Uchaguzi 2020 Tusidanganyane: Kwa mtindo huu sioni hata Mkurugenzi mmoja atayeweza kutangaza ushindi kwa upinzani abadani


"Nimekuchagua, nimekupa madaraka, nakulipa mishahara, nimekupa gari nzuri, nimekupa nyumba nzuri, nk. halafu umtangaze mpinzani kuwa ameshinda uchaguzi Mkuu utanitambua." Amesikika akisema bwana yule.
 
Ni kweli lazima kusitisha uchaguzi mpaka kieleweke na pia shinikizo la kujiuzulu kwa magu ni muhimu, anaharibu nchi yetu vibaya kabisa.
 
Yamejirudia. Ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Hakuna uchaguzi hapa; bali ni uchafuzi tu.
 
Mahakama nayo ni CCM. Wapinzani hawana pa kutokea. Wanapigwa kila kona. Wakubali kufa au kupigania uhai.
 
Wao kazi yao kuimba ni yeyeeee ni yeyeee badala ya kufanya mambo ya msingi kama haya.
 
Hii kauli mmeisahau? "Nikuteuwe mimi kuwa Mkurugenzi, nikupe gari, nikupe nyumba, nikupe mshahara na posho halafu umtangaze mpinzani mshindi!!".

Hii kauli ilithibitisha kuwa CCM imefanikiwa kufikia kiwango cha juu cha ujeuri kiasi cha kutohitaji tena ridhaa ya wananchi kubaki madarakani. Na inawezekana Watanzania wengi kufikiri kuwa hili ni tatizo la “wapinzani” - wao hawahusiki. Na hapa ndipo lilipo janga la taifa letu “national tragedy”. watu kufikiri kinachoendelea kwenye siasa ni matatizo ya Magufuli vs Lissu & Kabwe, Gwajima vs Mdee, Tulia vs Sugu, n.k.

Watanzania wangefahamu kuwa nchi kama Equatorial Guinea, Central African Republic na Congo DR zilipitia hatua hizi hizi kufikia majanga ya kitaifa yanayozitesa hadi leo, wasingepuuza (ignore) na kujivua wajibu wa kusimamia viongozi wa kisiasa kiasi cha kuwapa jeuri ya aina hii. Labda siku maumivu yakikolea kwa wengi, ndipo unafiki utawekwa pembeni.
 
Tatizo la Chadema ni SACOS ya Mbowe na familia yake, lini wanaweza kutengeneza mbinu za kuongoza wakati wamekaa kushibisha matumbo yao? Hizi kampeni ndio zinawavua nguo sasa.
 
Resistance ya hali ya juu inatakiwa kuanzia sasa kabla hata ya kampeni kuanza.
Hiyo resistance kumweka madarakani Chadema? You must be dreaming, CCM hata kama wana matatizo sio sababu ya kuwaweka CHADEMA. Matatizo yako wewe binafsi na kujiangalia wewe mwenyewe na familia yako ndio yanakusukuma na hoja potofu.

Leo hii hata ukiambiwa mnapewa nchi mna sera gani nyie ya kuinua maisha ya Mtanzania? FYI Watanzania sio wajinga hizo sarakasi mnazozipiga kia mwaka zinafahamika.
 

Sidhani kama hata wewe unaifahamu sera ya CCM ya “kuinua maisha ya wananchi”. Kama sivyo, itaje.
 
Umeandika kwa hisia Kali sana. Nimekuelewa sana mkuu!
 
Waache watu wafanye wanachokiamini. Usiwapangie ili mradi hawavunji sheria za nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…