Tukiona vijana wanajinyima starehe, anasa, matumizi holela tunafurahi sana.
Leo ni siku ya vijana kufunguka: Ni changamoto gani ulikutana nayo au unakutana nayo wakati unajenga nyumba yako? Umekwama wapi?
Shea nasi uzoefu tujifunze kwa pamoja.
Ujenzi wetu vijana wengi wa Kitanzania ni wa gharama kubwa kutokana na sababu zifuatazo
1. Kujenga bila ya kuwa na plan (Phases)
mfano mtu anaweza akaanza kujenga nyumba akiwa na milioni kumi.. lakini kiuhalisia hajapiga hesabu nyumba yake gharama kamili ni kiasi gan..
Wala haja anticipate gharama za uendeshaji mradi ambazo haziko wazi.. kama vile usafiri wa material.. upatikanaji wake.. gharama za maji.. na
vitendea kazi vingine.. anajikuta katika ile kumi 10% hadi 20% inaingia kwenye hidden charges ambazo hakuzifanyia utafiti..
Matokeo yake pesa inakata.. nyumba haijafikia ambapo alitegemea ifike.. huku akiwa kabakisha material ingine lakin hana pesa ya uendeshaji mradi .. hapo unajikuta mtu anapiga gape la miaka mingine kama 2 - 5 ndo walau aanze tena kusogeza nyumba.. lakini ile material haina ubora wa kutumika tena
2. Sababu ingine ni kujenga kutokana na jinsi pesa inavyopatikana yaani unapata 2m unashusha tofal.. unakaa miez sita unapata 2m unaita fundi mnanunua cement, mchanga na mengineyo mnasogeza kozi mbili tatu.. ujenzi wa hiv unajikuta unatumia gharama kubwa zaid hadi nyumba iishe..
Na ukitumia 5+ yrs katika ujenzi utakuta nyumba imeanza kuchoka kabla haijaisha.. sababu nyumba ambayo ni pagala au haikaliwi inachakaa haraka zaid.. kuliko inayokaliwa
3. Kutumia mafundi wetu waliojifunzia ujenzi mtaan ambao kiuhalisia hawana utaalam wa ujenzi.. yeye anajua kupanga tofali.. wamekariri vitu vingi tu ambavyo wanatuingiza chaka.. maana tunawatumia wao kama washauri wa kiufundi kumbe na wao watupu.. mbaya zaidi hawajui kuwa hawajui
Kwa hiyo unajikuta utatumia gharama nyingi kurekebisha makosa .. ndo maana wanaaema ujenzi wa kimaskini hauishi.. sababu fundi wa mtaan atakupa gharama ndogo.. ila kila leo utajikuta unarekebisha hiki au kile .. iwe sababu ilikuwa ni ushauri mbaya wa kiufundi.. au ushauri mbaya wa kununua vitu feki ambavyo havidumu.. aidha amefanya makusudi au bila kujua
Hata mara baada ya nyumba kuisha.. mara mabat yanavuja.. mara nyufa zimeongezeka.. mara mbao za paa zina hiki.. mara milango na grills kuna shida yaan kila mwaka walau una kitu cha kurekebisha.. iwe mfumo wa maji.. taka au maji safi au umeme au nyumba yenyewe..
Yote kwa yote changamoto za ujenzi zinakuwa kubwa zaid kama ndo unajenga ujenz wa kudunduliza.. maana kichwani akili yako itakuwa inawaza unafuu kwenye kila kitu kuliko ubora wa kitu.. kuanzia ufundi, vitendea kazi hadi material yenyewe.. mwisho wa siku unajikuta umeingia gharama zaid ..
Kikubwa hataka kama unajenga ujenz wa kudunduliza hakikisha una consider kila kitu na kila kila hatua umeifanyia upembuzi yakinifu..
Na njia rahis ya kufanya hata kama huna ABC za ujenzi kama umepanga kuanza ujenzi desemba ww leo hii tafuta mafundi hata wa 3 au wa 5 tofauti nenda nao site kila mtu na mda wake bila wao kujua hata ukitumia gharama kidogo sio mbaya
Kaa nao chini wahoji wakupe mchanganuo kiufundi.. wala usihangaike nao kwenye gharama waache wataje gharama zao sababu hapo ww unataka kujua je unaweza kumtumia kama mshauri wa ufundi na anajua anachokifanya?, hapo ww unawafanyia usaili wa utaalam wao ni wa kiwango gani
Katika mafundi wa tano utakuja kujua yupi anajua kupanga tofali tu lakini hana utaalamwa ujenzi na yupi kabobea kwenye nini.. itakupa picha nani unaweza mtumia kwenye level ipi kama ni full package au ama la..
Unawahoji kuanzia ufundi wao hadi ubora wa material zikakazo tumika na kila jibu akupe sababu kwa nn anahis hiki bora kuliko hiki.. kama amekariri utajua tu..
Mafundi wetu wengi wa mtaan iwe ujenzi, umeme au magari hawajuagi kusema kitu flan sijui.. ndo wanatuingizaga sana hasara