Tuseme tu ukweli, nani hajawahi kupotea mitaa ya Dar?

Tuseme tu ukweli, nani hajawahi kupotea mitaa ya Dar?

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
1,888
Reaction score
3,352
Nani hajawahi kupotea hapa town(dar es salaam) akaenda mahali bila kuulizia? Mimi mwaka jana nilizunguka sana pale Posta nilikuwa naitafuta ofisi za TNMC kuna form nilikuwa nazipeleka za sister angu yupo mikoani uwezi amini ofisi nilikuwa naipita palepale mpaka wale wanaofanya shughuli maeneo ya karibia pale wakawa hawpajui ndo nikaamini hakuna mwenyeji posta wote ni wakuja tu..
 
Duuh ni nyie tuu mie mbona sijawahi potea hata siku moja na nimeishi kkoo miaka mitatu
 
Yaani nikipotea sehemu huwa siulizi njia...ata kama nilikuwa na mpango wa kwenda Tegeta ila ghafla nikajikuta Gongo la Mboto, siulizi njia....kila nikitaka kumuuliza mtu, namuona huyo mtu kama mpotoshaji tu....Mkuu jifunze kusoma ramani...ata kama ni ya mtaani kwenu, kujua ramani ya mahali fulani ni dili sana.
 
Mie mara ya kwanza kwenda Dar nilishukia Kimara, sasa siku ya pili nikatakiwa kwenda Kkoo nikapandishwa mabasi wakaniambia niende nayo mpaka mwisho na baadae nipande hayo hayo nitarudishwa kimara. Kasheshe baada ya kumaloza kilochonipeleka nikapanda basi likaniacha mnazi mmoja jamaa kasema ndio mwisho, nikachanganyikiwa maana sikujua wapi niende na nani nimuulize niliambiwa nisiamini watu nilizunguka kwa masaa kadhaa nikajikuta posta ya zamani kimiujoza nikapanda basi lilioandikwa kimara na ndio ikawa bahati yangu. Baada ya hapo nikawa napanda mabasi naenda nayo mpka mwisho wa safari na kurudi na ndipo nilipojifunzia vituo vya mabasi ya Dar
 
Nakumbuka nilienda kariakoo ,nikaambiwa niende soko dogo la shimoni pale,nikaingilia mlango wa shimoni nikatokea soko dogo kwa nje ,wacha nipotee nisijue magari ya tegeta yako wapi nilizunguka mitaa karibu yote k/koo
 
Mlikuja lini "Mjini"?
 
Utapoteaje na una smartphone duh" labda huko zamani maana hata mm nikiwaza kaka standard 5 nilishawah kupotea pale kkoo niliachwa na niliyekua nae yani sikuhiyo niliona rangi zote..nilikuja kupatikana badae sana pale kituo cha police msimbaz
 
unaanzaje kupotea? labda uwe mtoto au mgeni
 
jsna niikuwa naenda serengeti...lakini nkajikuta mbagala rangi tatu
 
Kupotea ni hadi umkanyage yule Mdudu Mweusi... hata kwako unapapotea lazima
 
Mie mara ya kwanza kwenda Dar nilishukia Kimara, sasa siku ya pili nikatakiwa kwenda Kkoo nikapandishwa mabasi wakaniambia niende nayo mpaka mwisho na baadae nipande hayo hayo nitarudishwa kimara. Kasheshe baada ya kumaloza kilochonipeleka nikapanda basi likaniacha mnazi mmoja jamaa kasema ndio mwisho, nikachanganyikiwa maana sikujua wapi niende na nani nimuulize niliambiwa nisiamini watu nilizunguka kwa masaa kadhaa nikajikuta posta ya zamani kimiujoza nikapanda basi lilioandikwa kimara na ndio ikawa bahati yangu. Baada ya hapo nikawa napanda mabasi naenda nayo mpka mwisho wa safari na kurudi na ndipo nilipojifunzia vituo vya mabasi ya Dar
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Utapoteaje na una smartphone duh" labda huko zamani maana hata mm nikiwaza kaka standard 5 nilishawah kupotea pale kkoo niliachwa na niliyekua nae yani sikuhiyo niliona rangi zote..nilikuja kupatikana badae sana pale kituo cha police msimbaz
[emoji23] [emoji23]
 
mwisho wa yote dawa ni kutumia smart phone application za ramani zipo so unaweza kujua upo wapi na unapotaka kuelekea ni wapi etc
 
Back
Top Bottom