Tusiingize udini, suala la bandari ni urithi wa Watanzania

Tusiingize udini, suala la bandari ni urithi wa Watanzania

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
TUSIINGIZE UDINI, SUALA LA BANDARI NI URITHI WA WATANZANIA

Watu wanakuja na hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo hizi ni hoja binafsi na sisi Watanzania hatuna hizi kasumba za udini wala ukabila, ni vijihoja vinavyotaka kututoa kwenye reli tuache kudai mkataba wenye tija kwa Watanzania, hizi hoja zenu za udini tunazikemea, ni hoja binafsi sio za Watanzania na hazina mashiko katika suala la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, pelekeni hoja zenu za udini kwenye mabaraza ya dini mkakubaliane na Serikali,kwa sasa tupo kwenye suala la bandari, tunataka mkataba wenye tija kwa Watanzania, sio mkataba wa kuwauza Watanzania kama ule wa Chifu Mangungo wa Msovelo.

Kuna watu wanataka kuhalalisha kosa kwa kosa, hili nalo hapana, kama mikataba ya nyuma haijapita bungeni na huu Mungu katujalia umepita bungeni, na Watanzania tumeuona sijui umevuja au umeachiwa watu wausome na tumegundua makosa makubwa ya kutweza utu wa Mtanzania, ndio tuuachie uendelee hivyo hivyo kwa kuwa mikataba mingine uko nyuma haikupita bungeni, hili si sahihi, tulichokigundua kibovu lazima kirekebishwe na kiwekwe kwa maslahi mapana ya Watanzania.

#Maslahi ya Mtanzania kwanza.
 
Mbona kidanari pengo ndo wa kwanza kupinga na kueneza upinzani kanisani wapinge mkataba wakati kipindi cha Jpm hakuonyesha huo uzalendo, kipindi Jpm anaua na kufunga raia wanao mpinga
 
Back
Top Bottom