Tushauriane zawadi ya Valentine's Day isiyozidi Tsh 20,000/=

Hivi siku hizi maua na kadi haviruhusiwi kutolewa kama zawadi tena
Maua yanakauka baada siku mbili tatu; hayo tunatumia kama chambo tu mwanzoni.

Kadi maneno yanajirudia rudia tu miaka nenda rudi. Bora nimuandikie shairi kutoka moyoni au kumnunulia kanga yenye fumbo aivae chumbani.

Kumbuka bajeti yangu sh 20000 🙈.
 
Elf 20!

Elf 3 naweka bando nadownload movies kama nne hv. Elf 10 maini, ndizi mzuzu na viungo (karoti, hoho, kitunguu) elf 3 matunda kwa ajili ya juice na elf 4 popcorns chocolates, jojo

Naandaa msosi wa nguvu na juice ya kushushia baada ya hapo tunaangalia movies na kula zetu vichapuza!

The best gift itakuwa muda wangu [emoji4]!
 
Asante,mchanganuo mzuri
Sent using Jamii Forums mobile app
 
''Mwezi wa pili,siku ya kumi na nne ya mwezi,wakati wa jioni,wataishika;watamla pamoja na mkate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu."

Asante nimesoma,hivi ina uhusianao wowote?
Zawadi imesemwa kwenye biblia kitabu cha hesabu 9:11

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpangilio mzuri ,ila vichapuza ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…