Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Unapozunguuka mji wa Zanzibar na viunga vyake hasa muda wa jioni kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili unusu maranyingi utakutana na hali ambayo ilikua ni kawaida kwa jiji la Dar es Salaam miaka ya tisini kurudi nyuma. Utakuta vijana wakiwa katika makundi ya rika mbalimbali wakicheza soka, iwe viwanjani, mabarabarani au katika vichochoro vya mji mkongwe. Wanafanya hivo bila kua na makocha wa kuwasimamia au academy za kuweka kumbukumbu za takwimu za magoli na idadi ya mechi wanazocheza.
Jambo la muhimu kwao ni kucheza na kuuchezea mpira bila kua na tamaa kwamba siku moja watakuja kuuzwa ulaya au Tanzania Bara kama wachezaji wa kulipwa . Wanacheza kwa kujifurahisha, wanacheza kwa kuupenda mchezo wanacheza kwa passion! Haya yalikuwepo Dar miaka miingi iliyopita na yakatuletea matunda ya kuzalisha wachezaji wenye kuujua mpira na mpira ukawajua, wachezaji ambao utaenda uwanjani ukuwa na hamu ya kumuona akicheza, Niko Njohole au Sikinde Mbunga au Gagarino au Jumapondambwbwe au Athuman China kuwataja wachache. Waliujua mpira japo sera za nchi wakati wao zilikua hazitoi fursa za wazi kuweza kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania.
Na kwakweli hii ni aina ya kujifunza soka hata kwa watu kama Brazil. Soka la ukweli, soka la ufundi, soka la sanaa, soka la kufurahisha , soka la MTAANI. Tele Santana mwalimu wa timu ya taifa ya Brazil 1982 na 1986 na muumini mkubwa wa samba aliwahi kusema, Samba falsafa yake ni kua Cheza vizuri sana uwafurahishe watazamaji maana soka ni sanaa, cheza soka la kushambulia na ufunge magoli. Sasa hivi hakuna tena . Kila kitu kimetekwa na zinazoitwa soccer academies, ambapo kiuhalisia pamoja na gharama ya kuendesha vituo hivi wanaopata fursa ta kucheza ni wachache sana na hawafundishwi kuuchezea na kuupenda mpira
HAYA NDIO YANATOKEA HUKU BARA, WACHEZAJI WA LIGI KUU HAWAWEZA KUMILIKI MPIRA! Watu wameacha kucheza mpira wanajishughulisha na takwimu sijui assist, sijui kacheza mechi ngapi nk.
Zanzinziba mpira unachezwa mitaani na matokeo yake tutayaon amuda si mrefu