kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Viwanda vinahitaji malighafi ya uhakika ili viweze kuzalisha kwa mwaka mzima. Vile vinavyotumia malighafi ya mazao ya kilimo na ufugaji vitahitaji ukulima na ufugaji wa kibiashara unaozingatia wingi na ubora wa mazao.
Duniani kote mashamba makubwa ya kiwekezaji ndiyo yenye sifa ya kutoa ajira nyingi kwa vijana na kuzalisha malighafi zinazolisha viwanda. Tanzania tulikuwa na aina hiyo ya mashamba kule Tanga, Mbeya, Arusha, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Kilimanjaro na kwingineko ambayo yalikuwa na kazi ya kutoa ajira za uhakika na kulisha viwanda na kusafirisha nje. Bahati mbaya "tulikosea" tukayataifisha na baadae tukawapa "matapeli" wayaendeshe.
Sasa hivi kuna wimbi ya kufuta vibari vya plantations hizo na kuwapa akina "Masudi" walime wanachokitaka, wanavyopenda na wanavyoweza. Huku ni kuzidi kuikosea sera ya viwanda, maana mkulima mdogo asiye na pembejeo wala mtaji hawezi kulisha viwanda kwa mwaka mzima. Hivyo tutakuwa na viwanda vya msimu wa miezi 2 au 3 tu kwa mwaka kutokana na ukosefu wa malighafi.
Badala ya kufuta vibari vyao kwa mbwembwe tuwasaidie walipokwama, tuwabembeleze, tuwahimize, tuwape moyo au tutafute wengine wa kuyaendeleza ili yatoe ajira kwa vijana na malighafi kwa viwanda.
Wananchi wanazidi kuongezeka idadi na ardhi haiongezeki. Ardhi haitoshi duniani kote hivyo kilio cha wananchi kudai wapewe plantations hizo sio za msingi kabisa na hazipaswi kupewa kipaumbele kwakuwa sio kila mtanzania atahakikishiwa kupatiwa shamba. Hata huko China, Marekani, Cuba, Zanzibar, Brazil, Ulaya, Kenya, n.k mashamba makubwa sana ya mazao na mifugo yapo ingawa wanachi wengi hawana mashamba yao binafsi. Na hii ndiyo kanuni ya uchumi wa viwanda.
Hata hapa Dar es Salaam pangetosha kulima mashamba makubwa sana kama "vijumba" vyote vilivyojengwa kwa mtawanyiko vingevunjwa na kujengwa maghorofa kwenye wilaya moja tu ya Kinondoni na watu wote wakahamishiwa huko kuishi. Dar es Salaam nzima ingetosha kuishi Kinondoni tu na ardhi nyingine ingetumika kwa viwanda na uzalishaji mwingine. Ardhi yetu inatumika vibaya na kitakuwa chanzo cha umaskini wetu milele kama tukiendelea kuwaza na kutenda kwa namna hii.