Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Change inaanza na wewe

Tanzania has reached a tertiary stage stop blaming for the past will not change the current situation

Mabadiliko huanza na wewe kuna mambo mengi ya hovyo kwasasa ambayo ukianza kuchimbua yaliyopita tutabaki tumebung'aa

Yaliyopita sindwele tungange yaliyopo na yajayo vinginevyo tutapiga gwaride

Tushikamane kwa kupigania mfumo wa haki kwa maana haki huinua Taifa. Mithali:14:34
 
Acha bangi zako. Nchi inapaa ki uchumi chini ya mama. shauri yako utaachwa na hili gari la mshahara
 
Sasa tunatokaje hapa,je tuseme bunge,mahakama,sirikali,vyombo vya ulinzi na usalama vimeshikwa na wanamtandao,kama hivyo mbona namna ya kujikwamua kwenye makucha yao ni rahisi iwapo uwanja wa siasa ukaachwa huru?Mbona sheria za hovyo kwa maslahi ya wanamtandao zinaweza kubadilishwa kuleta ufanisi?1.ubunge wa kujua kusoma na kuandika marufuku 2.Kinga za viongozi wa kuletewa na wanamtandao marufuku 3.Ithibati za kuletewa na wanamtandao marufuku.4.Sheria za rasilimaslli za taifa zakuletewa na wanantandao marufuku.Mahakama zakupatiwa majaji na mahakimu wa wanamtanao marufuku.5.Ajira kwenye vyombo vya usalama za kuajiri watu wa tabaka la wanamtandao marufuku.Wadau mambo mengi muda muchache.Ongeza kwa nafasi.
 
JPM tulikosoa sana uongozi wake na kuweka sababu za kitaalamu kabisa hapa. Humphrey Polepole alikuwa ni moja kati ya Trusted Leuitenants wa Mzee JPM. Kuna mengi waliyafanya na Humphrey Polepole endapo tukiweka uchunguzi huru lazima na yeye atafungwa. TANZANIANS ARE NOT READY FOR THIS CONVERSATION.

Namuheshimu sana Mzee Nyerere na mchango wake kwa taifa, lakini sichelei kuyasema makosa yake makubwa ambayo aliyafanya kipindi cha utawala wake. Mengi aliyoyfanya yalileta madhara. ALSO, TANZANIANS ARE NOT READY FOR THIS CONVERSATION.

Kinachoendelea TANGANYIKA kipindi hiki, ni kile ambacho kilitokea mwaka 2016-2020 watu wengi kusema JAKAYA alikuwa ni Raisi Bora kuliko JPM kwasababu tu wengi wetu tulipofushwa hata na yale mazuri aliyoyafanya JPM. Nakumbuka hata alivyongia Samia Suluhu Hassan, wengi wetu walimshabikia mno kwamba nchi inafunguka hata pale alipofanya mabaya na tukasema mapema.

Leo hii ghafla, Mzee JPM amegeuka shujaa. Nafurahi kwasababu WATANGANYIKA wameanza kuona hadi MAZURI YAKE, ila ukweli haubadiliki kwamba aliumiza maelfu ya WATANGANYIKA na kuwaacha kwenye UMASIKINI MKUBWA. Kuna mambo hakutakiwa kuyafanya kama Raisi, hasahasa suala zima la uvunjaji wa sheria.

Binafsi nasema hivi, WATANGANYIKA inabidi tuache kuamini wanasiasa, tusimamie SHERIA, KANUNI na TARATIBU za KITAASISI. Maneno ya mtu hata yawe mazuri vipi yana ukomo kadiri muda unavyobadilika. Tulipofika hapa hakuna Mwana-CCM yoyote yule anayeweza kukimbia kuwajibika. Siyo Nyerere, Siyo Mwinyi, Siyo Mkapa, Siyo Kikwete, Siyo Magufuli,wala Siyo Samia. Sembuse Humphrey Polepole ???
​
 
Nakubaliana na wewe kabisa.

Na msingi mkuu wa yote ukiyosema hapo kuhusu SHERIA, TARATIBU NA KANUNI ni KATIBA MPYA.

Kuna nyuzi nyingi sana nimeliongelea hili ikiwemo kusisitiza umuhimu wa Nchi kupatiwa KATIBA MPYA inayosimika mifumo imara inayosimamiwa na kuangaliana vizuri.

Yanayotokea nchini hapa ni matokeo ya Wanasiasa kuwa juu ya mifumo na matokeo yake kila kitu kinafanywa kwa jicho la kisiasa na kwa manufaa ya Wanasiasa.
 
Unatambua wasifu wa huyo unayemtukana?, vijana wa sasa jifunzeni uungwana
Uzuri wote wanaonitukana mpaka sasa hakuna anayekanusha kwamba nilichokisema kina UKWELI na UHALISIA. Ndiyo hapa narudi kwenye usemi ule-ule, WATANGANYIKA ni watu wepesi mno kuhadaiwa kisiasa. SHERIA na KANUNI ndiyo mwongozo mkuu wa msomi yoyote yule, hasahasa kwenye nyakati hatari kama hizi:

SULUHISHO LA NDUGU HUMPHREY POLEPOLE KWA MATATIZO YA NCHI:
CCM isimruhusu Samia Suluhu kugombea Uraisi a.k.a imwage Oil. CCM ifanye mjadala na CHADEMA na kumtoa Lissu gerezani ndipo tufanye uchaguzi mkuu. Polepole anaamini kwamba CCM kwanza nchi baadaye, yaleyale mawazo ya Mzee Nyerere kwamba CCM IMARA = TANZANIA IMARA

SULUHISHO LA NDUGU TUNDU LISSU KWA MATATIZO YA NCHI:
Tundu Lissu anaamini hivi, KATIBA IMARA = TANZANIA IMARA. Ambapo anasema kabla ya kufanya chochote kile ni lazima nchi ifanye mabadiliko makubwa kisheria na kimfumo.Turekebishe katiba, tuamue hatma ya muungano, tuwe na tume huru, kisha tukafanye uchaguzi mkuu.

HAYA MAWAZO NI MAWILI TOFAUTI, KISHERIA NA KIMATOKEO. Mtu yoyote yule mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo mtambuka kwa kina lazima ataona utofauti. Kuna wengine wanataka tu RAISI SAMIA atoke, akishatoka wao ni CCM kindakindaki. Kuna wengine wanataka RAISI SAMIA atoke, na CCM pia itoke, hawa ni wapinzani kindakindaki wanaotaka dola.

MIMI BINAFSI NAONA JAMBO JEMA NI HILI:
Mabadiliko ya kisheria lazima yafanyike. Wanasiasa wote (CCM + CHADEMA) ni lazima wadhibitiwe ili mambo haya yasije kujirudia hapa TANGANYIKA endapo hata siku CHADEMA wakachukua nchi. Kubwa zaidi, ili kuzuia uvunjifu mkubwa wa haki za raia, unadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ni lazima tuunde TRUTH COMMISSION, ambayo itachunguza maovu ya serikali tokea awamu ya kwanza na kuwajibisha watu.

TRUTH COMMISSION itatusaidia kufanya VICTIM REPARATIONS, jambo ambalo ndiyo msingi mkuu wa taifa lolote lile linalotaka amani ya kisiasa (Transional Justice). Kuna maelfu ya watanganyika wenzetu waliuwawa kikatili, waliwekwa kizuizini, walifutiwa uraia, wakafukuzwa nchi, wakafungwa, wakafilisiwa na hata kuuwawa na serikali chini ya mwamvuli wa UZALENDO. Hawa ni lazima wapewa haki yao, aidha wakiwa hai au wafu.

TRUTH COMMISSION pia itatusaidia kufanya INSTITUTIONAL REFORMS. Vyombo vya kiusalama vitatakiwa kufanyiwa marekebisho ili mwanasiasa yoyote, ikiwemo Tundu Lissu wasije wakajisahau endapo watakuwa ikulu na kugeuka MIUNGU WATU.

MTAZAMO WA MBALI KABISA: Tatizo siyo watu peke yake. Matatizo ya Tanzania hayawezi kumalizwa kwa UCHAGUZI NA TUME HURU peke yake. TATIZO LETU KUBWA ni SHERIA NA MFUMO mbovu uliozalisha TAMADUNI ZA HOVYO ZA KISIASA. Mzee Mkapa alikuwa kiongizi safi wakampa jina MR CLEAN, lakini alifanya mambo mabaya mangapi ???

IFIKE MAHALI TUWE WAELEWA
​
 
Tatizo hata hii Katiba mbovu bado wanavunja.
Naamini hata tukipata mpya wataivunja pia. Kuna kitu lazima kifanyike kuzuia watu wasivunje katiba. Kisha tuunde katiba mpya.
 
Tatizo hata hii Katiba mbovu bado wanavunja.
Naamini hata tukipata mpya wataivunja pia. Kuna kitu lazima kifanyike kuzuia watu wasivunje katiba. Kisha tuunde katiba mpya.
Dawa ya kutovunja katiba ni ndogo sana.

Kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Viongozi wote wa Kisiasa na kuweka makosa ya kukiuka katiba kuwa makosa ya Jinai.

Alafu vyeo vyote vikuu vya kiutendaji unaviwekea ulinzi wa Kikatiba. Wanateuliwa ila hawawezi kutenguliwa.

Mbona simple sana
 
Tatizo la Tanzania siyo KATIBA MPYA tu, bali UTAMADUNI WA UWAJIBIKAJI.

Japo katiba mpya ni hatua ya awali kabisa inayoonyesha utashi wa kisiasa (Political Will). Kwenye mazingira kama yetu, katiba mpya lazima iende sambamba na TRANSITIONAL JUSTICE. Watu waliosababisha KATIBA 1977, kuchokwa ni lazima wawajibishwe, ili wananchi warudishe imani kwenye UTAIFA, DOLA na SERIKALI.

Wewe unafahamu fika kwamba hapa Afrika hakuna nchi iliyokuwa iliyoandaa katiba bora kabisa na kusifiwa duniani kote kama UGANDA. Mzee Musseveni mwaka 1995-1996, alifuata utaratibu mzima wa kisheria wa kuandaa katiba. Ila ukweli ni kwamba leo hii nini kimetokea ??? Katiba mpya bila UWAJIBIKAJI WA KISIASA kwa watu waliohusika kuvunja katiba iliyopita haiwezi kuleta heshima stahiki kwa katiba iliyoandaliwa upya.

NDIYO MAANA, tunaosoma SHERIA tunafundishwa kwamba, mbali na POLITICAL REFORMS kickstarted by CONSTITUTIONAL CHANGES, there has to be Transitional Justice that will ensure continuity and survival not only of a new constitution but peace and a state at large. Machafuko ya kisiasa yakitokea, mbali na katika ni lazima pembeni kuwe na TRANSITIONAL JUSTICE.

TRANSITIONAL JUSTICE huwa na vitu vifuatavyo:
1. Outlining repressions and abuse conducted by State Apparatus.
2. Identifying victims of State Repressions,.
3. Reparations to the victims of abuse.
4. Institional Reforms of State Apparatus.

Sasa hapa unaweza ukafanya TRANSITIONAL JUSTICE kupitia nyenzi zifuatazo:
1. TRUTH COMMISSIONS
2. CRIMINAL TRIBUNALS

Baada ya Raisi Mao Zedong kufariki, Deng Xiaoping na wenzake waliona kabisa Wachina hawana imani na nchi yao. Wakaamua kufanya TRANSITIONAL JUSTICE, ambapo mbali na kuandaa mfumo mpya wa nchi, wahuni wote waliotumiwa na Mao Zedong kuua na kufunga maelfu ya wachina walitiwa nguvuni kwenye mkono wa kisheria. Wengine wakahukumiwa kunyongwa kabisa.

Hili ndilo liliiokoa Uchina na kurudisha heshima kwa katiba, pamoja na imani kwa serikali. Maelfu ya wanasiasa ambao Mao Zedong aliwaua walitajwa majina yao na Serikali ikasema dhahiri kabisa kwamba WALIONEWA kwa kusingiziwa kuwa ni MABEBERU. Wanausalama waliokuwa chini ya Mkurugenzi Muuaji Bwana Kang Sheng waliwajibishwa. Waliopotezwa walikuwa (REHABILITATED).

TAASISI ZA KIUSALAMA za UCHINA zikakataziwa kutumika kisiasa chini ya mtu mmoja hata kama ni Raisi. Lazima utaratibu ufuatwe.
==============================================================
Binafsi kusema TUNAVUNJA SHERIA KWA NIA NJEMA halafu tunakataa kukiri makosa siliafikia na ntalipinga mpaka siku naingia kaburini.
​
 
Mkuu pamoja na andiko lako refu na uzuri fulani, mimi sioni tatizo kwa mtu ambaye ameamua kubadilika na kuuona ukweli na kuamua kuwa upande wa wananchi.

Kina Polepole, Mange, Maria na wengine naona wako sahihi sana kwa wanachotuletea. Unafikiri ni nani aside na mabaya yake ya nyuma ambaye ndiyo atakuwa sahihi akikemea mabaya. Ubaya unatakiwa kukemewa na yesterday bila kumhukumu alifanya nini huko nyuma.

Au mkuu Malcom unataka taifa liendekee tu kuhujumiwa kwakuwa wanaotaka lisihujumiwe walishakuwa na makosa yao nyuma. No kila mtu anayeungana na watanzania wenzake katika kutuonyesha maovu ya viongozi wetu mi namuona ni shujaa sana.
 
Tatizo hatuujui ukweli kwamba wanaofaidika na huu muungano ni sisi huku bara kuliko wao wazenji.

Angalu Jussa na wanaharakati wachache wanaelewa somo kwamba hakuna namna Zanzibar ikasimama katika usawa mmoja na Bara. Cha muhimu kutafuta elimu pana ya namna bara ilivyoimeza Zanzibar kiuhalisia.
 
Mwaka 1975, baada ya IDARA kufanya mauaji makubwa na kuonea raia wake kule kanda ya ziwa, Mzee Nyerere alichukua maamuzi magumu mno. Alifukuza kazi MAAFISA USALAMA kuanzia wakurugenzi waandamizi, WAZIRI OFISI YA RAISI na WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, hadi POLISI.

Mzee Nyerere kurudisha heshima alivunja kabisa IDARA, na kuteua MKURUGENZI msomi DR. Laurent GAMA aiongoze. Tofauti na ule utaratibu wa zamani wa kujaza TANU YOUTH LEAGUE ambao wengi walionekana kuwa THUGGISH and SADDISTIC, kina Dr. Gama waliaenda kufanya En Masse Recruitment mashuleni na vyuo vikuu.

Rucruitment ya 1975, ndiyo ilileta watu kama Membe, Mizengo na wengine ambao binafsi nawafahamu walioenda kupata mafunzo ya kinidhamu nje ya nchi. Walau IDARA iliendeshwa kiheshima, hasahasa baada ya kuona Mzee Emilio Mzena na Mzee Peter Siyovelwa ambao waligeuza IDARA kama mali yao binafsi wametimuliwa. Huyu Siyovelwa siku maafisa wameitwa Ikulu kwenye kikao aliinuka na kuanza kumtolea Mzee Nyerere maneno ya kashfa akimnyooshea kidole na kumwambia "Wewe Julius unahisi hii nchi ni yako peke yako"

Huyu Peter Siyovelwa alikuwa kama mungu-mtu. Ukimuona kwa nje-nje hivi unaweza ukasema ni mtu mwenye bashasha lakini ni moja kati ya watu waliochochea ugomvi baina ya Mzee Nyerere na Mzee Kambona. Ilifika hadi kipindui pale Iringa wakiteua WAKUU WA MIKOA wanawake alikuwa anapiga simu kwa Raisi au Waziri Mkuu, akisema hataki. A Megalomaniac Per Excellance.

SASA WATU AINA HII, ambao wanadhani wanaweza kutoa uhai wa binadamu mwenzao bila kuwajibika ndiyo wamejazana CCM, TISS, TPDF na PT. Wengine hujiita ni WAZALENDO. Ila ukweli ni kwamba MWANADAMU asipowekewa mipaka ndiyo kinatokea kile kilichotokea mwaka 2017 kwa Tundu Lissu.

BOOKMARK THIS: Siku Tundu Lissu anatolewa nje, Amin Amin nawaambia, tutafahamu madhambi mengi ya Ndugu Humphrey Polepole ambayo aliwahi kuyafanya. Pia sidhani kama atakuwa na uwezo wa kujibu hoja za Lissu. Wakati hili linatokea, WATANGANYIKA wengi watakuwa washachagua upande kati ya Lissu au Polepole. SUBIRI UONE
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…