Tusemezane ya Ukweli: Ni nani humu JF ukiwa unajadiliana naye anakupeleka puta mpaka, unatamani asi ku "Quote" kwa kujawa na hofu

Okay sawa

Hata sijasoma uliyoandika

Upo sahh kwa hayo uliyoandika

Hili hujaanza kulisema leo,na huwa nalizingitia sana. Kwahiyo hapo nimekuandikia wewe hasa ila na wengine kwa ujumla. Kwahiyo usipo soma wewe basi watasoma wengine.

Ili kutilia mkazo hili,huoni huwa na mquote Kiranga japokuwa ana dai ame ni "Ignore" na mimi nalijua hilo,kwa maana yeye au wewe huwa nawafanya kama "Wasila" tu kufikisha ujumbe kwa wengine.

Hili bila shaka limeisha,tujikite kwenye mada.
 
Ishi kuendana na mahali palivyo usilazimishe wote wafate kile unacho wewe, wape nafasi na wengine wakupe kile wanacho, fungua milango ya kupokea vitu vipya kila siku, hapo itakufanya ukomae kiufahamu na itakufanya uishi katika mazingira yoyote.

Hili mrembo mbona huwa nalifanya sana,ndio ile sisi Waswahili huwa tunasema "Kunya anye kuku,akinya bata amehara". Huwa tunapeana sana wasaa wa watu wengine kutoa hoja zao,ndio maana huwa tunajibi hoja zenu,tatizo lenu mwisho wa siku huwa mnakimbia na kuleta malalamiko yasiyo na msingi. Hii si sawa kabisa.

Lakini kuna ujinga mwingine watu wanautetea ambao historia ilishahukumu na matokeo yake yameshaandikwa na wino umekauka. Mambo hayo hata iweje hayawezi kuwa sawa,ila kusikilizana na kujua sababu za hao wayafanyayo kwanini wanayafanya ni jambo la dharura na ni katika kuwafanyia wema pia. Bila shaka umejua hapa nazungumzia nini.

Ahsante.
 
Hahahaha bora ulivyokua hujasoma maana ungepata kizungu zungu ukadondosha simu bureee.

Hao ni wale ambao wanatetea au kudai ya kuwa Dunia inazunguka,jambo ambalo hata kutuambia na kututhibitishia ya kuwa walifanya vipi majaribio na kujia hilo,majibu hawakupi,na ilikuwa lini hawakwambii na kwa kutumia nini hawakwambii,na kwanini wana "Assume" sana,sasa ukiwabana ndio wananza kurauka na kukutuhumu wewe mdini au wewe mbishi au wewe mjinga au wewe una elimu ndogo,hapo ameshashindwa hoja,sasa kama wanaweza kweli huu mtamnange wa kuthibitisha ya kuwa Dunia inazunguka wauanzishe halafu uone wanavyokimbia. Tatizo wakiona yale ma formula ya "Culculus" na zile nadharia za kina "Schrodinger" wanaona maisha ndio hayo wanasahau kuhoji ilikuwaje mpaka watu hao wakafikia hitimisho za nadharia zao na "Equations" zao.
 
Imagine huyu mtu anakwambia jua linazunguka dunia

Imagine what kind of stupid person you are
 
Ndugu yangu Zurri , iko hivi, kama lengo lako ni kubishana au kutafuta ushindi, daima utajikuta unaogopa au kuna watu unahofu nao kwa vile wewe kuibuka kidedea ni muhimu na jambo la maana zaidi kwako.

Kwa upande wangu sihofii mtu yeyote ila naheshim sana mawazo na michango ya kila mtu. Mabishano yasiyomaana yakizidi huwa nasema tu " You are right Sir" kwa kuwa lengo la huyo mtu ni kubishana, lakini hapa napo inategemea unatafsiri vipi hoja na ubishi.

Ushauri wangu, kwenye jambo lolote lile, hakikisha unalielewa vizuri kiasi cha kumweleza mwingine aelewe kirahisi. Pia kuna watu wanaelewa zaidi yako, uwe tayari kuyapokea mawazo yao, kuyachambua na kupima kuona usahihi wake. Utajikuta unaongeza ufaham wa jambo.

Pili, ukiona mnapishana na mtu kwenye hoja au kutofautiana nae, jua tatizo sio yeye wala wewe, kumbuka mna vyanzo tofauti vya taarifa na elimu, pia mnatofautiana kiwango cha uelewa. Ni kiasi cha kuchukua muda wa wewe kupitia na kulinganisha kupata uhakika zaidi. Haina haja ya mikwaruzano.

Mwisho, ukiona mtu analeta ubishi badala ya kujadili hoja kwa staha, unaendelea na mambo mengine!

Barikiwa sana
 
Wengi wanapatikana jukwaa la jamii intelligent. Hasa ukutane na wapagani kwenye thread yako/zao,au waabudu shetani/mizimu. Hawa ni watu wabishi kuliko wote na wanakera. Ngao yao kwenye mijadala ni ujinga walionao.
 
Imagine huyu mtu anakwambia jua linazunguka dunia

Imagine what kind of stupid person you are

Sababu hii ni elimu,weka hoja zako kama wewe unasema ukweli kisja nikuulize maswali,ukijibu maswali yangu wewe,mimi naacha kutumia hii Id hapa jf. Najua huna uwez huo. Ukweli husemwa,mnaojiita Wanasayansi wa kukariri na kiwa wavivu wa kufikir na kuhoji na mmaojiita "Wakana Mungu" huwa hamna uwezo wa kujenga hoja kwa dhati yenu kulingana na uelewa wenu zaidi mnakariri kile ambacho waliwaza wakubwa wenu,ndio maana hata maswali mnayoulizwa huwa hamjibu mnaishia kutu tuhumu ya kuwa hatuna akili mara ooh hatuwezi kuelewa. Hivi vituko huwa naviona jf pekee,pale mtu anapoongelea jambo ambalo hana elimu nalo.

Elimu haiongopi,mpaka roho zenu zitakapo tengana na miiki yenu na ukae na wakubwa zenu hamtaweza kuthibitisha ya kuwa Jua halitembei au kuzunguka na Dunia inatembea.


Sisi tulianza kuwasoma wakubwa zenu katika hizo nadharia zenu,huku kwenu tunawapuuza tu.

Nipo.....
 
Ndugu yangu @Zurri , iko hivi, kama lengo lako ni kubishana au kutafuta ushindi, daima utajikuta unaogopa au kuna watu unahofu nao kwa vile wewe kuibuka kidedea ni muhimu na jambo la maana zaidi kwako.

Umesema kweli kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…