Tusaidieni Elimu kuhusu Upokeaji wa Summons!

Tusaidieni Elimu kuhusu Upokeaji wa Summons!

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Naomba mtusaidie Elimu kuhusu taratibu za Upokeaji wa Summons. Je, ni Nani anapaswa kubeba summons kutoka mahakamani kumpelekea Mdaiwa? Je, Ni yeyote Yule au kuna mtu maalumu?
Je, kuna muda maalumu (namaanisha masaa ya kazi) au saa yoyote Ile ata saa 7 za usiku ni sahihi?
Je, ni sahihi kumpelekea summons Mdaiwa siku 1 au 2 kabla ya siku ya kesi wakati mahakama imetoa summons siku 28 kabla ya kesi, na Mdaiwa amekaa nayo (ameificha) anavizia siku mbili kabla ndio akuletee?
 
Kwa maendeleo ya teknolojia siku hizi zitatumwa hata kwa WhatsApp si chini ya saa 72
 
Kwa maendeleo ya teknolojia siku hizi zitatumwa hata kwa WhatsApp si chini ya saa 72
Kaka Mchana, iyo NI Sawa, lakini hii ya Hadi siku 2 kabla ya kesi imekaaje? Au tuseme ni Kama ngumi za kuvizia??🤣
 
Ipotezee tu, kausha jifanye hujapokea chochote.
 
Anaepaswa kupeleka summons ni third party ambaye sheria ya local goverment inamtambua. Mfano mjumbe
 
Nani anapaswa kubeba Summons?

Kwa kawaida, Summons hubebwa na Maafisa wa Mahakama, Askari Polisi, Wakili wa Mdai

Katika baadhi ya mazingira, Mahakama inaweza kumruhusu mtu yeyote mzima ambaye siyo afisa wa Mahakama kupeleka Summons.

Muda wa Kupeleka Summons:

Kwa kawaida, Summons hutakiwa kupelekwa wakati wa saa za kazi, yaani kuanzia asubuhi hadi jioni. Isipokuwa Katika baadhi ya kesi za dharura, Mahakama inaweza kutoa amri maalum ya kupeleka Summons wakati wowote, hata usiku.

Siku ya Kupeleka Summons

Kama Mahakama imetoa Summons siku 28 kabla ya kesi, Mdaiwa anapaswa kupewa muda huo ili aweze kujiandaa.
 
ya nin ujipe shida. lipia elf 50 kwa dalal wa mahakama kama unashindwa kum face muhusika/ mdai wako.
 
Back
Top Bottom