Tusaidiane namna kukomesha wizi wa nyaya za umeme baada ya kufanya wiring

Tusaidiane namna kukomesha wizi wa nyaya za umeme baada ya kufanya wiring

Mm nakushauri ukibahatika kumkamata mwizi muinamishe umle haswa iwe fundisho kwa wengine.
 
Bei ya waya sokoni kwa TWIN CABLE Ni 2500 kwa mita Moja.

Ukipigwa mita 50 tu,
Ni sawa na LAKI na ushee imeenda[emoji848]
 
Suluhisho ni watu kuacha kununua vitu vya wizi unaweza ukakuta unanunua sehemu vitu bei nzuri kumbe wametoka kukuibia mwezi uliopita
Hii ndio suluhisho kamili kabisa, tatizo ni kuwa binadamu tupo tofauti! Mtu anakuambia kabisa hiki nimeiba kwa mhindi na bado unanunua
 
Daah wezi achana nao. Mi walipita nyuma ya nyumba usiku wakatoboa gypsum board, wakakata waya wakasepa. Imenilazimu kuhamia january hii japo sikupanga kuhamia kipindi hiki.

Niliwatafuta ndugu zangu wa shirika la kijani "nikaongea nao", fasta nikaletewa umeme, nikamwita fundi karudia wiring upande wa nyuma ambapo ndo waliharibu sana, nimeunganisha moto sasa panawaka full usiku.

Namshukuru mungu master bedroom finishing tayari kila kitu, nimehamia kibabe ijapokuwa madirisha sijakamilisha bei ya aluminium imepanda sana, nimenunua jambia na sime nasubiri vibaka wale warudi tena niwatoe utumbo.
 
Back
Top Bottom