Mie mara ya kwanza kwenda Dar nilishukia Kimara, sasa siku ya pili nikatakiwa kwenda Kkoo nikapandishwa mabasi wakaniambia niende nayo mpaka mwisho na baadae nipande hayo hayo nitarudishwa kimara. Kasheshe baada ya kumaloza kilochonipeleka nikapanda basi likaniacha mnazi mmoja jamaa kasema ndio mwisho, nikachanganyikiwa maana sikujua wapi niende na nani nimuulize niliambiwa nisiamini watu nilizunguka kwa masaa kadhaa nikajikuta posta ya zamani kimiujoza nikapanda basi lilioandikwa kimara na ndio ikawa bahati yangu. Baada ya hapo nikawa napanda mabasi naenda nayo mpka mwisho wa safari na kurudi na ndipo nilipojifunzia vituo vya mabasi ya Dar