Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
TUSIPENDE KUWAHUKUMU WATU TUWANAO WAMEFANIKIWA KAMA HATUJUI KWA NINI WAKO HIVYO KWA NDUGU AU JAMAA ZAO
Wapo watu tunawatazama wamefanikiwa sana katika maisha yao ila ndugu zake wako nyuma sana kimaisha ukamhukumu katika ubaya tu
Yawezekana hata hao wanaolalamika juu ya huyo mtu hata hapo walipofika ni kwa mkono wa huyo mnayemuona hawawasaidii kitu ila kwakuwa hawezi kuyasema mabaya ya ndugu zake amekubali kusemwa vibaya na kutojibu ili kulinda utu wao ndugu zake na aibu ya familia
Yawezekana amewasaidia sana, amejitoa sana kwa hao watu, amefanya mengi mno ila hapewi thamani, hawazalishi wanachopewa wanakula chote na kuomba tena. Walingeuza msaada kuwa haki yao na waipate kwa wakati na kwa kiwango wanachokitaka bila kujali naye kuwa ana majukumu yake, anahitaji kusogea mbali zaidi kwenye matamanio ya familia aliyonayo
Yawezekana mtu huyo alipooa au kuolewa tu aliacha baadhi ya majukumu, au alipambana akawafikisha mahala fulani ila kwa kuendekeza starehe wakafeli shule au kwenye eneo fulani la maisha linalowapelekea waonekane ni watu wanahitaji msaada chanzo ni wao si yeye huyo. Acheni kumhukumu huyo mtu kama hamuijui sababu ya kwa nini hafanyi hivyo, hana uwezo wa kujibu mashambulizi kaamua tu kaa kimya
Kwahiyo, msiwahukumu watu waliofanikiwa kwa aina ya maisha ya ndugu au jamaa zake wanayoyaishi mkahisi anapenda wawe hivyo ila alishafanya sana au alishafanya kwa nafasi yake kwahiyo jukumu lililobaki ni lao si lake.