Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Vyombo vya dola, ni taasisi muhimu sana katika nchi. Mkikosea kwenye vyombo vya dola, basi mmetengeneza mateso na maangamizi kwa watu wengi, tena wasio na hatia.
Tanzania, kama kuna chombo cha dola ambacho angalao kina uweledi, ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hata kama linaweza kuwa na mapungufu yake, lakini yatakuwa ni madogo sana.
Jeshi letu la Polisi, tukiacha unafiki, tena kwa ushahidi ulio wazi, ndiyo taasisi ya hovyo, kuliko taasisi yoyote iliyo chini ya Serikali:
1) Jeshi la Polisi ndiyo linaongoza kwa rushwa nchini. Hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali rasmi, ikiwemo TAKUKURU. Unapokuwa na taasisi inayoongoza kwa rushwa, basi ni lazima taasisi hiyo itakuwa imeoza, na inaweza kutumika vibaya na kila mwenye uwezo wa kuhonga. Tujiulize, ni watu wangapi wameteswa na kuangamizwa na jeshi la Polisi bila ya kuwa na hatia. Rais Samia aliwahi kutamka kwa kauli yake kuwa malalamiko ni mengi dhidi ya jeshi la Polisi, kuanzia watu kuuawa kwenye mahabusu za polisi, mpaka barabarani. Cha ajabu, Rais aliishia tu kulalamika, badala ya kuchukua hatua madhubuti.
2) Kuna wakati Jeshi letu la Polisi linafanya kazi kama genge la maharamia. Kuna watuhumiwa, na wengine bila shaka ni watuhumiwa wa kutengenezwa, wamewahi kuuawa na polisi. Mifano ni mingi, na mingine ilithibitishwa mpaka na mahakama. Nadhani mnakumbuka wale wafanyabiashara wa madini waliotoka Morogoro walioporwa pesa zao kisha kwenda kuuawa msituni. Sasa hawa ni Polisi au majambazi?
3) Jeshi la Polisi, badala ya kuwa mfano wa kutii sheria ndilo linaloongoza kwa kudharau katiba, sheria na kanuni zinazoongoza utendaji kazi wa jeshi la Polisi. Polisi wa Tanzania, hakuna wanachojua, zaidi ya kupiga, kuchukua rushwa, kubambikia watu kesi, na maovu mengine mengi . Yaani wahuni na majambazi wamejazwa ndani ya taasisi muhimu huku wakiitumia taasisi hii kufanya unyama na ushetani wao.
4) Jeshi la Polisi ndiyo linalotajwa kuwateka, kuwaua na kuwapoteza raia wema, bila shaka ni wale ambao wapo mstari wa mbele kuukosoa uovu wao.
5) Jeshi la Polisi ili kuwapumbaza watawala, kila mara linafanya ushetani dhidi ya raia alimradi likiamini kuwa kwa kupitia ushetani huo, watawala watafurahi, na hivyo kuufumbia macho uovu wao. Na kila mara wanaamini kuwa CCM na viongozi wake wanaweza kuuachia uovu wowote ule alimradi kama uovu huo wanaamini unawagandamiza wakosoaji wa Serikali na viongozi wake, na hasa chama cha CHADEMA ambacho wanakiona kama ndiyo mwanga wa Watanzania katika kutambua haki zao. Kuna syndicate imeundwa baina ya polisi waovu, viongozi waovu wa CCM na watawala waovu. Ndiyo maana haishangazi kuona kuwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakifanyiwa uharamia na ushetani wa ajabu kila mara, huku CCM, viongozi wa CCM na viongozi wa Serikali wakishangilia na kufurahia. Fikiria tukio la juzi ambapo uharamia wa hali ya juu umetendwa na Polisi dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA, halafu katibu Mkuu wa CCM, anawaamuru Polisi kuwa iwaachie, na Polisi wanatii. Huwezi kumtii ambaye siyo mkuu wako. Hii imedhihirisha kuwa Polisi, kwa sasa ni sehemu ya taasisi haramia zilizo chini ya CCM, sawa na ilivyo greenguards, ambao wanaweza kuamriwa na kiongozi yeyote wa CCM. Amri ya Katibu Mkuu wa CCM, inadhihirisha kuwa ni yeye aliyewatuma Polisi, na baadaye akawaambia kuwa imetosha, waachieni.
Wananchi kama tunataka ustawi wa nchi yetu, nchi itakayotoa nafasi sawa za kiusalama kwa kila raia, ni lazima tutambue kuwa kwa sasa hatuna POLISI katika ile maana halisi na ya kweli ya POLICE. Tuililie nchi yetu kwa mwelekeo unatoa taswira ya wazi kabisa kuwa nchi haipo salama. hakuna jambo baya na la hatari, unapokuwa na maharamia ambao wamepewa mamlaka ya kidola, halafu wakatumia mamlaka hayo kutekeleza uharamia wao. Ukiwa na vyombo vya dola vilivyo safi, halafu nje ya vyombo hivyo kukawa na maharamia, ni rahisi maharamia hao kudhibitiwa na vyombo vya dola. Bahati mbaya kwa upande wa nchi yetu, maharamia wapo ndani ya vyombo vya dola, watu wema wapo nje ya vyombo vya dola, je tutwadhibiti vipi hawa maharamia walio ndani ya vyombo vya dola?
Tusifurahie kusikia eti viongozi na wanachama wa CHADEMA waliokamatwa kwa uonevu, sasa wameachiwa, bali twende mbali zaidi kuwataka maharamia wote waliohusika na ukamataji ule, utesaji na wizi wa mali za waliokamatwa, wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Tuupime uadilifu na ubora wa uongozi wa Rais Samia katika hili.
Kwa Polisi hawa tulio nao, hakuna aliye salama, labda wale tu wanaowatumia katika kutekeleza uovu.
Wananchi ni lazima tupiganie kuipata katiba mpya ambayo:
1) Itaondoa vipingamizi vyote vya kumshtaki Polisi mwovu. Na pia ile sheria ya kutomshtaki Rais, Makamu, Spika na Jaji Mkuu, zifutwe. Na Ile sheria inayotaka eti ukitaka kuishtaki Serikali au afisa wa serikali kuwa lazima umwunganishe Mwanasheria Mkuu, na ili umshtaki mwanasheria mkuu wa serikali ni lazima upate kibali cha Serikali, ni sheria ya kijinga kabisa, isiyo na mantiki. Yaani eti uombe kibali kutoka kwa unayemshtaki kuwa umshtaki, na yeye aridhie!! Hiyo inaingia akilini?