Tuseme ukweli Zanzibar mpira unachezwa

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Unapozunguuka mji wa Zanzibar na viunga vyake hasa muda wa jioni kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili unusu maranyingi utakutana na hali ambayo ilikua ni kawaida kwa jiji la Dar es Salaam miaka ya tisini kurudi nyuma. Utakuta vijana wakiwa katika makundi ya rika mbalimbali wakicheza soka, iwe viwanjani, mabarabarani au katika vichochoro vya mji mkongwe. Wanafanya hivo bila kua na makocha wa kuwasimamia au academy za kuweka kumbukumbu za takwimu za magoli na idadi ya mechi wanazocheza.

Jambo la muhimu kwao ni kucheza na kuuchezea mpira bila kua na tamaa kwamba siku moja watakuja kuuzwa ulaya au Tanzania Bara kama wachezaji wa kulipwa . Wanacheza kwa kujifurahisha, wanacheza kwa kuupenda mchezo wanacheza kwa passion! Haya yalikuwepo Dar miaka miingi iliyopita na yakatuletea matunda ya kuzalisha wachezaji wenye kuujua mpira na mpira ukawajua, wachezaji ambao utaenda uwanjani ukuwa na hamu ya kumuona akicheza, Niko Njohole au Sikinde Mbunga au Gagarino au Jumapondambwbwe au Athuman China kuwataja wachache. Waliujua mpira japo sera za nchi wakati wao zilikua hazitoi fursa za wazi kuweza kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.

Na kwakweli hii ni aina ya kujifunza soka hata kwa watu kama Brazil. Soka la ukweli, soka la ufundi, soka la sanaa, soka la kufurahisha , soka la MTAANI. Tele Santana mwalimu wa timu ya taifa ya Brazil 1982 na 1986 na muumini mkubwa wa samba aliwahi kusema, Samba falsafa yake ni kua Cheza vizuri sana uwafurahishe watazamaji maana soka ni sanaa, cheza soka la kushambulia na ufunge magoli. Sasa hivi hakuna tena . Kila kitu kimetekwa na zinazoitwa soccer academies, ambapo kiuhalisia pamoja na gharama ya kuendesha vituo hivi wanaopata fursa ta kucheza ni wachache sana na hawafundishwi kuuchezea na kuupenda mpira

HAYA NDIO YANATOKEA HUKU BARA, WACHEZAJI WA LIGI KUU HAWAWEZA KUMILIKI MPIRA! Watu wameacha kucheza mpira wanajishughulisha na takwimu sijui assist, sijui kacheza mechi ngapi nk.

Zanzinziba mpira unachezwa mitaani na matokeo yake tutayaon amuda si mrefu
 
Ni kweli mkuu..
huku znz mazoezi ni sehem ya maisha yao, hata wanaweke asubuhi na jioni utawaona kwenye mazoezi mbali mbali..
Sio bara, mazoezi mpaka Samia suluhu atoe tamko..!!
 
Ni kweli mkuu..
huku znz mazoezi ni sehem ya maisha yao, hata wanaweke asubuhi na jioni utawaona kwenye mazoezi mbali mbali..
Sio bara, mazoezi mpaka Samia suluhu atoe tamko..!!
Mazoezi ni jambo la utamaduni wa watu kama hayapo kwenye damu utafanya siku moja au wiki then utaacha, lakini kwa Zanzibar mwamko upo juu sana kwa watu kushiriki mazoezi na michezo kwa ujumla
 
Hata kama ni kweli, hilo haliwapi kibali cha kutukana Watanzania wenzenu kuwadharau kama shit?

Ni mara ngapi team ya bara imefanya vizuri kuliko Znz Heroes?


Asiejua akipatia hujisifu mpaka anakunya hadharani. Ndicho hao vijana wenu walichofanya
 
Hizi timu za Zanzibar kama Polisi au Kmkm zikishiriki michezo ya Caf huwa zinatolewa kwa goli si chini ya 7
 
Hata kama ni kweli, hilo haliwapi kibali cha kutukana Watanzania wenzenu kuwadharau kama shit?
Ni mara ngapi team ya bara imefanya vizuri kuliko Znz Heroes?
Asiejua akipatia hujisifu mpaka anakunya hadharani. Ndicho hao vijana wenu walichofanya
Ni timu gani kwenye mashindano gani zisizotambiana kabla ya kupambana? Ni timu gani kwenye mchezo gani ikishinda haishereheki kwa sababu tu iliyemshinda atajisikia vibaya? Ni ushangiriaji gani wa namna hiyo utaofanyika bila ya kujibu majilabu ya aliyeshindwa aliyoyatoa kabla ya pambano? Kama majilabu hayo yalikuwa ni matusi, utategemeaje atayeyajibu baada ya ushindi asijibu matusi pia?
Binafsi matusi hayakufanywa na wachezaji wala viongozi wa Zanzibar wala wa Tanzania Bara; wala hayakufanyika kiwanjani au mitaani. Matusi mengi yalitolewa kwenye mitandao ya kijamii, ambako hakuna kigezo cha kumtambua mhusika. Hiyo mitandao si ya Wazanzibari watupu. Utasemaje waliyoyatoa lazima wawe Wazanzibari? Mbona wanaomtukana Wenger na Arsenal yake wote si Waingereza? Mbona wanaoshsbikia timu za Taifa za nje mpaka wakafikia kutukanana huwa siyo wote ni raia wa nchi hizo? Si tulishuhudia matusi mpaka huku kwetu Brazil ilipofungwa saba nyumbani na Ujerumani kwenye fainali ya KD?
Waswahili wanasema anayejibu hana tusi, mwenye tusi ni aliyetukana mwanzo. Tusiitumie mitandao ya kijamii kwa kuanza kutukana, ili tusichochee kujibiwa matusi. Anayetukanwa mwisho ndiyo anayetukanika zaidi.
 
Zanzibar hii hii ninayoijua mimi au ipi nyingine!? Wachezaji wao akina Makame, Ninja nk!? Wanacheza kama vita. Mguu shingo kidevu!!
CECAFA wanabugizwa magoli 11 na Eritrea.

Au mnaongelea Zanzibar ipi!?
JUZI LIGI KUONESHWA NA AZAM KELELE ZIMEANZA.

Mapinduzi Cup miaka yote bara wanachukua.

JKU wanacheza na Simba U20 wanabugizwa goli za kutosha.
 
Kina Mudathir Yahaya, Agrey Moris, Makame, Feitoto, Abduhalim Humud nk
 
Wala Urojo Hao Wengi Wamerojoka kama Urojo.....ni Mmoja Kwa Kumi.
Ndo maana nafasi Wanazopewa Kushiriki Michuano ya CAF huwa ni Vituko Vitupu.
 
Kina Mudathir Yahaya, Agrey Moris, Makame, Feitoto, Abduhalim Humud nk
Mzee hao ni wachezaji wa kawaida sana mwanangu.
Feitoto na Ndemla ni group moja.
Usichanganywe na miluzi mingi kumsifia Fei, hizo ni mbwembwe za kisiasa kwa sababu rais ni mzanzibar.

Zanzibar ilishawahi kutoa mchezaji mmoja tu ambaye ni Dua Said.
Hivi hao CECAFA wamewahi chukua kombe!?
 
Zanzibar ilishawahi kutwaa kombe CECAFA Senior Challenge Cup tena kwenye ardhi ya ugenini. Walilichukulia kombe Uganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…