SoC04 Tusichague viongozi (wabunge) kwa kigezo cha wao kuja kutatuta matatizo yetu. Tuchague viongozi waaminifu na wenye uzalendo juu ya taifa letu

SoC04 Tusichague viongozi (wabunge) kwa kigezo cha wao kuja kutatuta matatizo yetu. Tuchague viongozi waaminifu na wenye uzalendo juu ya taifa letu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kong xin cai

Member
Joined
Dec 12, 2020
Posts
76
Reaction score
87
TANZANIA TUITAKAYO
1.0 UTANGULIZI
Takribani miaka 63 imepita tangu Tanganyika kupata uhuru na miaka 60 ya muungano wa jamuhuri ya muungano wa tanzania. Chaguzi nyingi zimepita pamoja na marekebisho mbalimbali ya katiba yamekwisha fanyika ili kuleta uongozi bora na kuimarisha demokraia nchini. Ni awamu ya saba sasa ya uchaguzi unaotarijiwa kufanyika mwaka 2024/2025, huku juhudi za wanasiasa wakiamka kwa kasi ili waweze kurejea madarakani.

Wapo wale wanaokaa mjini A sasa ni wakati wao kurudi vijijini(majimboni) kupiga kampeni, si ajabu hata wale waliotuahidi kutujengea barabara na hawakufanya hivo wameanzia jitahada za kukarabati vinjia vyetu ili waweze kupita salama na magari yao ya kifahari wakati wa kampeni zao.

Huku wananchi wa hali ya chini, waliopewa dhamana ya kutembea na bendera za vyama, walioitwa wafia vyama, wanaotuhumiwa ukada wamejiandaa kuwapamba wale wale waliopotea msimu uliopita, ila sasa wamerudi na vizawadi vya vitisheti na kofia, akina mama zawadi za vitenge wakiawaambia nyimbo nzuri za ushindi pasipo kufikiria ni miaka 63 sasa tangu tupate uhuru na ado kuna vijiji havina maji, zahanati, na barabara.

Ndugu watanzania, hakuna kiongozi(mbunge) atakaekuja kujenga nchi hii kwa hera yake mwenyewe, taifa hili linajengwa na kodi zetu wenyewe, sio zawadi kwa sababu ya kumchagua kiongozi furani, sio ahadi alizotoa wakati wa kampeni, bali kodi zetu na ndizo zinazotumika hata kwenye kulipa mishahara yao.

Nimetoka kwenye kijiji ambacho toka nikiwa mdogo, mbunge aliahidi kuwa tukimchagua atajenga Barbara, zimepita takribani awamu nne bado shida ni ileile, na wananchi wanaendelea kuwachagua viongozi kwa kigezo kile kile cha kwamba wakimchagua ataleta barabara, sasa sijui hio barabara inatoka china au urusi mimi sifahamu.

Viongozi hawatatui changamoto zetu ili waendelee kutumia zilezile wakati wa kampeni, wapo wanaochelewesha miradi maendeleo kwa makusudi na kuindeleza mara uchaguzi unapokaibia, nini kipi tunachozingatia tunapowachagua viongozi wetu, mavazi wanaotupa, fedha, au zile nyimbo zinatufanya tuamini wao ni kama sisi, kumbe kiuhaisia wao naendelea kuwa wao na familia zao.

Wakati huu tunapoelekea kwenye kampeni za uchaguzi kila mmoja(kiongozi) atajionesha kuwa yeye ndio serikali, kuwa ataweza kutufany chochote tukimchagua, lakini si ajabu wakati huu kila mmoja si wananchi, na viongozi(wabunge) wanalia na serikali, lakini serikali haikuja kuomba kura kwako, alikuja kiongozi, akaletea jezi, mkacheza mnavyojua wenyewe, lakini ushindi mkampa yeye, leo hii huyo huyo anaiomba serikali ipeleke maji jimboni.

Ni wakati sasa sisi (Watanzania) tunapoelekea kwenye uchaguzi wa awamu ya saba 2024/2025, tukachague viongozi watakaobeba dhamana, waaminifu na wazarendo na taifa letu. Lakini sisi kwasababu ya ushawishi wao au vyama vyao.

TANZANIA TUITAKAYO ipo mikononi mwa viongozi tutakaowachagua,tukichagua viongozi bora ndivyo tutaifikia tanzania tuitakayo lakini kama tukiendelea kurubiniwa na wanasiasa bado TANZANIA TUITAKAYO itakuwa ya miaka ya 2000s na si ile ile ijayo.

TANZANIA TUITAKAYO inahitaji viongozi shupavu, uzalendo na demokrasia shirikishi kwa kuwa maendeleo ya taifa ni uongozi.

2.0 USHAURI KWA SERIKALI:
Tunapoelekea kwenye TANZANIA TUTAKAYO ni vema kwenda na viongozi wenye utayari wa kulitumikia taifa letu. Wale watakaobanikia kuhujumu uchumi, kuchelewesha miradi ya serikali ama kushutumiwa kwa makossa ya jinai ni vema kuachanao moja kwa moja na si kuwahamisha vituo vya kazi, wapo watanzania wenye uwezo wa kiuongozi kwa hivyo si vema kuendelea kung’ang’ana na mtu mmoja.

Hii itasaidia kuleta nidhamu ya kazi, na hali ya kujituma kwa viongozi.
 
Upvote 1
Kichwa cha somo chajieleza.

Nakubaliana na wewe kwamba sisi kama nchi tupo tayari katika safari ya kujiletea maendeleo kupitia kodi zetu. Hivyo ni kweli kabisa tunachotaka ni viongozi watakaoendana na dira hiyo. Wasitupinge wala kutupoteza kwenye reli. WAZALENDO

Shukrani kwa kutukumbusha jambo la msingi ambalo hata Mwalimu Nyerere alitufundisha. Maendeleo yetu tunajiletea wenyewe - KUJITEGEMEA. Late JPM alikazia hayohayo.

Mwanasiasa yeyote atakayeleta 'swagga' za kutuletea hiki mara kile huyo anaturudisha nyuma. Inatia moyo kuona watu wameinuka kifikra
 
Back
Top Bottom