Tuseme ukweli Zanzibar mpira unachezwa

Zanzibar ilishawahi kutwaa kombe CECAFA Senior Challenge Cup tena kwenye ardhi ya ugenini. Walilichukulia kombe Uganda
Zanzibar imechukua kombe Mara ya mwisho 1990 nchi ikiwa chini ya mwinyi Dua Said akicheza.
 
Hebu nitajie mwaka gani. Usikete taarifa nusu nusu humu Mzee.
Mwaka siwezi kukumbuka hadi mwaka labda wadau humu watatusaidia. Tena kuna wakati wakashika pia nafasi ya tatu kisha wacjezaji wakagawana pesa za zawadi ndani ya ndege

Zanzibar ina baadhi ya wachezaji wazuri. Sema kwa vile hawapo kwenye timu moja ndio maana vilabu vyao havifanyi vizuri sana

Kwani huku bara ukiondoa Simba na Yanga timu gani inaweza kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Afrika kwa mafanikio? Hata hao Simba, Yanga, Azam, Namungo au hata Biashara bila wachezaji wa nje ya Tanzania unadhani wanaweza kufanya lolote kimataifa???!!!!
 
Acha kurukaruka umesema CECAFA SENIOR CHALLENGE.
Tumalize kwanza hilo.
Mara ya mwisho Zanzibar kuchukua kombe ni 1990 Dua Said akiwa mchezaji.

Pili kuna mapinduzi cup ambayo huunganisha ZANZIBAR na bara
Timu ya mwisho kutoka Zanzibar kuchukua kombe ni Miembeni SC
Mwaka 2008.

Nataka tuongee kwa facts siyo mihemko.
 
Zanzibar hawana wadhamini kama huku bara vinginevyo vijana wao wana vipaji vikubwa kama huku.
 
Zanzibar hawana wadhamini kama huku bara vinginevyo vijana wao wana vipaji vikubwa kama huku.
Siku hizi mpira sio wa ridhaa. Nipatie hizo statistics zinazoonesha hao vijana wanavipaji vikubwa. Tungewaona mapinduzi cup wakichukua makombe. Au wangekuwa wanapiga chenga kali
 
Zanzibar ilichukua kombe la CECAFA Senior Challenge Cup mwaka 1995 kwa kuwafunga wenyeji Uganda Cranes 0-1. Walifanya hivyo baada ya Tanzania Bara kua wameshinda kikombe hicho 1994 pale Nairobi

Tanzainia Bara ilikuja kuchukua tena Cecafa 2010, kwahiyo hatucheka viwango vyetu. Bahati mbaya timu ya Taifa ya Visiwani hairuhusiwi kushiriki yenyewe kwenye michuano ya Afrika inayoandaliwa na CAF wala ile ya FIFA World Cup ambapo tungeona vipaji vyao kikikusanywa na kutumika
 
Sasa unaposema Zanzibar wanacheza nimekuuliza kwa statistics zipi.
Au unapoona vijana wanapiga dana dana mia mia mtaani ndio unasema wanajua kucheza!!
Zanzibar kuna mapinduzi cup. Mbona hatuoni uwezo huo kwenye hilo kombe!?

Usilazimishe 2 kuwa 100.
 
Siku hizi mpira sio wa ridhaa. Nipatie hizo statistics zinazoonesha hao vijana wanavipaji vikubwa. Tungewaona mapinduzi cup wakichukua makombe. Au wangekuwa wanapiga chenga kali
Feisal Salum. Motisha ndogo huko visiwani vinginevyo wanao uwezo mkubwa wa kuucheza mpira.

Mechi moja ya ligi kuu unguja pato la kiingilio halizidi tshs 10,000 unategemea utachezwa mpira hapo?!!
 
Sasa unaposema Zanzibar wanacheza nimekuuliza kwa statistics zipi.
Au unapoona vijana wanapiga dana dana mia mia mtaani ndio unasema wanajua kucheza!!
Zanzibar kuna mapinduzi cup. Mbona hatuoni uwezo huo kwenye hilo kombe!?

Usilazimishe 2 kuwa 100.
Wachezaji wao wote wazuri wako Bara.
 
Wewe unawajua, kama huwajui pole sana. Sipo kwenye chumba cha mtihani hapa.

Umesema Zanzibar haijawahi kuchukua Challenge nilipokwambia ukasema nikutajie mwaka nikataja. Sasa unataka nitaje wachezaji wa Zanzibar wanaocheza Bara! Basi tufanye hakuna
 
Feisal Salum. Motisha ndogo huko visiwani vinginevyo wanao uwezo mkubwa wa kuucheza mpira.

Mechi moja ya ligi kuu unguja pato la kiingilio halizidi tshs 10,000 unategemea utachezwa mpira hapo?!!
Fai na Ndemla ni size moja.
Kitu gani kinakufanya useme Zanzibar inawachezaji wazuri!? Mbona huleti takwimu!? Unaanza kulalamikia lingi.
Leta takwimu ya wachezaji hao.
 
Wewe unawajua, kama huwajui pole sana. Sipo kwenye darasa la mtihani hapa
Wewe umeanzisha uzi. Mbona unaleta makasiriko!? 🤣🤣🤣 Siku nyingine usiandike thread kwa mihemko.
Nipatie hao wachezaji unaodai wametoka Zanzibar wanacheza vizuri.

Unaongelea Akina Ninja au!? Makame anayetaka kuvunja mguu wa Kapombe!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…