Tusi sio neno au jina la sehemu ya mwili bali tabia ya sehemu ya mwili ndio tusi

Tusi sio neno au jina la sehemu ya mwili bali tabia ya sehemu ya mwili ndio tusi

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Mara nyingi katika jamii zetu kumekuwa na tabia ya watu kurushiana matusi la hasha tusio neno au jina la sehemu bali ni kutokana na tabia ya sehemu fulani kwa mfano;

1, Puru, tundu la kutolea haja kubwa ni moja ya tusi kubwa sana hasa kwa jamii za Arusha mjini na kwingineko!
Kwanini sehemu hiyo hutafsirika kama tusi ni kwakuwa sehemu hiyo kazi yake ni kutoa uchafu hivyo likitamkwa hujenga taswira ya ule uchafu unaotolewa na kwa bahati mbaya sikuhizi imepewa kazi nyingine kinyume na kazi iliyoumbiwa, jiulize tu hili swali neno mdomo, mkono au mguu kimaandishi lina tofauti gani na mkun...nd.

2, Uke, hii ni sehemu muhimu sana kwa mwanadam si ke wala me but imekuwa ikitumika kama tusi kwani imekuwa ikitumika vibaya sana na bht mbaya kwa jamii za nyuma kidogo kile kitendo cha kujamihiana kilitafsirika kama aibu kwa mwanamke but sikuhizi imekuwa sifa hivyo mtu akiitwa ku..... anaweza kupigana nusu kufa shida sio hilo neno shida ni hiyo kitu kwani neno au kiungo kama k inatofauti gani kimaandishi au kimatamshi na kongosho, kidari nk

NB
Maana ya kitu chochote ni hutokana na kitu unavyokitafsiri hivyo maneno sio matusi bali tusi ni jinsi unavyolifikiria lile neno kwa mazingira yako na dhana uliyo nayo juu ya kitu/sehemu hiyo .

Tutaendelea siku nyingine.
 
Last edited:
Shukran kwa elimu uliyotoa. Kwa maneno uliyotolea mfano ni kweli siyo matusi. Natofautiana na wewe kidogo uliposema “tusi siyo neno”, yapo matusi ambayo ni maneno au maneno ambayo ni matusi, hebu fanya uchunguzi!
 
Toa mfano mkuu
 
Tusi ni the way neno unaloambiwa unalitreat unaweza ambiwa hata wewe kichwa ukachukulia tusi
 
Mfano "pumbavu", ni neno lakini ni tusi ambalo ni tofauti maneno uliyotolea mfano kwenye uzi wako!

Kitafsida neno pumbavu sio tusi bali ni neno linalotumika kupunguza ukali wa neno mjinga yani asiyejua kitu fulani sasa mtu asiyejua kitu fulani linawezaje kuwa tusi mkuuu?
 
Kitafsida neno pumbavu sio tusi bali ni neno linalotumika kupunguza ukali wa neno mjinga yani asiyejua kitu fulani sasa mtu asiyejua kitu fulani linawezaje kuwa tusi mkuuu?
Katika KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU toleo la 1981, wameeleza maana ya neno "tusi" kama ni neno lolote chafu lenye kumuudhi mtu; tukano, kwahiyo hata neno "mpumbavu" ilhali litamuudhi anayeambiwa, basi litakuwa ni tusi!
 
Hivi hujaona mtu anaitwa we bishoo tu na anaudhika hata kupigana na kutupiana matusi kwani hapendi kuitwa bishoo kwani linamuudhi!
Kwa mantiki hiyo tunaweza sema neno bishoo ni tusi?
 
Hivi hujaona mtu anaitwa we bishoo tu na anaudhika hata kupigana na kutupiana matusi kwani hapendi kuitwa bishoo kwani linamuudhi!
Kwa mantiki hiyo tunaweza sema neno bishoo ni tusi?
Kwa yule ambaye linamuudhi, basi ni tusi kwake. Kumbuka, neno linaweza kuwa tusi kwako lakini kwa mwingine lisiwe tusi!
 
Wasomi wa fasihi husema DUNIANI HAKUNA MATUSI BALI NI VIUNGO VYA MWILI
 
Back
Top Bottom