Tushachoka kubembeleza undugu, itapendeza Ufaransa ikiwapa Morocco kipigo cha mbwa koko wapigwe mpaka wachakae

Tushachoka kubembeleza undugu, itapendeza Ufaransa ikiwapa Morocco kipigo cha mbwa koko wapigwe mpaka wachakae

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Offcourse tunajua kuna tofauti kubwa kati yao na sisi hasa linapokuja suala la asili yao, Lakini kweli wakatae hata undugu wa kiafrika kwamba wapo nasi ndani ya bara la Africa?

Morocco wametukataa, yaani wanaona wao siyo ndugu zetu ni kwamba tunajipendekeza. Basi ndiyo tumekoma hatujipendekezi tena.

Kwa hali hii nahamia kuishabikia Ufaransa, hata huko France bado wapo ndugu zetu kibao ambao walikuwa na mchango mkubwa kushinda kombe la dunia 2018 na hawakuwa na tatizo lolote walivyopewa sapoti na waafrika ... wapo kina Dembele, Mbappe, Pogba, Camavinga, Konate yule dg aliyefunga juzi na England na wengine kibao. Sasa tunaachaje kuwasapot France?

Morocco wapigwe kama ngoma !! kinyume na hapo ushindi wao utatunyanyasa hasa waafrika weusi (hata maji ya kunde na kina brown) waliopo chini ya jangwa la Sahara.

Nakazia pia hata hio ijumaa kwenye kutafuta mshindi wa 3 wapigwe tena.
 
Unajifurahisha? Hawakujui hao wote wawili sidhani hata kama kuna mchezaji wa Ufaransa anaifahamu nchi inayoitwa Tanzania
 
Hata mimi siwakubali kabisa morocco. ati alisema ushindi huu ni kwa ajili ya waarabu na waislam!
 
Kwahio Ufaransa ndio Ndugu zako ?

Ni kwamba Morocco wanawakilisha Africa watake wasitake..., Ingawa zaidi ya nusu wa hao Wa-Morocco hawakuzaliwa wala hawakai Morocco (ila all that matters wanawakilisha Bara gani as far as FIFA is concerned) hayo mengine sisi watu wa Kabumbu hatuyatambui...

 
1671026359512.jpeg


Kama kuna Football Confederation ambayo wana figisu ni UEFA... bora kombe liende South America ila sio Europe hawa jamaa wajiona ndio kings of football Brazil wasingechukua mara nyingi huenda bara zote zingekuwa na timu moja moja na Europe zote zilizobaki...

Ashukuliwe Joao Havelange (the only non European FIFA President to Date) na ndugu Blatter kwa kuwanyoosha Europe...
 
Majinga Sana hayo, yalivyoleta mambo ya uarabu na dini kwenye mpira ndio niliona ni majinga Sana , mabaguzi na yasiyokuwa na exposure ya jamii nyingine nje ya jamii zao walizolelewa kidini na kilishwa amini kwamba dini Yao ndio Bora kuliko zote, na watu wema na watenda mema wanatokana na watu wa Imani Yao tuu. Hizo ni propaganda unazolishwa ukiwa mdogo kwenye mafunzo ya dini kwa watoto ili uipende dini yako, lakini ikishakuwa mkubwa una uwezo wa kufanya tafiti juu ya Maisha halisi ya watu wa tamaduni na dini nyingine ambao wapo watenda mema saaaana na watenda mabaya vile vile kama ilivyo kwenye jamii yako
 
Ila mwisho wa siku hata kama hao Morocco wanajiona kama Waarabu; still wanapatikana ndani ya Bara la Afrika!

Na hata kocha wao amekiri kuwa timu yao ndiyo ya kwanza kufikia hatua hiyo kutoka Afrika.
 
Waliotenga mabara walikosea ilibidi kuwe na bara la Arabia ambapo nchi za Morocco,Algeria,Tunisia ,Misri na Sudan zingeunganika na Waarabu wenzao.
 
Kwani Morocco ni waafrika? Wale wanaishi Africa tu ila si waafrika.
 
Tatu zitapendeza afu mbili afunge mbappe ili yule baba wa kule argentina asibebe ile golden boot 😍😍
 
Back
Top Bottom