Tusaidiane mawazo wadau kuhusu kilimo

mosktear

Member
Joined
Nov 9, 2014
Posts
7
Reaction score
0
Mimi ni mfanyakazi katika mahali (mwajiriwa) hapa Dar ila kama unavyojua kwa maisha ya hapa mjini ajira pekee utachelewa sana kupata maendeleo hivyo nawaza kidogo nnachopata kwenye ajira huku nikitupie kwenye kilimo angalau kiongezeke ila sijui nianzie wapi hivyo niombe mawazo yenu wakuu na ushauri wenu kuhusu yafuatayo;

- Kilimo gani kitanifaaa niweze mudu ajira na kilimo chenyewe.
- maeneo kinapolimwa/stawi vizuri
- Upatikanaji wa mashamba, gharama za kuendesha kilimo chenyewe, upatikanaji wa masoko na yanapopatikana pia.
-msimu wa kilimo chenyewe.

Karibuni Wakuu nawasilisha kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ya hewa ya Dar sidhani kama inaruhusu kilimo, vyanzo vya maji vipo? Kuna mdau alilima nyanya maeneo ya Bagamoyo changamoto kwake ilikuwa Joto, Yaani jioto ni kali sana kiasi kwamba mauwa yana kauka na kupukutika. Kama ni mpenzi wa kilimo omba uhamisho, hamia mikoani.
 
Kwa kweli kwa ushauri uliompa umemaliza kila kitu. Kama kweli anapenda kilimo aombe uhamisho; atakuja kukushukuru siku moja.

God save us
 
Acha kumtisha mwenzako labda hujawahi kuishi dar chanika,mvuti,pugu bangulo,mbande ni baadhi ya maeneo ya dar ambayo watu wanalima mahindi, mihogo na mazao mengine.vilevile kigamboni kimbiji,malale,kibada ,geza ulole Kuna mashamba makubwa watu wanalima
 
Tembelea kigamboni, chanika,mvuti,masaki ya chanika,mbagala,mabwe pande,bunju Kuna mashamba mengi utapata taarifa zote unazohitaji
 
Asange mkuuu ila kuhamishwa ni ngumu ofisi zipo dar tu labda niache kazi na pia nilimaanisha hatakama ni mkoa wa jirani kama moro, dodoma sio lazima dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, wejamaa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asange mkuuu ila kuhamishwa ni ngumu ofisi zipo dar tu labda niache kazi na pia nilimaanisha hatakama ni mkoa wa jirani kama moro, dodoma sio lazima dar

Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia ya leo hakuna kuaminiana, watu wengi wamepoteza pesa zao kwa kilimo cha kutumia simu. Kilimo kinakutaka uwepo shambani kwenye kila hatua - kupanda, kupiga dawa, kuweka mbolea na palizi zote, lazima usimamie mwenyewe. Kama huwezi hama Dar basi nakushauri tufuta mishe nyingine ya kukuingizia kipato ambayo utaisimamia hapa hapo Dar.
 
OK. Huko kunakilimo ambacho kweli unasema unaenda shamba unalima eka 3 au 4 za mahindi au mhogo? Au ni kilimo cha vishamba vidogo vidogo ambavyo miezi 4 unahangaika nacho, mahindi ambayo hata gunia la 100kg halijai?
 
Sio hekari tatu tu watu wanalima mpaka hekari kumi tembelea maeneo ya pembeni uone
OK. Huko kunakilimo ambacho kweli unasema unaenda shamba unalima eka 3 au 4 za mahindi au mhogo? Au ni kilimo cha vishamba vidogo vidogo ambavyo miezi 4 unahangaika nacho, mahindi ambayo hata gunia la 100kg halijai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…