musicarlito
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 368
- 556
MTAKATIFU VALENTINO, PADRI NA ASILI YA SIKU YA WAPENDANAO ( VALENTINE DAY )
Siku ya Valentine Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi.
Ni siku ya kumkumbuka Padre Valentino aliyeuawa na utawala wa Kirumi.
Mt. Valentini alizaliwa mwaka 226 AD huko Terni, Nchini Italia na aliuawa Februari 14, 269 AD huko Roma, Italia.
Aliuawa kwa sababu ya kutetea Waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu.
Lakini sikukuu hiyo imeenea sana nchi za Magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya Ulimwengu huisherehekea kama siku ya Mapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.
Vijana hawakutakiwa kuoa ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi.
Hii ilimaanisha kuwa kama wangeoa wasingekuwa na uhuru wa kwenda Vitani bali kuwa na familia zao.
Padre Valentino ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele za macho ya MUNGU.
Akawa anafungisha ndoa kwa siri kubwa kwenye Makatakombe yaani Mahandaki chini ya Kanisa ambako kuna sehemu za Ibada kwa watu wachache na alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka Amri ya Wakuu wa Dola.
Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentino alishikwa na uongozi wa Dola ya Warumi na kuuawa kama Shahidi Mfiadini.
Kanisa Takatifu Katoliki Ulimwenguni kote likatenga tarehe 14 FEB maalum ya kumkumbuka Mt. Valentino kama mfiadini sababu ya kutetea maisha ya Wanakanisa kuwa wanandoa.
Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya Kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentino kama mtetezi wa Ndoa.
Maudhui ya siku hiyo kwa wasio Wanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa ilimradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya Mfia Dini Mt. Valentino aliyetaka vijana wafunge Ndoa.
Wenye hofu ya MUNGU tunaalikwa kuiheshimu Siku hii kama ni Siku Takatifu ya kumpendeza MUNGU kwa watu tuwapendao na sio kuifanya kama siku ya kutenda machukizo mbele ya MUNGU.
Tumuombe Mt. Valentino, atuombee kwa MUNGU tuwe na upendo wa kweli kwa watu tuwapendao ili hatimaye tutimize mapenzi ya MUNGU wetu.