Uchaguzi 2020 Tusidanganyane! Tundu Lissu ndie mpinzani pekee anaeweza kumpa ushindani Rais Magufuli kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oct 2020

Kwa hiyo ulitaka Chadema wafanye kama CCM yaani ingechapishwa form moja tu ya Tundu Lissu?
 
Lema ameshakataa nenda kamuombe abadirishe msimamo. Lakini kwa taarifa yako Rais Magufuli hana wakushindana naye!!
Pasipo na tume huru hana wa kushindana nae ila penye tume huru anaondoka mapema sana.
 
Huyo Hana hoja ya kupambana na Magufuli labda Kama ameisha inunua CHADEMA Ili imupitishe
Ulishawahi kumsikia huyo kuongozi wako akitoa hoja, unaishi nchi gani kwa sasa. Nchi yetu ilishapoteza vichwa vyenye hoja for a long time.
 
Tundu Lisu Aongelee kupambana na wagombea akina Mbowe, Nyalandu nk ndani ya Chadema Kama atawashinda Magufuli sio saizi yake .Saizi yake hao wagombea wenzie ndani ya Chadema waliotia Nia Kugombea kuteuliwa ugombea uraisi ndani ya Chadema

Huwezi rukia chuo kikuu wakati mtihani hata wa shule ya msingi hujafanya na kufaulu

Ahangaike kufaulu mtihani huo alionao chadema Kwanza wa kugombania uteuzi
 
Lisu hawezi kuwa rais kama antegemea kura za wananchi, lazima awe na chombo X cha kumpa support.
 
Bavicha hawajui wamchague nani kati ya lissu na mbowe
Lissu atakwama tu,ataambiwa aje achukue mwenyewe fomu ufipa na yeye anaogopa
Haya sasa
Lisu kashachukua form, sijui aibu yako unaiweka wapi
 
Watumishi wa umma miaka 5 bila nyongenza. Mtu anachukua form ya kugombea; bila kuwa na huruma.
 
Mkuu, tunawnda na Membe. Jasusi mbobezi.
 
Ccm watahakikisha akirudi tu wanamweka ndani, demokrasia imeondolewa nchini tusikubali uozo huu watanzania.
Aliondoka akiwa na kesi mahalamani, kesi iko palepale! Na kaonekana anazurura zuruta huko, anaidharau mahakama! Akitua tu ni kukamatwa.
 
Chadema mmechanganyikiwa.
hamjui mpaka sasa mshike lipi.alafu vitu vidogo vinawashinda ndo mnataka nchi!!.
 
Aliondoka akiwa na kesi mahalamani, kesi iko palepale! Na kaonekana anazurura zuruta huko, anaidharau mahakama! Akitua tu ni kukamatwa.
Wewe huna tofauti na huyo shetani kwenye avatar yako.
 
Kuwazuia watu wengine wasichukue fomu ni udikteta kama Tundu Lissu lazima apimwe kwa hoja na wenzake badala ya kumpitisha kwa mchakato wa kidemokrasia.

Tunapigania demokrasia ila hatutaki kuifanya hiyo demokrasia ndani ya vyama vyetu this is not right.
 
Chama lazima kipate viongozi wa kitaifa kupitia mchakato wa kidemokrasia haya mambo ya kuchagua viongozi kwa kivuli cha busara siyo sahihi.

Tutajitofautisha vipi na ccm ambao wanaprint form moja tu? Tuache watia nia tuwapime kwa hoja zao na uwezo wao wa kiuongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…