Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Serikali imeendelea kusisitiza kwamba hadi sasa hakuna kinga wala tiba ya ugonjwa wa Ukimwi.
Katika kusisitiza msimamo huo, imewaonya waganga wa kienyeji waliobandika mabango sehemu mbalimbali za nchi na watu wengine wanaojitangaza kuwa wanatibu ugonjwa wa Ukimwi.
Msimamo huo ulitolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paniel Lyimo, katika mkutano ulioandaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) jijini Dar es Salaam na kuwajumuisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya dini, taasisi binafsi na watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU).
Lyimo alisema kuwa dawa ikipatikana itatangazwa na serikali na kwamba wanaojitangaza kutibu Ukimwi wanakiuka sheria za nchi na kwamba wanastahili kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Pamoja na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kwamba dawa ya Ukimwi haijapatikana, bado kuna vikundi vya watu hususani waganga wa jadi ambao wameendelea kuwarubuni watu kwa kutumia matangazo katika vyombo vya habari na kutumia mabango kuwa wanatibu Ukimwi.
Hata tafiti ambazo zimeshafanyika zinabainisha kwamba hadi sasa hakuna tiba wala kinga ya Ukimwi, isipokuwa dawa zilizopo na zinazoendelea kutumiwa na waathirika sio za kutibu bali ni za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Katika mazingira hayo ni wazi kwamba wale wanaojitangaza kwamba wanatibu Ukimwi wanawadanganya watu kwa tamaa ya kujipatia fedha bila kutokwa na jasho
Pengine kutokana na kukata tamaa ndiyo maana baadhi ya waathirika wamekuwa wakirubuniwa na kukubali kutoa fedha kwa watu hao ili wawapatie dawa ambazo hata hivyo hazina uwezo wa kutibu ugonjwa huo.
Kwa bahati mbaya sana miongoni mwa waathirika wanaolazimika kununua dawa kutoka kwa watu hao ni wale ambao hawana uwezo kiuchumi. Kutokana na kutojua kuwa wanadanganywa, wanajikuta wakipoteza fedha ambazo wangezitumia kupata mahitaji muhimu kama lishe.
Hata hivyo, serikali pamoja na kutoa tahadhari hiyo, haipaswi kuwalalamikia waganga wa jadi wanaowatapeli wananchi kwamba wanatibu Ukimwi. Inachopaswa kufanya ni kuwachukulia hatua wahusika kwa kuwapa onya na watakaokaidi kuwafutia leseni za biashara kwa kuwa wanafanya vitendo hivyo kwa makusudi.
Mamlaka za serikali ikiwamo Tacaids zinapaswa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa umma kuhusiana na dawa na chanjo ya Ukimwi kwa kuwaeleza wananchi wazi kwamba hadi sasa hakuna dawa wala tiba isipokuwa kuna dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Hatua hiyo itawasaidia kuelewa ukweli na kuacha kuhangaika kutafuta tiba kwa watu ambao hawana uwezo wa kutibu ugonjwa huo.
Tukio la maelfu ya watu kukimbilia kwa babu wa Loliondo kusaka dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ukiwamo Ukimwi halinabudi kuwa fundisho kwa jamii yetu.
Pamoja na kwamba baadaye imebainika kuwa kikombea cha Babu hakikuwa tiba mbadala ya magonjwa kadhaa, lakini wananchi wengi walikimbilia huko wakiamini watapata tiba kutokana na serikali kuwahakikishia kuwa kuna tiba halisi.
Lazima tukubali ukweli kwamba kinga na tiba ya ukimwi haijapatikana. Tunakubaliana na kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), Vitalisi Makayula, aliyoitoa katika mkutano huo kuwa tatizo la dawa feki za Ukimwi ni njama ya watu wanaotaka kujipatia fedha, lakini kisayansi dawa ya kutibu Ukimwi haijapatikana.
Tunashauri kwamba wananchi wafuatilie na kuheshimu taarifa za tafiti mbalimbali kuhusu Ukimwi pamoja na taarifa zinazotolewa na Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) ambalo kimsingi, ndicho chombo chenye mamlaka ya kuthibitisha dawa.
Aidha, wananchi wanapaswa kujilinda dhidi ya mambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujiepusha na ngono isiyo salama.
Tunasisitiza kwamba lazima tuambiane ukweli kwamba tusijidanganye kwa kuwa hadi sasa hakuna kinga wala dawa ya kutibu Ukimwi.
SOURCE: NIPASHE