X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
tusicho kijua ni kuwa Marais wengi sio Binaadam na sio Watu pia, ili uwe Binaadam ni lazima uwe na sifa za kibinaadam na ili uwe Mtu ni lazima uwe na sifa njema za Kiutu. ndio maana wagombea wa Urais ambao ni Watu na Binaadam watagombea Urais hadi kifo kinawachukua awafanikiwi ng'oo kukikalia kiti cha Urais. Ambae sio binaadam na wala sio mtu yupo zake tu amekaa kijijini kwao huko cheo cha Urais kinamfata huko huko.
wengi tunategemea Rais afanye chochote ili kuturahisishia maisha yawe mepesi, ndugu zangu mtu yoyote hapa duniani ambae sio Mtu hutafuta nafasi yoyote kwa maslahi yake yeye mwenyewe, Rais amepambania ndoto zake hadi akawa Rais leo aje apambane ili wewe uwe na maisha mazuri kweli hiyo si ni ndoto...? {jukumu la kutengeneza maisha mazuri umelibeba wewe mwenyewe hakuna mtu anaweza kukutengenezea maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe}
madalaka huwa yanalevya na huo ndio ukweli wenyewe, kadri mtu anavyo zidi kupanda cheo ndivyo hali ya kuwa na tamaa ya mambo makubwa zaidi inavyo muingia, hapo ubinaadam na Utu humtoka kabisa, kwaajili ya cheo huwa teyari kufanya lolote kinyume na Ubinaadam na Utu...
kama kungekuwa na cheo kikubwa zaidi ya Urais amini nakwambia Marais wote unao wajua wangekigombania cheo hicho kwa hali na mali.
tuamke kwenye ndoto za kuitegemea serikali kuwa itatusaidia, tuondokane na utumwa wa kifkra na tusikifirie serikali kama chombo ila tuwafikirie viongozi wa serikali kama watu ambao huwa na sifa ya kugeuka na kujigeuza vyovyote watakavyo. tuwekeze nguvu nyingi kwenye kufanya kazi haswa biashara na kilimo, tuondoe dhana kuwa msaada wetu upo kwa serikali.
tusipo kuwa na matumaini makubwa na serikali tutapunguza msongo wa mawazo. afya ya akili inatakiwa kulindwa kwa hali na mali, na chanzo kikubwa cha kulemaa kwa afya ya akili ni kuweka matumaini makubwa kwa kitu ambacho hakina manufaa kitu ambacho muda wowote kinakugeuka na kukufanya chochote kipendavyo.
TUNAKOELEKEA NI KUBAYA ZAIDI,wengi tunategemea Rais afanye chochote ili kuturahisishia maisha yawe mepesi, ndugu zangu mtu yoyote hapa duniani ambae sio Mtu hutafuta nafasi yoyote kwa maslahi yake yeye mwenyewe, Rais amepambania ndoto zake hadi akawa Rais leo aje apambane ili wewe uwe na maisha mazuri kweli hiyo si ni ndoto...? {jukumu la kutengeneza maisha mazuri umelibeba wewe mwenyewe hakuna mtu anaweza kukutengenezea maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe}