Tusiotumia mitandao ya kijamii tujuane!


Mitandao inasaidia Sana ndo maana wewe mwenyewe upo hapa unatumia JF


Hili sio jukwaa ni mtandao wa kijamii ambao unawakutanisha watu pamoja na kutoa mawazo yao , taarifa , fursa , ajira n.k

Kitu ambacho kinawatesa watu weusi ni kuwa na uelewa mdogo katika mambo ya msingi .

Nakumbuka kuna Mwalimu alikuwa anatukana watumiaji wa mitandao na kusahau kuwa kwa sasa kuna walimu Kama yeye they make a lot of money kwa kuuza mawazo yao mitandaoni .

Kwahiyo ikiwa hauelewi mambo haya utahisi Consumers wanakosea n.k

Hakuna anayekosea Ila MTU hufata mambo yanayoendana na akili yake

Wengine husema mitandao ni Kama MTO wapo wanaovua samaki na wapo wanaoliwa na mamba.
 
Umekosea, Social Media na Forum vyote vipo kwenye platform ya mtandao lakini ni tofauti,
Social Media ipo zaidi kwenye maisha binafsi ya watu wakati Forum ipo kwenye mada na mijadala mbali mbali kwa kina,

Kabla hujapinga kitu, fanya kwanza research.
 
Okay 😹
 
Je, JF ni mtandao wa kijamii? Ndiyo na hapana. Ni sehemu ya mitandao ya kijamii.

Features ndiyo zinaamua. Ukitafsiri neno 'social media' unaweza kuona kila kilichopo kwenye Internet kinachowezesha mawasiliano na uwasilishaji taarifa ni mtandao wa kijamii, lakini si hivyo.

JF inafanya nusu ya kinachofanywa na mitandao kama Instagram, X, Threads, TikTok, Bluesky n.k.
 
Umekosea, Social Media na Forum vyote vipo kwenye platform ya mtandao lakini ni tofauti,
Social Media ipo zaidi kwenye maisha binafsi ya watu wakati Forum ipo kwenye mada na mijadala mbali mbali kwa kina,

Kabla hujapinga kitu, fanya kwanza research.
Duh, haya Mkuu
 
Nakubaliana na wewe, ni ngumu kujitenga na mitandao. Ndiyo maana nikaamua kubaki na ile ambayo naweza ku-control taarifa na machapisho ninayotaka kuyaona: JF, Reddit, na YouTube.

Tofauti na hapo,

Instagram wanakulazimisha uone suggested posts, ukienda kwenye explore/search wanakulazimisha uone trending posts.

X (Twitter) nao wanakulazimisha uone trending posts, angalau feature yao ya following (timeline) inafanya kazi vizuri tofauti na Instagram ukiweka timeline ya following bado kuna suggested posts utakuna nazo. Lakini walivyoweka X verified & X payout mtandao umepoteza authenticity, ukifungua comments users waliokuwa verified ndiyo comments zao zinakaa juu na kila mtu ana-post chochote kile ilimradi a-trend, impressions nyingi maana yake anapata pesa kwa ku-tweet tu. Kila mtu anataka kuwa content creator, matokeo yake consumers wanakutana na kila aina ya ujinga.

Mtandao kama JF ni rahisi kusoma kile unachokitaka tu kwasababu ya majukwaa, Reddit nayo unaweza kutengeneza timeline yako pekee kulingana na communities unazozitaka. YouTube yenyewe uki-pause search & watch history hawakuletei recommendations, hivyo utaona videos za channels ulizo-subscribe tu... kwenye desktop version zipo Chrome extension zinazozuia kila kitu.

Mitandao mingi haimpi user uwezo wa ku-filter taarifa ndiyo maana inakuwa rahisi mtumiaji kuwa addicted.
 
Mimi mwenyewe ni mnufaika wa Internet kama Freelance Software Developer & Graphic Designer.

Internet kiujumla ni moja ya tech bora kuwahi kutokea, tatizo langu kubwa ni jinsi social media ilivyo-shift kutoka kwenye lengo kuu na hii imetokea kwasababu social media imekuja kuwa a billion-dollar business, huku addiction, mental health issues zikiongezeka hasa kwa vijana wa 16-24.
 
100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…