Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu ndugu zangu,
Wana JF wenzangu, kuna watu wamekuwa wakijiuliza kwamba inakuaje nchi kama vile Malawi, Kenya, Zambia na kwingineko wapinzani walifanikiwa kushinda chaguzi mbalimbali na kuvitoa vyama tawala katika madaraka, huku kwa Tanzania hilo limeshindikana. Jibu ni kwamba wakati wenzetu walianzisha upinzani kwa lengo la kuikosoa na kuisimamia serikali pale inapofanya mambo ya hovyo kwa wananchi na nchi kwa ujumla.
Kwa Tanzania hali ni tofauti kwa vile vyama hivyo vya upinzani Tanzania vimeanzishwa kwa lengo la kulinda masilahi ya mabwanyenye wachache wa vyama hivyo, vimeanzishwa kwa lengo la kujitafutia kula na kujitajirisha kupitia siasa za hovyo (chukulia ruzuku, makato ya wabunge kwa muda wa miaka 5, michango iliyochangwa ktk uchaguzi mkuu, msaada wa mamilioni ya Sabodo nk), kwa lengo la kuwatetea wahujumu uchumi, wauza unga, wakwepa kodi kwa makubaliano ya kuvilipa vyama hivyo nk. Kwahiyo kwa upinzani wa namna hii ni vigumu sana wananchi wengi kuwaamini na kuwapa kura zao ili waongoze nchi.
Kilichotokea mwaka 2005 kwa viongozi wa upinzani kuingiza majambia nchini, na 2015 viongozi wa upinzani kuuza utu wao, kupoteza heshima zao na kubadili kauli zao kizembe zembe kwa malipo madogo ambayo wengi wameyamalizia kwenye ulevi, ni ushahidi tosha kuwa upinzani wa Tanzania haupo serious kushinda uchaguzi wowote wa uraisi.
Nimerusha Jiwe gizani kwa lengo la kumjua litakae mpata.