Daah wezi achana nao. Mi walipita nyuma ya nyumba usiku wakatoboa gypsum board, wakakata waya wakasepa. Imenilazimu kuhamia january hii japo sikupanga kuhamia kipindi hiki.
Niliwatafuta ndugu zangu wa shirika la kijani "nikaongea nao", fasta nikaletewa umeme, nikamwita fundi karudia wiring upande wa nyuma ambapo ndo waliharibu sana, nimeunganisha moto sasa panawaka full usiku.
Namshukuru mungu master bedroom finishing tayari kila kitu, nimehamia kibabe ijapokuwa madirisha sijakamilisha bei ya aluminium imepanda sana, nimenunua jambia na sime nasubiri vibaka wale warudi tena niwatoe utumbo.