Nani anapaswa kubeba Summons?
Kwa kawaida, Summons hubebwa na Maafisa wa Mahakama, Askari Polisi, Wakili wa Mdai
Katika baadhi ya mazingira, Mahakama inaweza kumruhusu mtu yeyote mzima ambaye siyo afisa wa Mahakama kupeleka Summons.
Muda wa Kupeleka Summons:
Kwa kawaida, Summons hutakiwa kupelekwa wakati wa saa za kazi, yaani kuanzia asubuhi hadi jioni. Isipokuwa Katika baadhi ya kesi za dharura, Mahakama inaweza kutoa amri maalum ya kupeleka Summons wakati wowote, hata usiku.
Siku ya Kupeleka Summons
Kama Mahakama imetoa Summons siku 28 kabla ya kesi, Mdaiwa anapaswa kupewa muda huo ili aweze kujiandaa.