Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,207
Wasalaam Wakuu.
Katika dunia ya sasa, ngono imekuwa ni kibwagizo katika maisha ya binadamu.
Iwe jinsia ke au me, wote wanapenda kufanya ngono kuliko inavyostahili.
Kufanya mapenzi ni tendo takatifu kwa ajili ya kufanya uumbaji. Yaani kwa ajili ya kuendeleza kizazi. Lakini binadamu wameigeuza kama Starehe.
Tukitazama kwa Wanyama wengine wafugwao na wa mwituni, hufanya mapenzi kwa nia pekee ya kurutubisha na kutungisha mimba. Ikishatimia hawafanyi tena mpaka pale watakapokuwa tayari kupata uzao mwingine.
Kutokana na binadamu kuendekeza ngono kama Starehe, imeleta athari kubwa sana katika uso wa dunia.
Hata jinsia fanano zimeanza kuingiliana kwa sababu ya kupenda starehe. Wanaume kwa wanaume wanageuzana kwa nia tu ya kugundua raha katika kufanya hivyo. Vivyo hivyo kwa wanawake. Kama tungelitumia kwa minajili ya kuendeleza kizazi basi mapenzi ya jinsia moja kamwe yasingelikuwepo abadani.
Kuendekeza ngono kumeleta magonjwa mengi sana katika uso wa dunia. UKIMWI, homa ya ini, kaswende na magonjwa mengi ya kuambukiza ni matokeo ya Starehe ya ngono. Kama ngono isingelidekezwa basi kusingelikuwepo na idadi kubwa ya magonjwa ya zinaa.
Kuendekeza ngono kumeondoa uaminifu, urafiki na undugu. Kama mmoja wa wanandoa ameendekeza ngono na mwenzake kutambua basi mfarakano hutokea baina yao. Uaminifu uliokuwepo hupotea. Undugu huvunjika. Urafiki hufifia. Yote haya ni kwa sababu wahusika wameendekeza Starehe ya ngono.
Kuendekeza ngono kumezalisha sana watoto wa mitaani. Hamu ziliwazidi, wakakutana kutimiziana. Mimba ikafungwa. Hawakujiandaa kumpokea mgeni. Kitakachotokea ni mtoto kukimbiwa na kuanza maisha yake mwenyewe.
Kuendekeza ngono kumepelekea vifo, ulemavu na umaskini. Watu wengi wamejinyonga kwa sababu kushindwa kuhimili ukweli wa walichotendewa. Wengine wamebaka na kuuwa kwa sababu ya mafumanizi. Ngono hugharimu pesa na muda ambao ungetumika kwa ajili ya uzalishaji mali na hivyo umaskini.
Ngono ni kiini cha maovu yote katika uso wa dunia. Tukae mbali nayo.
Kuna jamii moja ambayo, hufanya mapenzi pale tu ambapo wana nia ya kupata mtoto. Pale ambapo baba na mama wataona kwamba mtoto sasa ameshakua, basi mama ataambiwa aache kunyonyesha mtoto. Watafanya kwa wakati kisha mwanamke akishabeba ujauzito, wanahairisha mpaka pale ambapo watakuwa tayari tena kutafuta mtoto mwingine.
Hata wanandoa, msiendekeze sana tendo la ndoa. Lifanyike kwa kiasi.