Maisha Ni mapito Na mapitio Kuna mengi yanatokea ambayo hubaki kama kumbukumbu kwa muda mrefu vichwani mwetu. Mwaka unaelekea ukingoni.
Tusimulie jambo lolote ambalo hautalisahau lililokutokea iwe mafanikio au mateso kwenye mapenzi,kazi,biashara au mihangaiko mingine ya kimaisha.
[HASHTAG]#Binafsi[/HASHTAG] nimepitia mambo mengi lakini kubwa la mafanikio ni kuwa nimeweza kufungua biashara kadhaa ambazo bado ziko stable pia natarajia kupata mtoto mwakani januari. Lakini kwa upande wa matatizo mojawapo ambalo sitalishau ni kupelekwa polisi na kulazwa mahabusu kutokana na kupigana na trafiki baada ya kunibambikia kosa. Hayo ndiyo ambayo sitayasahau kwa mwaka huu......
Pia kwa humu Jamiiforum nimefanikiwa kuanzisha Uzi pendwa wa Kupeana Likes ambao umekuwa namba moja kwa kuzipiku nyuzi nyingi za zamani.
[HASHTAG]#Tueleze[/HASHTAG] na wewe kipi hutasahau...............!