SoC03 Tusichoke kupanda miti

SoC03 Tusichoke kupanda miti

Stories of Change - 2023 Competition

John Kwambaza

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
6
Reaction score
4
Nakumbuka namna ambavyo kampeni ya upandaji miti ilivyokuwa na mwitikio mkubwa miaka ya nyuma kidogo hasa mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Kampeni Ile ni Kama ilizimika au imepungua Sana Ile nguvu yake, msingi wa hoja ya kuishadidia kampeni hii ni uhalisia wa hali ya ukigeugeu usiotabirika wa hali ya hewa(mabadiliko ya tabia nchi).

Kwa Sasa hali ya ukataji miti ni WA kiwango Cha juu Sana na ukifanya ulinganifu na kiwango Cha upandaji miti kwa kweli huko mbele hali yetu itakuwa ngumu Sana.

Ukatwaji wa miti unasababishwa na mambo mengi na kwakweli kati ya hayo mengi ni yasiyoepukika.Haya ni Yale yanayokwenda sambamba na njia za utafutaji na kujikimu kimaisha na pia ongezeko la makazi ya watu; haya ni baadhi ya mambo ambayo hayaepukiki kirahisi.

Nakiri pia kwamba zipi namna nyingine ambazo zitokana na hali yetu ya tamaa na kutaka kujitajirisha kimagengo na wizi kwa njia ya kukatwa miti na kuuza mbao na mazao ya miti.

Nafahamu kwamba zipi njia mbadala za kuishi bila kutegemea misitu lakini kwa maoni yangu naona bado tuna safari ndefu katika kufikia kuishi kwa kutumia njia hizo.

Uhitaji wa Kuni na mkaa kwa aijli ya kupikia bado Nia suala mtambuka Sana;uhitaji wa miti na mbao kwa ajili ya ujenzi bado ni jambo ambalo litaendelea kuathiri mustakabali wa misitu.

Pamoja na hayo lakini pia tunashuhudia uanzishwaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo Kama vile Mabwawa ya kufua umeme na mashamba makubwa haya yote yanafanyika kwa gharama za ukatwaji wa miti.

Huko vijijini kunaanzishwa mashamba mapya Kila siku na upanuaji wa makazi ya watu. Kwa msingi huu napendekeza kwamba sisi Kama jamii ya watanzania na kwa ajili ya kuitunza nchi yetu tuwekeze zaidi katika upandaji wa miti hasa sisi tuishio maeneo ya pembezoni mwa miji.

Serikali ifanye kwa namna yake lakini sisi mimi na wewe,wanawake kwa wanaume wote Kila mmoja na afanye kwa uwezo wake na juhudi zake.

Nilishawahi kufanya zoezi la kupanda miti miaka ya nyuma wakati nikiwa mwalimu maeneo ya vijijini kidogo.Na ndani ya miaka mitano au sita tulistawisha miti zaidi ya elfu tatu katika shule mbili nilizopata kuwa mwalimu.

Njia tuliyotumia haikuwa na gharama kubwa zaidi ya muda na nguvu kidogo.Mathalani eneo Fulani tulipanda miti aina ya mikomba na sedrella.

Aina hizi za miti Huwa Zinatoa mbegu nyingi kwa hiyo sisi tulikwenda na wanafunzi maeneo yaliyo na miti hiyo na tukakusanya mbegu halafu tukaenda kutengeneza vitalu na baadae zilipoota tukazihamisha kwenye maeneo tuliyokwisha kuyaanda.

Hii yaweza kuwa njia moja lakini tukiweka Nia twaweza kubuni na kutekeleza njia kadhaa rahisi TU na tukaleta mabadiliko.

Miti aina ya misedrella na mikomba kitabia hukomaa kwa muda mfupi na Leo hii ni mbao zinazouzwa kwa bei nzuri na uhitaji wake ni mkubwa. Njia hii yaweza kutumika na kutengeneza misitu ya mitiki(misaji)miti ya matunda Kama miembe, mifenesi, milimao na kadhalika.

Kwa hiyo kampeni hii zaidi TU ya kuitunza mazingira yetu lakini pia ni mradi mzuri wa kuweza kutupatia kipato. It can be done play your part.

Ahsanteni.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom