SababuYaKununua
Member
- Nov 26, 2018
- 14
- 38
Wiki Iliyopita nimepigiwa simu na Rafiki yangu akihitaji msaada namna ninavyoweza kupata suluhisho ya jambo limetokea kwenye kampuni "Y" ambayo ni ya rafiki yake juu ya manunuzi waliyofanya mtandaoni.
Case ilikua kama hivi, Kampuni Y ya Tanzania ilikua inahitaji kemikali yenye form ya powder kwa ajili ya matumizi ya shughuli zao, kwa vile hawakuwahi nunua China na wanataka kununua China, walitumia mtandao wa Alibaba ambako huko walikutana na kampuni ya kuuza ( trading company )sio kiwanda ( manufacturer) ambapo baada ya maswali mengi walisema wazi kua wao sio kiwanda ni kampuni ya kuuza ( trading company).
Kwakua Kampuni "Y" ilikua inahitaji mzigo kwa uharaka kidogo, walikubaliana na kampuni hiyo kua kwasababu wao sio Kiwanda (manufacturer), wao wapewe maelezo ya bidhaa iweje ( product specifications), wao wafanye mazungumzo na kiwanda na bill ( proforma invoice) kutoka kiwandani moja kwa moja na Kampuni Y ya Tanzania, ambapo malipo yatafanywa moja kwa moja kiwandani na sio kampuni ya Kuuza. Taratibu zikafatwa kama makubaliano tajwa hapo juu.
Mzigo ulipofika Tanzania, jambo lisilokuwa la kawaida, umefika mzigo tofauti na ule ambao Kampuni Y ya Tanzania imeagiza. Wakafanya mawasiliano na kampuni ya kununu iliyowasaidia kupata kiwanda ikakataa kuwa order iliyowekwa na mzigo uliotumwa ni sahihi, wakajaribu kuuliza kiwanda moja kwa moja. Kiwanda kinasema mzigo uliotumwa na order iliyowekwa na kampuni ya Kununua ni sawa na bidhaa waliyotuma Tanzania. Kiwanda na Kampuni ya kununua wote Hawapokei simu (wiki 2 kabla ya Mwaka mpya wa Kichina), hawahitaji mawasiliano, manunuzi yaliyofanyika ni zaidi ya milioni 30, hii inaweza kuwa
Swali linakuja kama wote, kampuni ya kununua na kiwanda wanasema order iliyowekwa na mzigo uliotumwa ni sawa na hauna shida, wakati mwenye mzigo anasema order aliyoweka na mzigo ni tofauti. Shida ilikua wapi?
Karibu kwa mawazo
Jumatatu njema.
a hasara....