha mdogo wa Mengi, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Hata serikali kuwahoji tu wahusika ili kujiridhisha kuwa hakukuwa na njama zozote za wizi bali ni matatizo ya kiufundi, hakuna, nchi za wenzetu NICOL wangeitwa hadi kwenye parliamentary committee kujieleza lakini hapa kwetu hawajawahi hata kuchunguzwa kama kuna wrong doing.

Mitaji ni tatizo sugu hapa nchini, umebahatisha kamtaji kako then ukapeleke kwenye MF ambako kama wasanii wakichakachua si serikali wala bunge litaingilia kati kujaribu kutetea vijisenti vya wananchi wake ni vigumu sana. Hakuna serious Fraud crackdown in the country, heri niendelee kudunduliza na kuja kutoka at 55 yrs kuliko kudhulumiwa at 35 yrs na nisitoke maishani mwangu mote .
 
..... Mfano kuna watu walifanya Insider Dealing NICOL ikanunua hisa kwenye kiwanda cha dawa cha mdogo wa Mengi....
Kwenye hii acquisition, insider (Dr. R. Mengi) acted in favor of NICOL and its shareholders. Kwanza kwa ku-declare interest kufuatia udugu wa damu na mwenye Kiwanda. Pili akaenda mbali zaidi kupinga huo uwekezaji na alipoona wenzake kwenye Kamati ya Uwekezaji hawamuelewi na badala yake wanamuona kama mtu mwenye wivu wa maendeleo ya mdogo wake, akaamua kujiuzuru ujumbe wa hiyo Kamati. Kwa hiyo hii kama ni kuwa insider dealing haikuwa mbaya. Ilikuwa njema ya kuokoa pesa za wanahisa.

Hata mie naona ni udhaifu mbaya unaoua moyo wa uwekezaji kwa CMSA siku hizo kushindwa kuwachukulia hatua wahusika. Hata majuzi vitabu vyao vya mahesabu vilikuwa na misleading information lakini DSE bado ikaishia kurushiana maneno badala ya kuwachukulia hatua. Mambo yaleyale yametokea kwa Precision Air kuingia IPO ikiwa na mahesabu yenye warakini! CMSA na DSE inabidi waongeze umakini na udhibiti katika kusimamia Sheria ya Uwekezaji wa Pamoja, Sheria ya Masoko ya Hisa na Mitaji ama sivyo watu watapoteza imani kabisa na masoko ya dhamana na hisa.

References:
 

Haimaanishi kuwa moja kwa moja Insider ni Reginald Mengi, but upo uwezekano katika hao waliopingana na ushauri wa Mengi wapo waliokula njama kununua kampuni ambayo inakufa kwa bei kubwa na kupoteza kiasi kikubwa cha hela za NICOL ambazo kamwe haziwezi kurudi na zilizotoka kwa wavuja jasho waliopoteza nguvu zao kwa miaka mingi kuzipata. Na yet hakuna mamlaka ya serikali iliyojaridbu kujiridhisha kama kuna element yoyote ya wrong doing.

Kwa mtazamo wangu CMSA na DSE ni majanga ya kitaifa ambayo yanaundwa na watu ambao kwa kiasi kikubwa hawakuwahi kufanya biashara. Ni watu ambao walikuwa maofisini kwa miaka mingi, hawana competence katika kufanya biashawa wao wenyewe. Hatu Wall Street hapa Tanzania, lakini kama nchi lazima tungezitafutia experts wa kiwango cha juu hizi taasisi ili zisukume mbele gurudumu. Nionavyo mimi hata wale waliopeleka fedha zao Precission wanaelekea kule kule kwa NICOL, haiwezekani kampuni iliyopata faida mwaka mmoja uliopita iangukie kwenye biggest loss in aviation industry.

Athari za kutokuwa na usimamizi imara katika masoko ndio hizo zinadidimiza uchumi na hivyo watu wengi kushindwa kupeleka fedha zao kwenye MF. Mfano mkubwa kuna vijana wa Kitanzania kwa mamia sasa hivi wananunua maplot makubwa ya mashamba huku hawajui hata watayafanyia nini. Nilishuhudia jamaa yangu akitoa milioni 20 miaka miwili iliyopita kununua shamba ambalo hadi leo ni pori na sidhani kama amelitembelea katika huu mwaka. Hiyo hela angeipeleka katika mutual funds huenda angejipatia ka return kidogo, lakini the risk is too high. Vijana wanaona heri wamiliki ardhi ambazo huenda watakufa na kuziacha hazina hata mti wa mwembe kuliko hizo Mutual Funds
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…