Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Mvua imekuwa habari kuu maeneo mengi na watu wengi wanadhani jukumu la kuiombea inyeshe ni la waumini wa makanisani na misikitini. Wengine hudhani jukumu la kuomba mvua ni la wazee wa mila kumbe sivyo.
Jukumu la kuomba mvua inyeshe ni la binadamu wote. Lakini maombi yoyote yale yanaambatana na toba, hili ni lazima kila mmoja wetu alifahamu. Toba ni kujutia kwa ovu ulilolifanya na kujiepusha nalo usilirudie tena.
Ovu lolote unalofanya maana yake unakuwa kuna haki uliyonyang'anya na kuimissplace pahala hivyo toba yako lazima iambatane na kuirudisha haki hiyo sehemu ilipohitajika kuwepo. Kama haki ni ya Mungu irudishwe kwa Mungu na kama ni mwanadamu basi arudishiwe huyo mwanadamu.
Twende kwa mifano:
Kama hamsemezani basi ni muda wa kupeana salamu muanze kusemezana, una kinyongo na mtu basi kunjua moyo na msameheane, magomvi yote sitisha muishi kwa amani. Ulidhulumu mtu basi rejesha mali za watu ulizowadhulumu, ulikuwa huswali basi rudisha haki ya mungu kwa kuanza kuswali.
Kuomba mvua inyeshe siyo kusema tu maneno ya kuomba mvua bali kuambatane na matendo mazuri mazuri mfano kufunga, kutoa sadaka na mengine. Hayo ndiyo kwa ufupi tunatakiwa kufuata katika kuomba mvua zinyeshe katika miji yetu tofauti na hapo si kwamba mvua hazitanyesha bali zitakuwa ni mvua zisizo na manufaa sana kwetu!
Asanteni