Tushauriane zawadi ya Valentine's Day isiyozidi Tsh 20,000/=

Tushauriane zawadi ya Valentine's Day isiyozidi Tsh 20,000/=

mnunulie kiatu simple kama anapenda au mafuta mazuri ya kupaka. kuna mdau hapo juu kasema pads nalo ni wazo zuri utakuwa umemsave
 
Kuelekea sikukuu ya wapendao 14/02/2020.

Hebu weka wazo la zawadi unayofikiri utanunua au kuandaa kwa ajili ya mpenzi/mpendwa wako ila bajeti isizidi Shilingi 20,000/=

Kwa kuweka limit ya kiwango hiki pengine itashawishi wengine wanaofikiri zawadi ni lazima iwe ya gharama kubwa.

Inaweza kuwa zawadi ya elfu 1,2,5,10 nk ilimradi isizidi kiwango tajwa hapo juu,lengo ni kuonyesha upendo na kujali bila kuangalia thamani ya zawadi.

N:B Mimi nafikiria kuandaa kuku wa kukaanga kwa kachumbari na Pepsi 1
(Nitaandaa mwenyewe Nyumbani)

Bajeti:

Kuku 1 wa kienyeji. 10,000
Pepsi take away. 1,000
Jumla. 12,000

Karibuni.


Sent using Jamii Forums mobile app
hebu cheki zawadi itakayodumu mwaka mzima na kila siku ataiangalia bei yake pia ni nzuri nayo ni kalenda
 
Mishumaa inayonukia na mafuta ya mwili.

Nitawasha mishumaa hio ghetto na hayo mafuta nitatumia kumpa massage.

Hio zawadi safi kwa bajeti yangu ya sh 20,000 na wote tutafurahi na kuikumbuka siku ya wapendanao.
 
Back
Top Bottom