Tusidanganyike na Jinsia, Dini, Kabila, Rangi, Sura ya Rais Ubaya hauna kwao. Tuzingatie katika Chaguzi zetu

Tusidanganyike na Jinsia, Dini, Kabila, Rangi, Sura ya Rais Ubaya hauna kwao. Tuzingatie katika Chaguzi zetu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Siku zote nimekuwa nikisema.... UBAYA HAUNA KWAO. msije mkadhani Rais kwa kuwa ana Jina zuri la Kikristo au Kiislamu basi atakuwa mwema. Sababu linatoka kwenye Biblia au Quran.

Msije mkaangalia Rangi ya Rais mkamchagua kutokana na rangi yake mkiamini atakuwa mtu mwema sababu ni mweupe au ni mweusi. Huu ni ukichaaa.

Kuna kipindi watanzania wanakwambia huyu ndo anafaa hata sura yake inapendeza kwenye picha,ana tabasamu, ana rangi.

Mkiangalia Jinsia mkasema huyu sababu ni mwanamke au mwanaume atakuwa na roho njema mnajidanganya. Ubaya hauna kwao. Ni roho ya mtu na akili yake.

Sasa hivi watu tunagawanyika kutokana na Dini na Jinsia. Kuwa huyu ni mwenzetu tumsifu na kumwabudu. Kama ambavyo pia tuligawanyika before kwa vigezo hivyo hivyo. Ndo maana mambo hayabadiliki.

Yatabadilika majina ya Marais, Dini, Rangi, Kabila na Jinsia. Ila ufisadi, ukatili, unyama na uonevu utabaki.
 
Inamaana unampinga Mtemi Hangaya aliyesema wanawake wako wengi siyo?
 
Ubaguzi dhahiri wa Mwendakuzimu dhidi ya Waislamu ambao alikuwa anauficha kwa kuchangisha fedha ya kujenga ka msikiti Dodoma tuufumbie macho?
 
Back
Top Bottom